
SERIKALI nchini Swaziland imeziagiza shule zake kufundisha somo la dini ya Kikristo pekee, hatua iliokosolewa na wadau mbalimbali kwa kuwa haiheshimu dini nyengine.
Agizo hilo lilitolewa wiki iliyopita na Wizara ya Elimu nchini humo, ambapo ilipita shuleni ikiwaagiza walimu wakuu wote kuhakikisha mtaala hautaji dini nyingine zaidi ya Kikristo.
Sahid Matsebula, ambaye ni Muislamu anayefanya...