KINGAZI BLOG: 09/05/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 5 September 2016

Download Audio: Dullayo Ft Raymond – Yule Yule

Download Audio: Jux & Vanessa Mdee – JUU (Snippet)

Download Audio: Christina Shusho – Roho


Makubwaaa!!!  Hebu ona picha live KIJANA AJIRUSHA TOKA JUU YA GHOROFA HADI CHINI NA KUPASUKA PASUKA ENEO LA MNAZI MMOJA DAR ES SALAAM





 

KIJANA MMOJA AMBAYE JINA LAKE HALIKUWEZA KUFAHAMIKA KWA HARAKA ,,JANA SIKU YA JUMAPILI ALIJIRUSHA TOKA KATIKA JENGO REFU LILILOKO MAENEO YA MAKUTANO YA BARABARA YA MOROGORO ROAD NA BIBI TITI .HAIKUFAHAMIKA MARA MOJA NINI SABABU ZA KUJIRUSHA KWAKE

HUYU NDIYE MWANAUME ANAYEMKOSESHA USINGIZI SNURA


 

Staa wa Ngoma ya Chura, Snura Mushi, juzikati alieleza jinsi anavyowewesekea penzi la mwanaume ambaye ni staa mwenzake wa Bongo Fleva lakini hakumtaja. Katika pekuapekua, Wikienda limenyaka jina la staa huyo kutoka kwa mtu wa karibu wa Snura ambaye amedai kuwa ni Raymond au Rayvanny wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB).


 Sosi huyo ambaye hakutaka kuchorwa gazetini alidai kuwa, Snura amekuwa karibu na Raymond na ukaribu wao ulizidi baada ya kufanya video ya msanii huyo ya Natafuta Kiki ambapo ndani yake walionesha mambo yao ya chumbani kama mapichapicha yanavyoonesha mitandaoni. “Kama mnakumbuka Snura alitangaza kuwa kati ya majina matano ya wanaume maarufu wa muziki Bongo, yupo mmoja anayemuwewesekea, jina la Raymond lilikiwemo.

“Baada ya video ya Natafuta Kiki, mapichapicha yalianza kumwagwa lakini unaambiwa kuna picha nyingine ambazo haziwezi kuwekwa gazitini kwani ni balaa na kwenye video picha hizo hakuna,” alitonya mnyetishaji huyo. 


Baada ya ubuyu huo kumwagwa juu ya meza ya Wikienda , wanahabari wetu walitinga nyumbani kwa Snura kisha kumuweka mtukati juu ya sakata hilo ambapo mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo; Wikienda:  Snura, picha zako na Raymond zinakuonesha ukijiachia bila masihara, je, kuna nini kinaendelea au nako ni kutafuta kiki? Snura: Hahahaaa… niliamua kufanya kweli kwani mtu anapokupa kazi yake lazima uitendee haki. Kwani kuna ubaya gani? Wikienda: Inasemekana Raymond ndiye yule ambaye wiki kadhaa zilizopita ulisema anakukosesha usingizi na unampenda ndiyo maana hata mabusu yenu ni zaidi ya video na kuna kitu kinaendelea kati yenu, je, nini kinaendelea? Snura:  Mh! Watu wataongea mengi kweli ila ipo siku watamjua ninayemzimikia. Kama ni Raymond nitasema. 

Kwa sasa mimi na Raymond tumefanya video na sijaona la kushangaza. Wikienda: Je, kwa pozi lile mpenzi wako uliyenaye hajakasirika? Snura: Mpenzi? Yupi tena? Mimi niliamua kufanya kweli hakuna wa kuniuliza. Watu wanashangaa pozi hilo? Mbona zipo picha kali kabisa ambazo hata kwenye video hakuna? Sikuona la kushangaza hapo na hakuna wa kunizuia mimi kufanya mambo yangu. Wikienda: Lini utamuweka wazi umpendaye? Snura: Naanza kumuweka wazi hivi karubuni. Nitaanza na mkono, baadaye kiungo kimoja baada ya kingine, mwisho mtamuona, hahahahaa watu wana hamu eee… mbona watamjua tu! Wikienda: Lakini wewe na Raymond inasemekana mna mawasiliano ya ziada kama wapenzi kwani hata picha nyingine mbali na video zinawaonesha mkiwa pamoja, unalizungumziaje hilo? Snura: Mnachimba sana ila ipo siku mtaujua ukweli. Sipendi kutangaza uhusiano mara kwa mara maana mwisho naonekana sifai wakati ninaoingia nao kwenye uhusiano ndiyo hunisaliti na kunishinda. Ila kwa huyu anayekuja, inshallah penzi ni kikohozi kulificha huwezi, kama ni yeye (Raymond) basi mtaujua ukweli.

RAYMOND VIPI? Baada ya Snura kufunguka hayo, mwandishi alimwendea hewani Raymond lakini hakupatikana kwa maelezo kuwa yupo nchini Kenya. Alipotumiwa chatting na Wikienda kupitia WhatsApp kuulizwa ishu hiyo alijibu kwa kifupi: “Jamani nooo…hahaha…ile ni kazi tu, ilibidi tuvae uhusika but nothing else (lakini hakuna kingine chochote).

” NI MWENDELEZO? Kumekuwa na kasumba ya mastaa wa kike wenye umri mkubwa kutoka kimapenzi na vijana wadogo kiumri hivyo wapenda ubuyu wananyetisha kuwa inawezekana Snura anaendeleza kasumba hiyo baada ya Jacqueline Wolper, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, Wema Isaac Sepetu na wengine.

GPL

Wabunge wa Upinzani Kuanza Vikao vya Kutafuta Suluhu na Naibu Spika

Kambi rasmi ya upinzani imepanga kufanya vikao vya kujadili suluhu ya kudumu ya mgogoro na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson uliosababisha wabunge wanaounda Ukawa kususia vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo.

Vikao hivyo vinapangwa kufanyika wakati mkutano wa nne ukianza rasmi kesho, baada ya kuahirishwa mwishoni mwa Juni mwaka huu wakati wa mkutano wa Bajeti. 

Mbunge wa Vunjo (NCCR- Mageuzi), James Mbatia alieleza jana kuwa uamuzi wa kufanya vikao hivyo umefikiwa baada ya upinzani kukaa kikao na viongozi wa dini Agosti 24 mwaka huu ili kutafuta suluhu ya kudumu. 

“Kikao cha kwanza tutakaa kamati ya uongozi ya wabunge wa upinzani kujadili suala hilo na baadaye tutamaliza na kikao cha wabunge wote ili kubaini njia endelevu za kumaliza jambo hilo,”alisema Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi. 

Wabunge wa Ukawa wamekuwa wakisusia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika kwa madai ya kutoridhishwa na uongozi wake tangu Mei mwaka huu, baada ya Dk Tulia kukataa kujadili hoja ya kufukuzwa wanafunzi zaidi ya 8,000 stashahada ya ualimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom). 

Hata wakati wakisubiri kufanyika vikao hivyo ambavyo Mbatia hakutaka kuelezea kwa undani, upinzani ulitangaza kurudi bungeni baada ya mkutano wao na viongozi wa dini. 

Katika mkutano na wanahabari Agosti 25, Mbatia kwa niaba ya vyama vilivyoshiriki mkutano huo wakiwamo ACT-Wazalendo, alisema wangejadiliana namna ya kufanikisha jambo hilo kama sehemu ya kutii ushauri wa viongozi hao wa kiroho. 

Hata hivyo, haijawekwa bayana iwapo kesho Ukawa wataendelea na vikao hata kama Dk Tulia ataendelea kuongoza kiti hicho ama la. 

Mbatia alisema jana kuwa watatoa taarifa rasmi leo namna vikao hivyo vitakavyofanyika na siku husika. 

Kuhusu kupata taarifa ya mwenendo wa mchakato wa kutafuta maridhiano ulioelezwa na Spika Job Ndugai hivi karibuni, Mbatia alisema hawajapata chochote na wao wanasikia kwenye vyombo vya habari kama wengine. 

Alipoulizwa ni lini vikao vya maridhiano kati ya pande hizo yataanza, Ofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya alisema Spika anatarajiwa kufika ofisini leo na kwamba kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo atapanga utaratibu wa namna anavyoona inafaa. 

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Septemba 5

Hizi hapa kwa ufupi habari zilizopewa nafsi ya juu katika magazeti ya Tanzania leo septemba 5 kwenye habari za kitaifa kimataifa na michezo. KARIBU. 


CHECK LIST YA MASTAA AMBAO NI JAMVI LA WAGENI ,WOTE WATAJWA HAPA LIVE


Madai mazito! Kufuatia baadhi ya mastaa wa kike Bongo kuwa na tabia kila anapokuja staa wa nje kwa ajili ya kupafomu au mwanaume mwenye fedha kufanya jitihada za kumnasa kimapenzi, wanadaiwa kuwa ni ‘jamvi la wageni’ kwa kile kinachosemekana kuwa huwa wanajilengesha wenyewe, Wikienda lina listi kamili.

 Chanzo makini kimelidokeza Wikienda kuwa baadhi ya mastaa hao wamekuwa wakijilegeza kutoa penzi kwa mastaa wanaotoka nje ya nchi kwa sababu tofauti. Wengine wanaamini ni kupata umaarufu. Wengine kupata mkwanja mrefu kuliko wanaume wa hapa nyumbani na kuna wanaotaka ‘koneksheni’ za nje ya nchi. “Kiukweli Gazeti la Wikienda tunajua ninyi huwa hamuogopi kusema. Yaani hawa mastaa wa kike wamekuwa ni jamvi la wageni maana kila staa wa nje anayekuja Bongo lazima utasikia amelala na huyu mara yule, jambo ambalo linatupotezea sifa kwani tunaonekana ni washamba wanaopenda kushobokea mapenzi,” kilisema chanzo hicho na kuanika listi kamili. Bila kupepesa, chanzo hicho kilisema kuwa kuna mastaa kibao waliowahi kutajwa kwenye skendo ya kulala na staa wa nje aliyetua nchini au wanaume mapedeshee wanaotua nchini. 

LISTI KAMILI “Nawasaidia listi. Yumo Gigy Money (video queen wa Bongo, Gift Stanford) ambaye alidaiwa kulala hotelini na Mwanamuziki wa  Nigeria, Tekno Miles. “Listi nyingine ni Linah na Wizkid (alipotua mwaka jana), Shilole na Wizkid (mwaka huu), Masogange na yule mwanaume raia wa Uganda, Wema na Mshiriki wa BBA, raia wa Nigeria, Luis Mnana, Amber Lulu na Run Town na wengine wengi kama akina Wolper, Jini Kabula, Mary Mawigi, Kidoa na Lulu Diva,” kilidai chanzo hicho. Baada ya kumwagiwa ubuyu huo mzito, Wikienda lilizungumza na baadhi ya mastaa hao kuhusiana na suala hilo ambapo kila mmoja alikuwa na lake la kuzungumza. Gigy Money: “Siyo kwamba tunawashobokea hao wanaume bali mastaa wa nje ndiyo wanaotushobokea wenyewe kwa sababu mademu wa Bongo ni wazuri. Nilipolala na Tekno walinitafuta wao wenyewe. Kitu kingine hawa Wanigeria wanajua kujali sana wanawake. Pia wanaume wa kutoka nje ya Bongo wanatoa fedha nzuri na ya maana siyo kama Wabongo.” Amber Lulu: “Wanaume mastaa wa nje wanajali sana wanawake kwa kweli na wanatoa fedha nzuri siyo kama wanaume wa Bongo ambao hawako romantic ndiyo maana tunawashobokea. Nimewahi kuwa kimapenzi na staa anayejulikana kwa jina la Run Town, nili-enjoy mno.” Mary Mawigi: “Mapenzi ni popote, unaweza ukampenda yeyote hiyo ni hali ya kawaida tu haijalishi yukoje.”

MWANAMKE ALIYEBADILI JINSIA NA KUWA MWANAUME AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME

Mwanaume mmoja aliyebadili jinsia ni wa kwanza barani Ulaya kujifungua mtoto baada ya kuwa mjamzito kwa njia ya kupandikiziwa mbegu za kiume. 

Mwanaume huyo ambaye hakutajwa jina, ambaye alizaliwa mwanamke, alijifungua mtoto wa kiume nyumbani kwa msaada wa mkunga katika wilaya masikini ya Neukoellin ya mjini Berlin. 

Alisisitiza kujifungulia nyumbani sababu alikataa kuorodheshwa kama mama kwenye nyaraka zozote za hospitali - hitaji la kisheria nchini Ujerumani. Baba huyo, ambaye alibakisha viungo vya uzazi vya mwanamke, amekuwa akifanyiwa tiba za kubadilishwa homoni kwa miaka kadhaa kubadili jinsia.


Habari zaidi kuhusu upandikizwaji mbegu au taarifa za uhusiano wowote zimehifadhiwa kutolewa hadharani kutokana na baba huyo kutaka kumlinda mtoto wake huyo.

Rasmi mtoto huyo, ambaye alizaliwa Machi 18, hana mama, ana baba pekee.

Msemaji wa Mambo na Ndani wa Berlin alisema: "Mtu huyo aliyezusha maswali hakutaka kujitokeza kama mama ila baba kwenye cheti cha kuzaliwa na matakwa hayo yameheshimiwa."

Baba huyo mtarajiwa pia alitaka kwamba jinsia ya mtoto huyo 'isifichuliwe kwa namna yoyote'. Lakini mamlaka zilipuuza hilo na kutangaza kuwa ni wa kiume.

Vyombo vya habari vya Ujerumani viliibuka kwa namna ya kushangaza katika habari ya uzazi huo wa kubadili jinsia.

'Baby belly instead of a beer belly!' (Kitambi mtoto badala ya kitambi bia!") kilikuwa moja ya vichwa vingi vya habari kwenye magazeti ya Ujerumani yakiripoti kuzaliwa kwa mtoto huyo.

Wakati huohuo, Falko Liecke, diwani wa wilaya hiyo ambako mtoto huyo alizaliwa, alisema: "Hiki ni kitu ambacho sikuwahi kusikia maishani ana kushuhudia."

Mwaka 2011 Mahakama Kuu ya Ujerumani iliamuru kwamba mtu binafsi hatakiwi kuondolewa viungo vyake vya uzazi awe mwanamke au mwanaume 'kupata kutambuliwa hadharani kisheria kwa jinsia atakayowekewa'.

Ndio maana baba huyo wa mtoto wa hivi karibuni amekuwa mwanaume wakati akiendelea kuwa na viungo vyake vya uzazi vya kike.

Dk Tobias Pottek wa Hospitali ya Asklepios West mjini Hamburg alisema: "Hata kama mwanamke anataka kuishi kama mwanaume na kuwekewa homoni kuotesha ndevu, kwa kuwa mji wa mimba na mayai bado yapo, pia inawezekana kupata ujauzito.

Hili ni jambo la kwanza la mtoto kuzaliwa barani Ulaya wa mzazi aliyebadili jinsia, lakini katika Marekani jambo la Thomas Beatie, mwanaume aliyebadili jinsia ambaye alikuwa na watoto watatu, linafahamika mno.

Beatie alikuwa akidai talaka kutoka kwa mkewe, lakini alikataliwa sababu jaji hakuweza kuthibitisha kama alikuwa mwanaume wakati akifunga ndoa.

Jaji huyo aliamua hakukuwa na mamlaka ya kisheria ya kuomba talaka kama ndoa hiyo haikuwa ikitambuliwa.

MAAJABU MAITI ZAFUKULIWA NA KUBALISHWA NGUO KISHA KUZIKWA TENA


Nchini indonesia katika kijiji cha Tana Toraja, maiti huwa zinafufuliwa na Kubadilishwa nguo, zoezi hili hufanyika kila mwaka baada ya maiti kuzikwa, na wanafamilia ndio huifanya kai iyo;

Mara nyingi mtu anapo kufa huwa wanamzika katika sehemu aliyo zaliwa na sio aliyokufia so kila baada ya mwaka humfukua na kumbadilisha mavazi, hii ni moja kati ya mila zao wenyewe:

Duuh hii nouma sana mimi kwa hapo neno sina khaa!!!

 

Gallery

Popular Posts

About Us