CHECK LIST YA MASTAA AMBAO NI JAMVI LA WAGENI ,WOTE WATAJWA HAPA LIVE | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 5 September 2016

CHECK LIST YA MASTAA AMBAO NI JAMVI LA WAGENI ,WOTE WATAJWA HAPA LIVE


Madai mazito! Kufuatia baadhi ya mastaa wa kike Bongo kuwa na tabia kila anapokuja staa wa nje kwa ajili ya kupafomu au mwanaume mwenye fedha kufanya jitihada za kumnasa kimapenzi, wanadaiwa kuwa ni ‘jamvi la wageni’ kwa kile kinachosemekana kuwa huwa wanajilengesha wenyewe, Wikienda lina listi kamili.

 Chanzo makini kimelidokeza Wikienda kuwa baadhi ya mastaa hao wamekuwa wakijilegeza kutoa penzi kwa mastaa wanaotoka nje ya nchi kwa sababu tofauti. Wengine wanaamini ni kupata umaarufu. Wengine kupata mkwanja mrefu kuliko wanaume wa hapa nyumbani na kuna wanaotaka ‘koneksheni’ za nje ya nchi. “Kiukweli Gazeti la Wikienda tunajua ninyi huwa hamuogopi kusema. Yaani hawa mastaa wa kike wamekuwa ni jamvi la wageni maana kila staa wa nje anayekuja Bongo lazima utasikia amelala na huyu mara yule, jambo ambalo linatupotezea sifa kwani tunaonekana ni washamba wanaopenda kushobokea mapenzi,” kilisema chanzo hicho na kuanika listi kamili. Bila kupepesa, chanzo hicho kilisema kuwa kuna mastaa kibao waliowahi kutajwa kwenye skendo ya kulala na staa wa nje aliyetua nchini au wanaume mapedeshee wanaotua nchini. 

LISTI KAMILI “Nawasaidia listi. Yumo Gigy Money (video queen wa Bongo, Gift Stanford) ambaye alidaiwa kulala hotelini na Mwanamuziki wa  Nigeria, Tekno Miles. “Listi nyingine ni Linah na Wizkid (alipotua mwaka jana), Shilole na Wizkid (mwaka huu), Masogange na yule mwanaume raia wa Uganda, Wema na Mshiriki wa BBA, raia wa Nigeria, Luis Mnana, Amber Lulu na Run Town na wengine wengi kama akina Wolper, Jini Kabula, Mary Mawigi, Kidoa na Lulu Diva,” kilidai chanzo hicho. Baada ya kumwagiwa ubuyu huo mzito, Wikienda lilizungumza na baadhi ya mastaa hao kuhusiana na suala hilo ambapo kila mmoja alikuwa na lake la kuzungumza. Gigy Money: “Siyo kwamba tunawashobokea hao wanaume bali mastaa wa nje ndiyo wanaotushobokea wenyewe kwa sababu mademu wa Bongo ni wazuri. Nilipolala na Tekno walinitafuta wao wenyewe. Kitu kingine hawa Wanigeria wanajua kujali sana wanawake. Pia wanaume wa kutoka nje ya Bongo wanatoa fedha nzuri na ya maana siyo kama Wabongo.” Amber Lulu: “Wanaume mastaa wa nje wanajali sana wanawake kwa kweli na wanatoa fedha nzuri siyo kama wanaume wa Bongo ambao hawako romantic ndiyo maana tunawashobokea. Nimewahi kuwa kimapenzi na staa anayejulikana kwa jina la Run Town, nili-enjoy mno.” Mary Mawigi: “Mapenzi ni popote, unaweza ukampenda yeyote hiyo ni hali ya kawaida tu haijalishi yukoje.”

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us