KINGAZI BLOG: 12/05/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 5 December 2016

Official Music (Video) [ Vanessa Mdee - Cash Madam ] Mp4 Download


Official Music (Video) [ Vanessa Mdee - Cash Madam ] Mp4 Download






Picha: Jay Z asherehekea miaka 47 ya kuzaliwa na familia

 Rapper nguli na tajiri wa nchini Marekani, Jay Z, Jumapili, December 4, alitimiza umri wa miaka 47.

Hitmaker huyo wa Empire State Of Mind alisherehekea siku hiyo muhimu pamoja na familia na watu wake wa karibu kwa dinner maalum usiku wa Jumamosi huko Los Angeles. Kelly Rowland na Tina Knowles, mama yake Beyonce walikuwa sehemu ya wageni.


 Kelly Rowland na mume wake, Tim Witherspoon walikuwa miongoni mwa mastaa waliohudhuria sherehe hiyo

Jay Z na Beyonce, wanaopenda kufanya mambo yao kwa faragha, walilazimika kufunika mgahawa walioutumia kwa maturubai ili wasionekane kwa nje.


Mama mkwe wa Jay Z, Tina Knowles akiwa na mume wake mpya, Richard Lawson

ZARI AMEJIFUNGUA?? DIAMOND AMEANDIKA HAYA AKIWA SAFARI KWENDA SOUTH.

Diamond Platnumz weekend hii amepost picha instagram akiwa safarini na Mama yake kuelekea Afrika Kusini huku kwenye picha hiyo akiwa ameandika ujumbe ambao unaonyesha huwenda mpenzi wake Zari amejifungua.

Mapema mwezi uliopita katika hatua za kujiandaa na mapokezi ya mtoto huyo, Zari alifanya baby shower nchini Afrika Kusini na kuwashirikisha marafiki zake na watu wa karibu.

Jumapili hii Diamond akiwa safarini na mama yake kwenda Afrika Kusini, ameandika :

Na mama Chibu D Chibu De … flying to our new Second home, South africa For my New Born… #MiniMe #ChibuJunior #YoungSimba #YoungLion Ungependa nimpe jinangani eti?


Kama Zari amejifungua basi huyo ni mtoto wake wa pili na Diamond. Pia atakuwa mtoto wake wa tano kwa ujumla.

Mchezaji wa Mbao FC afariki baada ya kugongana na mchezaji wa Mwadui FC

Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao FC U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki  Dunia jana jioni  baada ya kuanguka uwanjani Kaitaba wakati wa mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui FC ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana.

Ismail Khalfan  alifariki baada ya kufikishwa Hospitali ya Serikali ya mjini Bukoba.

Ismail Khalfan kabla ya kufikiwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na bao la pili lilifungwa kwa mkwaju wa Penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2-0.

Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui FC  na baadae akiwa peke yake alianguka chini lakini akainuka halafu akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa katika Uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa kwenye gari la zima moto na kupelekwa hospital ambapo mauti yalimkuta.



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Disemba 5

 

Gallery

Popular Posts

About Us