Rapper nguli na tajiri wa nchini Marekani, Jay Z, Jumapili, December 4, alitimiza umri wa miaka 47.
Hitmaker huyo wa Empire State Of Mind alisherehekea siku hiyo muhimu pamoja na familia na watu wake wa karibu kwa dinner maalum usiku wa Jumamosi huko Los Angeles. Kelly Rowland na Tina Knowles, mama yake Beyonce walikuwa sehemu ya wageni.
Kelly Rowland na mume wake, Tim Witherspoon walikuwa miongoni mwa mastaa waliohudhuria sherehe hiyo
Jay Z na Beyonce, wanaopenda kufanya mambo yao kwa faragha, walilazimika kufunika mgahawa walioutumia kwa maturubai ili wasionekane kwa nje.
Mama mkwe wa Jay Z, Tina Knowles akiwa na mume wake mpya, Richard Lawson
0 comments:
POST A COMMENT