Wiki chache baada ya kutokea kwa stori za ‘Scorpion’ ambaye alizichukua headlines kutokana na kuhusishwa kwake na matukio ya uporaji na kuwadhuru watu kadhaa kwenye maeneo ya Buguruni Jijini Dar es salaam, Leo Heka Heka ya Clouds FM imekuja na stori nyingine ya Rambo mkata mapanga.
Geah Habib kupitia Leo Tena ameipata stori hii ya jamaa anayefahamika kwa jina la Rambo kutoka maeneo ya Karakata, Uwanja wa Ndege Dar es salaam. Huyu jamaa inadaiwa kuwa amekuwa na tabia ya kuwapora watu na wengine kuwakata mapanga.
Wananchi wa maeneo hayo wamezungumzia vitisho ambavyo wamekuwa wakivipata kutoka kwa Rambo ambaye aliwahi kufungwa jela na kuachiwa wiki mbili mpaka tatu zilizopita. Wanawake wengi wameonesha kumuogopa Rambo kwa madai kwamba anaweza kuwadhuru kwasababu hata wanaume zao wamekuwa wakihofia kurudi nyumbani inapotokea wamechelewa kurudi au wanarudi mapema ili kumkwepa.
"Yule mtu alifanya fujo mtaani akakamatwa, tangu kipindi cha Kova, walimweka ndani lakini wamemuachia tena amerudi kutunyanyasa tena wananchi. Sisi tunailaumu serikali kwanini wamemuachia, mtu amechoma watu visu, amekata wanawake matiti, wanaume wenyewe wanamuogopa"- Mwananchi
"Huyu Rambo ni shida na alianza haya mambo kitambo kidogo alikuwa anakata watu mapanga kweli alikamatwa na polisi akapelekwa mahakamani akahukumiwa kifungo. Lakini baadaye walikata rufaa akatolewa jela. Baada ya kutoka jela akavamia watu akawakata mapanga watu eneo la shule ya msingi Muhogo akachukua simu akaondoka nayo" – Diwani wa Sitaki Shari.
SOURCE:MUUNGWANA BLOG