Nyuma ya Pazia kifo cha Mume wa Zari | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 27 May 2017

Nyuma ya Pazia kifo cha Mume wa Zari

 KAMPALA: Kifo cha aliyekuwa mume wa staa wa Uganda na Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Tycoon Ivan Semwanga ‘The Don’, raia wa Uganda, mwenye maskani yake Johannesburg na Pretoria, Afrika Kusini, kimeibua simulizi nzito nyuma ya pazia.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya familia ya Ivan iliyopo Muyenga jijini Kampala, kilichokaririwa na mitandao ya kuaminika nchini Uganda, katika siku za mwisho za maisha yake kabla ya kuripotiwa kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo ambao kitaalam huitwa Coronary Artery Disease (CAD). Ilifahamika kuwa, ugonjwa huo ndiyo uliomsababishia kifo usiku wa kuamkia juzi.

Habari zilieleza kuwa, Ivan alionekana kwa mara ya mwisho kwenye Pati ya Blankets and Wine iliyofanyika huko Kampala, Uganda wiki mbili zilizopita. Ilielezwa kuwa, rais huyo wa Kundi la Rich Gang, mwenye umri wa miaka 39, alionekana aliyedhoofu na asiyekuwa na furaha kama kawaida yake huku akinywa soda na kula samaki, tofauti na alivyozoeleka kuwa ni mtu wa kupiga vinywaji vikali, tena vya bei mbaya. “Nyuma ya hali yake kiafya alionekana dhahiri mwenye matatizo yaliyosababisha hata kula yake kuwa ya kusuasua na kusababisha hali kuwa mbaya zaidi,” kilikaririwa chanzo hicho.

CHANZO CHA UGONJWA

Chanzo hicho kilidai kuwa, chanzo cha Ivan kupatwa na ugonjwa huo ni pale alipotokea Sauzi na kwenda kuangalia moja ya mali zake (mashamba makubwa) zilizopo Kampala na kukuta kuna watu wamebadilisha umiliki bila yeye kujua. Ilisemekana kuwa, kuna wakazi waliotengeneza nyaraka na hati za kumiliki ardhi ya jamaa huyo ambayo ilionesha walikuwa wamiliki wapya ilihali ni mali ya jamaa huyo.

Wakati watu hao wakifanya hivyo, Ivan hakujua kilichokuwa kikiendelea. Ilielezwa kwamba, ishu hiyo ilimsababishia Ivan mshtuko wa moyo na maumivu makali ya kichwa ambayo pia yaliathiri utendaji wake wa kazi wa kila siku.

Mbali na hilo, pia, kuliibuka taarifa za kuuzwa kwa nyumba yake na watu wasiojulikana ambapo alitumia nguvu kubwa kukanusha taarifa hizo na kueleza kuwa kwa utajiri alionao hawezi kuuza nyumba yake ya kifahari iliyopo Munyonyo, Kampala.

“Mwishowe, alipoona hali yake kiafya inakuwa mbaya kutokana na mshtuko uliotokana na mambo hayo, Ivan alichukua ndege na kwenda Afrika Kusini kisha kuripoti mwenyewe katika Hospitali ya Steve Biko Academy iliyopo Pretoria. “Vipimo vilionesha kuwa alipatwa na mshtuko wa moyo ambao ulisababishwa na kuganda kwa damu kwenye mishipa,” alisema sosi huyo wa jijini Kampala. Mwishoni mwa wiki iliyopita, baba huyo wa watoto watatu aliozaa na Zari alielezwa kuwa hali yake ilizidi kuwa mbaya zaidi hivyo kufanyiwa operesheni kubwa ya kichwa.

ZARI ATHIBITISHA

Kupitia ukurasa wake Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Zari alithibitisha kifo cha mumewe ambapo aliandika
waraka wa simanzi: “Mungu huwapenda wale ambao ni maalum kwake ndivyo ulivyokuwa, umewagusa na kuwasaidia maelfu, ulifanya mengi ya kushangaza na nakumbuka maneno yako ‘maisha ni mafupi mno, acha tuishi kwa ukamilifu’. Hii ni saa ya giza, sasa naelewa kwa nini ulikuwa ukisema maneno hayo kwangu. “Kwa wanao, umekuwa shujaa -aina fulani ya superman. Mtu yeyote ambaye amewahi kuwa karibu yako anajua wewe ni mtu wa aina gani, anajua ucheshi wako.

Watu watakumisi na kukumbuka sana kwa namna nyingi…Ulikuwa IVAN DON.

Baadhi ya mastaa wa Uganda walieleza ni namna gani walivyoshtushwa na kifo cha Ivan. Bebe Cool –Natoa rambirambi zangu za dhati kwake na familia yake. RIP kaka IVAN. Jose Chameleone -Mungu anaumba na kuchukua kilicho chake! Mungu akurehemu rafiki yangu na kuimarisha familia yako na sisi rafiki zako. Pumzika kwa amani Ivan. Ed Cheune –Ulieneza furaha miaka yote ulipokuwa nasi wote, sasa ni zamu ya Mungu kukupa furaha yote katika kurudi kwako kwake.

Pumzika kwa amani ndugu yangu mpendwa Ivan Semwanga. Baadhi ya mastaa wa Kibongo walioandika mitandaoni kumlilia Ivan ni pamoja na Wema Isaac Sepetu, Emmanuel Mbasha, Ali Kiba, Ester Kiama, Shilole na wengine wengi kutokana na ukaribu wake na wao. Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, bado utaratibu wa mazishi ulikuwa haujawekwa wazi. Ivan alipata umaarufu Afrika Mashariki kutokana na biashara zake kubwa ikiwemo umiliki wa vyuo mbalimbali nchini Afrika Kusini huku akisifika kwa kusaidia shughuli za kijamii nchini Uganda.


google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us