Saturday, 29 April 2017
Mtoto wa Mwakyembe Apachikwa Ujauzito
Vitendo vya wanafunzi kupewa mimba vinazidi kuendelea ambapo Leah Mwakyembe (15), mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Ikimba na mkazi wa Kata ya Ikimba wilayani Kyela, Mkoa wa Mbeya, anadaiwa kupewa ujauzito.
Mkuu wa Shule hiyo Zawadi Mpunji, alisema alifuatwa na baba mzazi wa mwanafunzi huyo, Abdalah Mwakyembe, akidai ana hofu kuwa mwanawe ana ujauzito ambapo mikakati ya kupima ilifanyika.
Alisema baada ya kumwita shuleni mwanafunzi huyo ambaye inadaiwa alianza utoro siku nyingi, ikabidi wampeleke hospitali ya Wilaya na kubainika kuwa ana ujauzito wa miezi minne na kuwa ilibidi bodi ya shule waandike barua kuhusu taarifa za mwanafunzi huyo, nakala ikapewa serikali ya kijiji na ofisi ya elimu.
Alisema yeye kama mkuu wa shule amekamilisha taratibu za kishule na kumfukuza rasmi mwanafunzi huyo na kuiachia serikali kuendelea na taratibu nyingine za kisheria.
Baba mzazi wa mtoto huyo, Abdalah Mwakyembe, alisema mwanawe alikuwa mzuri kitaaluma na kuanza kushuka ghafla, huku akiwa mtoro. Ilifika hatua anaficha nguo za shule kwenye mashamba ya migomba na kusingizia hana nguo na alipobaini alitoa ripoti shuleni.
Afisa Mtendaji wa Kata hiyo Stephen John, amethibitisha kuwapo kwa taarifa hiyo na kusema wamekamilisha taratibu zote na kukabidhi ripoti kwa afisa elimu na kwa Jeshi la Polisi wilayani humo kwa hatua za kisheria.
Alisema juhudi za kumpata mwanaume aliyempa ujauzito ili achukuliwe hatua bado hazijazaa matunda, baada ya mwanafunzi huyo kutotoa ushirikiano wa kumtaja ambapo awali alipohojiwa alimtaja mfanyabiashara wa viatu, na baada ya kumfuatilia ilibainika kuwa anadanganya.
CREDIT: MTANZANIA
KIMENUKAA..Rais Magufuli Ayanyooshea Kidole Makampuni ya Simu..Adai Dawa Yao Iko jikoni inachemka!
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametahadharisha kuwa, wapo mbioni kuhakikisha mapato ya serikali yanadhibitiwa zaidi ili taifa liweze kujitegemea kikamilifu, huku akionya makampuni ya simu nchini.
Rais Magufuli ameyasema hayo Ijumaa hii, mjini Dodoma wakati akikabidhiwa taarifa ya vyeti feki. Rais ameyaonya makampuni hayo, akisema, dawa ya makampuni hayo bado inatengenezwa.
“Bado kuna maeneo mengi ambayo tunaibiwa fedha. Kwenye haya makampuni ya simu haya, yanafanya transactions nyingi lakini hela haziingii serikalini, dawa yao tunaitengeneza baada ya muda mfupi kidogo itakamilika,” alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa.
Amber Lulu: Hata Kichaa Natembea Naye, Kikubwa..
MODO ‘aliyepinda’ Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ amefunguka kuwa, yeye linapokuja suala la kuchagua mwanaume wa kuwa naye kimapenzi wala hachagui, anachoangalia ni kuridhishwa faragha.
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Amber Lulu alisema kuwa watu wengi wanadhani ili mwanamke ayafurahie mapenzi lazima awe na mpenzi mwenye mali nyingi au anayemiliki magari ya kifahari wakati kwake yeye ni tofauti.
“Mimi naweza kutembea hata na kichaa, kikubwa awe anajua ‘kuu-take care’ (kuuhudumia) msambwanda wangu, lakini pia mwanaume wa kuwa na mimi kikubwa ajue kunipa furaha, haijalishi ni mtu wa aina gani, yaani hata chizi,” alisema Amber Lulu.
Mrembo Rayuu Afungukia Kuhusu ndoa yake Kuvunjika
BAADA ya madai kuzagaa kuwa ndoa yake imevunjika, msanii wa filamu Bongo, Alice Bagenzi ‘Rayuu’ ameibuka na kueleza kuwa madai hayo yametokana na watu waliozoea kuona akimuuzisha sura mumewe mtandaoni lakini ameamua kusitisha tu na siyo kwamba ndoa haipo.
Akipiga stori na chanzo chetu, Rayuu alisema, awali alikuwa anapenda kumuanika mumewe kwenye mitandao ya kijamii lakini kutokana na maneno ya hapa na pale ya watu wasioitakia mema ndoa yake akaona bora asimuweke lakini ndoa yao ipo imara na hawafi kirii kuachana.
“Naweza kusema hii ndoa imenikuza, kwa maneno ya watu nimejifunza mengi kwenye hii dunia yaani utoto wote umeisha, wengi wanajadili kuwa tumeachana sababu hawaoni nikimuweka kwenye mitandao kama mwanzo, kwani nimegundua hakuna faida bali ni kujiletea matatizo yanayoweza kuvunja ndoa, japo kukosana ni kawaida kwenye mapenzi,” alisema.