Wednesday, 26 October 2016
BODI YA MIKOPO: WANAFUNZI WAPYA 20,183 WAMEPANGIWA MIKOPO KATI YA 88,163 WALIOOMBA KUPEWA MKOPO.
Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:
I. Vipaumbele vya kitaifa vinavyoendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.
i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa viungo 118
o Wadahiliwa wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali 87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine 9,867
Jumla 20,183
Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.
Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
List of first year students who have been Re-allocated to Bsc.Education in Sokoine university
The following students have been re-allocated to BSc. Education, the program for which they were earlier selected by TCU. Those who have been given accommodation at the Main Campus will need to report to SUASAB in order to be moved to new accommodation at Solomon Mahlangu Campus (SMC). CLICK HERE TO SEE YOUR NAMES
List of first year Continous students of University of Dar es salaam who have been allocated to loans in 2016/17
Wizara ya Mikopo Chuo Kikuu Dar es salaam imekuwa ikifuatilia malipo ya fedha mbali mbali kwa wanafunzi na inawatangazia wanafunzi wote kuwa mnaombwa leo mpaka kufikia
saa 4 subuhi muwe mmeangalia mpangilio wa majina yenu na namba ya kusaini iliyopo kwenye karatasi za malipo ya Mafunzo kwa Vitendo na mgawanyo wa malipo ya fedha za kujikimu pamoja na ada kwa mwaka mzima ambazo zilibandikwa wiki iliyopita kwani muda huo ukifika tutaondoa karatasi zote na kubandika karatasi zifuatazo:
1. karatasi za malipo ya malazi na chakula kwa wanafunzi wanaoendelea.
2. Malipo ya ada kwa awamu ya kwanza na ya pili kwa Ndaki, Shule na Taasisi mbalimbali kwa wanafunzi wanaoendelea.
3. Malipo ya fedha za Mafunzo kwa Vitendo kwa wanafunzi wanaoendelea ambao hawakupata fedha zao (CoHU na SJMC).
MAJINA YOTE YANAPATIKANA
http://Updatesudsm.weebly.com
Pia, Wizara inawakumbusha wanafunzi wanaoedelea kwenda kusaini fedha za Mafunzo kwa Vitendo ambazo ziliingizwa kwenye akaunti za wanafunzi kipindi cha mafunzo hayo; Karatasi zimeshabandikwa muda mrefu sana na leo zitaondolewa ili kupisha karatasi za malipo mengine zibandikwe. Mwanafunzi yoyote ambae hatasaini karatasi za malipo hayo, atafungiwa mkopo wake mara moja na atalazimika kurudisha fedha zote alizopokea kwa kipindi chote cha nyuma mara tu baada ya kufungiwa mkopo huo.
Wizara ya Mikopo imepanga kufuatilia mambo yafuatayo siku ya kesho na tutarudisha mrejesho.
1. Malipo yote ambayo hayajafanyika mpaka sasa mfano fedha ya Mafunzo kwa Vitendo na mengine
2. Karatasi zilizobaki za wanafunzi wanaoendelea (CONTINOUS STUDENTS) za malipo yote na karatasi hazijafika kwasababu matokeo yao yalikuwa hayajapelekwa Bodi ya Mikopo kwakuwa walifanya mitihani ya sapu ama mitihani maalumu.
3. Uongezaji wa majina mengine ya mwaka wa kwanza kwani mpaka sasa bado hayajafikia lengo yaani majina ni machache
4: Karatasi za mgawanyo wa fedha za kujikimu na ada kwa mwaka wa kwanza
5. Kuhusu suala la usainishaji wa karatasi zenye malipo ya fedha za chakula na kujikimu na kutumia kitambulisho kipya, bado tunawasiliana na utawala ili tutumie vitambulisho vya zamani na vitambulisho vya muda kwa pamoja kama vitambulisho vya kusainia kwani mpaka sasa hakuna vitambulisho vipya vilivyotolewa (hili litafuatiliwa kwa haraka sana leo hii)
Pia Wizara ya Mikopo inashukuru kwa ushirikiano wenu na kuwa wavumilivu kwa kipindi kigumu kilichotokea pia shukrani sana kwa viongozi wote tulioshirikiana katika kuwatetea mwaka wa kwanza; Ofisi ya Rais DARUSO, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Spika DARUSO, Muhimili wa Mahakama DARUSO na Wanafunzi wote kwa ujumla
MUHIMU
Usainishaji wa karatasi za Mafunzo kwa Vitendo utafanyika kwa KITAMBULISHO CHA ZAMANI
Imetolewa na Wizara ya Mikopo kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano, Mambo ya Nje na Jumuiya za Wanafunzi.
Kasunzu Eliud Apolinary
0658202828
Mahmud Abdul Nondo
0656366125
Makupa Erick Christian
0655191254
casfr_meals_and_accomodarion-1.pdf |
casfr_meals_and_accomodarion.pdf |
iks_meals_and_accomodation.pdf |
pt_sjmc.pdf |
ids_meals_and_accomodation..pdf |
coict_meals_and_accomodation_2.pdf |
Here is Sheila Mwanyigha's last moment with Achieng Abura, She is a true friend indeed
Rais Magufuli Ateuliwa kuwania tuzo ya Forbes kwa watu maarufu barani Afrika
Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameingia katika listi ya watu ambao wametajwa kuwania tuzo ya Person Of The Year 2016 ambayo hutolewa na Jarida la Forbes Africa.
Rais Magufuli ameingia katika kinyang’anyio hicho, akiwania tuzo hiyo pamoja na Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel le Roux, Thuli Madonsela, Ameenah Gurib na watu wa Rwanda.
Kama Rais Magufuli atafanikiwa kushinda tuzo hiyo, basi Tanzania itakuwa imepata tuzo hiyo kwa mara ya pili mfululizo kwani mwaka jana 2015, mshindi wa tuzo hiyo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji.
Utaratibu wa jinsi ya kupiga kura kwa mwaka huu ni kutumia tovuti ya http://poy2016.com/ ambapo baada ya kuingia hapo, unaweza kugusa jina la mtu ambaye unapendekeza ashinde tuzo na hapo kura itakuwa imehesabiwa.
Edward Lowassa Anena Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli
Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa amechambua mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli tangu aingie madarakani akisema kuna mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu.
Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 aliungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema hayo jana katika andishi lake kwa vyombo vya habari.
Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008, amesema katika andishi hilo kwamba, “kile ambacho tulikisema wakati ule kwa nini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.
“Kwamba pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa, utumishi wa umma umekuwa kaa la moto.”
Asilimia 90 ya Wanafunzi kupata Fedha zao za Mikopo Kesho
Wakati baadhi ya wanafunzi wa elimu ya juu wakiendelea kusubiri kupata mikopo yao, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia kesho, asilimia 90 ya wanufaika watakuwa wameshapata fedha zao.
Majaliwa alisema hayo jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
“Taarifa niliyonayo ambayo nimepata asubuhi hii (jana), wachache sana wameanza kulipwa jana (juzi), lakini ulipaji utaendelea mpaka keshokutwa (kesho), tunatarajia kufikia asilimia 90 ya wanaostahili kulipwa watakuwa wameshalipwa,” alisema.
Majaliwa ambaye ni mhitimu wa UDSM, aliwataka waombaji wa mikopo washirikiane na Wizara ya Elimu kwa kutoa taarifa sahihi ili kurahisisha ulipaji.
“Serikali haitavumilia tena ucheleweshwaji wa makusudi wa malipo ya fedha za mikopo ya chuo. Kama kuna tatizo, taarifa zitolewe haraka ili kuzuia migogoro kati ya wanafunzi na Serikali yao,” alisema.
Alisema upungufu wa wahadhiri waandamizi umesababishwa na masharti ya ajira za mkataba, unaowataka kuwa miaka 65 na maprofesa kuwa miaka 70.
“Hii inaathiri hali ya utoaji wa taaluma kwa fani za ‘Post-Graduates’. Serikali itaendelea kuweka kipaumbele cha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa ajili ya mafunzo,” alisema Majaliwa.
Alisema licha ya juhudi hizo za Serikali, vyuo pia vinatakiwa kuwa na utaratibu wa kurithishana kazi ili kusiwe na pengo katika utoaji wa taaluma pale baadhi ya wahadhiri wanapostaafu.
Majaliwa ambaye pia alizindua kitabu kilichopewa jina la ‘From Lumumba Street to The Upper Hill and Beyond’, alisema Serikali itatoa ushirikiano katika utekelezaji wa mipango ya chuo hicho.
Akizungumzia kuhusu masilahi ya watumishi wa vyuo vikuu, alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuondoa malimbikizo ya madai kwa watumishi wote wa umma na sasa inakamilisha uhakiki wa taarifa za kiutumishi ili kubaini watumishi hewa.
“Serikali inaendelea na maboresho na kuimarisha masilahi kwa watumishi wote wa umma kupitia bodi ya mishahara na mara tutakapokamilisha, tutapanga upya mishahara na motisha kwa watumishi,”alisema.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Dk Leonard Akwilapo alisema wizara hiyo imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya kufanya ukarabati wa miundombinu kwenye chuo hicho zikiwamo maabara.
Awali, katika hotuba yake, Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala aliishukuru Serikali kwa kuanza kufanyia kazi baadhi ya changamoto zanazokikabili chuo hicho ikiwamo upungufu wa hosteli za wanafunzi.