Wakati Waziri Mkuu ameagiza kaburi la Faru John lifukuliwe na kuchukuliwa vipimo vya vinasaba kuthibitisha kama pembe alizopelekewa ni zake, mabaki yanayoaminika kuwa ni ya mnyama huyo (pichani) yameonekana yakiwa porini katika eneo la Grumeti, wilayani Serengeti alipofia.
Vilevile, gazeti hili limebaini kuwa kabla ya kifo chake, Faru John alikuwa analindwa kwa gharama ya Sh225,000 kila siku.
Faru John alihamishiwa Grumeti, Desemba 17, mwaka jana na kufa Agosti 18, mwaka huu katika mazingira yanayodaiwa kuwa tata.