Ambapo kwa mujibu wa Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo akisoma maamuzi ya Mahakama Huruma Shaibu amesema Mahakama imeridhia ombi hilo ambapo watuhumiwa hao watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja tofauti na ombi la Jamuhuri la miaka mitatu, lakini pia ameagiza Jeshi la Polisi kuwafanyia uchunguzi wa Mara kwa Mara katika maeneo yao, na si kufika kituo cha Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam kama Jamuhuri ilivyoomba.
Tuesday, 7 February 2017
Maamuzi ya Mahakama kuhusu Watuhumiwa wa dawa za kulevya Leo Feb, 7
Ambapo kwa mujibu wa Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo akisoma maamuzi ya Mahakama Huruma Shaibu amesema Mahakama imeridhia ombi hilo ambapo watuhumiwa hao watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja tofauti na ombi la Jamuhuri la miaka mitatu, lakini pia ameagiza Jeshi la Polisi kuwafanyia uchunguzi wa Mara kwa Mara katika maeneo yao, na si kufika kituo cha Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam kama Jamuhuri ilivyoomba.
Picha 16 : Wema sepetu hakupanda kizimbani leo .TID, Tunda Na Wasanii Wengine Wanaotuhumiwa Kwa Madawa ya Kulevya wafikishwa MahakamaniWema
Wakili wa upande wa utetezi amedai taarifa hizo hazijakamilika kwani hazioneshi wanaojiusisha na dawa za kulevya na walikamatwa lini na wapi na hakuna ushahidi wa kujitosheleza wa madai hayo kiasi cha wao kupata dhamana ya kuangaliwa tabia zao bila polisi kutoa ufafanuzi wa kina wa kwanini wanahitaji kupata dhamana ya uangaliz
Mbunge Adai yuko tayari kutaja Wabunge Wanaouza Madawa ya Kulevya
” Suala ninalotaka ni hili suala linashika headline ni suala la madawa ya kulevya, naomba niwaambie sisi viongozi naomba niquote, ‘nitasema ukweli uongo kwangu mwiko.’ Kwahiyo nitakachotaka kukisema mtu yeyote akitaka anihukumu akihukumu chama changu kwanza, na kama wewe ni mwana CCM utanichukia rudisha kadi ndo unichukie.
"Wafanya biashara wa madawa ya kulevya hakuna asiowajua, tunawajua humu ndani wapo, nje ya bunge wapo, kwanini hatuwataji?"alihoji.
Aliongeza, “Kwanini hatuwataji tunakaa kimya? Mheshimiwa mwenyekiti kama kwa ridhaa yako unaniruhusu mimi nitawataja hata humu ndani. Madawa ya kulevya ni pamoja na bangi, kuna mbunge alisimama humu alisema bangi hazina madhara alijuaje kama hazina madhara kama hatumii? tungeanza na huyu.
"Viongozi wenzangu naomba niwahakikishie kama tutakuwa wanafiki mbinguni sisi ndiyo tutakaokuwa kuni, tutakuwa kuni mbinguni tunawafumbia macho watumiaji wa madawa ya kulevya tunakula nao.
"Nimpongeze ndugu yangu Paul Makonda kwa kuthubutu kutaja neno madawa ya kulevya lakini nimhakikishie kila marafiki watano wanaomzunguka watatu ni wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, aanze na hao.”
Ray Vanny kuja na ngoma aliyomshirikisha Diamond
Good News kwenye muziki wa Bongo Fleva wiki iliyopita ni Ishu ya watanzania Diamond Platnumz,Alikiba na Navy Kenzo kushinda tuzo za Hipipo Music Awards huko Uganda. Moja ya tuzo alizoshinda Diamond ni tuzo ya Video bora East Africa kupitia video ya Salome aliyomshirikisha msanii wa label yake, Ray Vanny.

Baada ya ushindi huo, Raymond amefunguka kuhusu kufanya tena ngoma a Diamond ambapo amedai kuwa itakuwa ni ngoma yake yeye. “Lazima,watu wasubiri,” amesema Ray kupitia Supermega ya Kings Fm.
Tayari Rich Mavoko na Harmonize wamemshirikisha bosi wao huyo kwenye nyimbo zao, Kokoro na Bado.
Video! Hii hapa kauli ya Rais Magufuli kuhusu madawa ya kulevya
Rais alisema Serikali na vyombo vyote vya dola vinatakiwa kupambana na suala hili na kukamata yeyote anayehusika na uuzaji ana usambazaji ana utumiaji wa madawa ya kulevya hapa nchini bila kuangalia umaaraufu alionao mhusika, cheo chake, mtoto wa fuklani N.K
ZAIDI HEBU TAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI