Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imeridhia ombi lililowasilishwa Mahakamani hapo na upande wa Jamuhuri la kuwakata watuhumiwa 8 wa Dawa za kulevya kuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka 3,huku wakitakiwa kufika katika Kanda maalum ya Dar es Salaam Mara mbili kwa mwezi.
Ambapo kwa mujibu wa Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo akisoma maamuzi ya Mahakama Huruma Shaibu amesema Mahakama imeridhia ombi hilo ambapo watuhumiwa hao watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha mwaka mmoja tofauti na ombi la Jamuhuri la miaka mitatu, lakini pia ameagiza Jeshi la Polisi kuwafanyia uchunguzi wa Mara kwa Mara katika maeneo yao, na si kufika kituo cha Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam kama Jamuhuri ilivyoomba.
0 comments:
POST A COMMENT