KINGAZI BLOG: 10/25/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Tuesday, 25 October 2016

ALIKIBA AFUNGUKA HAYA KUHUSU COLLABO NA WASANII WAKUBWA AFRIKA

Image result for alikiba
Alikiba amedai kuwa collabo si kitu kilichopo kwenye menu yake.
Akiongea na mtangazaji wa Times FM, Lil Ommmy kwenye red carpet za MTV MAMA jijini Johannesburg, Afrika Kusini Jumamosi iliyopita, aliyemuuliza iwapo ametumia fursa hiyo kuzungumza na wasanii mbalimbali wa Afrika kuhusu collabo.

Ali Kiba
iba alidai kuwa mipango yake ni kufanya muziki mzuri.
“Hiyo sio focus yangu, focus yangu ni kufanya muziki mzuri,” alisema Alikiba.
Muimbaji huyo alikuwa ametajwa kuwania vipengele viwili akiwa na Sauti Sol kupitia wimbo wao Unconditionally Bae.

Serikali kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo kwa kipaumbele



Serikali ipo katika mkakati wa kuwabana wanafunzi wanaopewa mikopo katika fani za kipaumbele, kutumikia katika utumishi wa umma nchini kwa muda fulani ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya inatimia.

Fani hizo ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta, gesi asilia, sayansi asilia, mabadiliko ya tabia nchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Serikali inachukua uamuzi huo, baada ya kubaini kuwapo wanafunzi wanaosomea fani hizo ili kupata mikopo, lakini baada ya kumaliza hukimbilia kufanya kazi nyingine au nje ya nchi na hivyo kuendelea kuwepo upungufu wa wataalamu waliowakusudia kubaki.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na mafunzo ya ufundi, Stella Manyanya aliyasema hayo hivi karibuni, alipozungumzia utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Alieleza kuwa serikali inafikiria kuwe na utaratibu kwa wanaonufaika na mikopo ya kipaumbele kuingia makubaliano na serikali.

Alisema suala hilo halitakuwa jipya kwani hapo nyuma walikuwa wakibanwa kuwa lazima kufanya kazi angalau kwa miaka mitano serikalini na baadaye ni ruhusa kwenda popote, lakini kwa sasa hawawezi kuwabana wote, lakini lazima kufanya hivyo kwa hao wa kipaumbele.

Aidha Manyanya alizungumzia ulipaji mikopo hiyo na kudai wanaboresha sheria ya kukusanya madeni kwa kushirikiana na waajiri.

“Serikali itakusanya madeni hata kwa wakopaji ambao wamejiajiri kwa sababu wengi wakimaliza masomo hawafikirii kulipa,” alisema.”Sasa lazima walipe, wakopaji watambue fedha hizo ni mikopo na lazima kulipa.”

Alisema kwa wakopaji watakaoajiriwa, wizara inataka mkopo huo kuwa wa kwanza kukatwa kabla ya mingine ili kuepuka kuingiliana na sheria za kazi, zinazotaka mkopaji kuachiwa fedha fulani katika mshahara wake.

Serikali Yakanusha Taarifa Iliyosambaa Katika Mitandao Ya Kijamii Kuwa Itaanza Kutoa Ajira


1.Ipo taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimnukuu Waziri wa Nchi -Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb), kuwa Serikali itaanza kutoa ajira, kupandisha Vyeo na kulipa Stahiki mbalimbali za Watumishi wa Umma mwezi Februari, 2017. Chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Jamii Forum kupitia mjadala ulioanzishwa na nkanga chief (JF-Expert Member) na baadaye kusambazwa katika mitandao mingine.

2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inapenda kuwafahamisha Watumishi wa Umma na Umma kwa ujumla kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote na ina lengo la kuupotosha

Umma. Hivyo watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla wanaombwa kuipuuza taarifa hiyo na kuendelea na majukumu yao kama kawaida.


3.Serikali inasisitiza kuwa, suala la Ajira mpya na upandishaji Vyeo litafanyika kwa kuzingatia Bajeti ya Serikali ya Mwaka wa Fedha2016/17. Malipo ya stahili za watumishi wa umma yatafanywa na Serikali kwa kuzingatia, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo.

4. Ikumbukwe, Serikali ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa Umma, hivyo Serikali itatoa taarifa rasmi kwa Umma kupitia mamlaka husika.

5. Serikali kupitia taarifa hii inawaasa wananchi kuacha tabia ya kusambaza habari za uongo au zisizothibitishwa dhidi yake. Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kuzusha na kusambaza habari za upotoshaji kuhusu shughuli za Serikali. 

Imetolewa na:

Habari kuu kwenye Magazeti ya Leo Jumanne ya Octoba 25.



 Magazeti ya Leo Jumanne ya Octoba 25..


















 

Gallery

Popular Posts

About Us