Wednesday, 5 April 2017
Hii ni Habari njema kwa watumiaji wa WhatsApp duniani kote
Huduma ya kutuma ujumbe kubwa zaidi duniani, WhatsApp, hivi karibuni itawaruhusu makumi kwa mamilioni ya watumiaji wake kutuma kitu muhimu zaidi ya picha ama video – fedha.
WhatsApp inailenga zaidi India, soko lake kubwa zaidi kwa uwezekano wa kuingia katika malipo ya mtandaoni. App hiyo inayomilikiwa na Facebook, inaajiri mkurugenzi wa kuongoza jitihada hizo za malipo ya dijitali katika nchi hiyo ya Kusini mwa Asia.
Huduma hiyo itashirikiana na mabenki katika kusaidia miamala ya kidijitali kwa kutumia WhatsApp. India ina watumiaji wa WhatsApp milioni 200 kila mwezi ambayo ni moja ya tano ya watumiaji wake wote hivyo si jambo la kushangaza kuona imelengwa yenyewe kwanza.
Tumekuwekea Kisa kizima cha yule binti aliyejitupa Baharini na kuokolewa, ndugu zake wafunguka A-Z . Ni mambo mazito yaliyokuwa yakiendelea.!
KISA cha binti mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa kutokana na miaka yake) kujitupa baharini akiwa katika boti ya Kilimanjaro V akitoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar juzi, kinaanzia kwenye mawasiliano yake na mvulana mmoja, kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, imefahamika.
Msichana huyo alikuwa akiwasiliana na mvulana huyo ambaye walifahamiana kupitia Facebook, kwa kutumia simu ya mkononi.
Nipashe ilifika Kikwajuni, nyumbani kwa msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu (shule inahifadhiwa) na kuikuta familia yake ikiwa na majonzi, huku wakiwa hawaamini kilichotokea na binti huyo akiwa bado hai.
Akizungumza kwa huzuni, mama mdogo wa msichana huyo, Asha Saleh Mandhi, alisema palitokea mzozo baina yake na binti huyo baada ya kumkuta na simu ya mkononi wakati wazazi wake hawajamnunulia.
Alisema Jumatano iliyopita majira ya jioni akiwa nyumbani hapo na baada ya kupata taarifa kuwa mtoto wake wa kumlea anamiliki simu, alimwita na kumtaka aeleze amepewa na nani la sivyo atampeleka polisi akajieleze.
Alisema siku ya pili yake asubuhi, msichana huyo alitoroka nyumbani na ndipo alipotoa taarifa kituo cha polisi Madema kuwa amepotelewa na mtoto.
“Mimi ndiye ninayemlea huyu mtoto. Kwa kweli sijui amefikwa na mtihani gani kwa sababu hatujampa simu, lakini nashangaa tumemkuta na simu na hakutaka kumtaja aliyempa," Asha alisema.
"Kitendo cha kumuuliza ndicho kilichomfanya kukimbia na kwenda kusikojulikana.”
Mama mdogo huyo alisema baada ya kuwa ametoroka, aliichukua simu hiyo na kuangalia mawasiliano yake na ndipo alipofanikiwa kupata jina la kijana mmoja wa kiume ambaye alikuwa anawasiliana naye mara kwa mara. Hakumtaja.
Alisema baada ya kumpata kijana huyo kwa njia ya simu, aliulizwa anamfahamu vipi binti yao na kujibu kuwa wamejuana kupitia Fecbook, lakini hawajawahi kuonana kwa sababu yeye anaishi Dar es Salaam na binti anaishi Zanzibar.
Alisema alimpa taarifa kijana huyo kuwa binti yao ametoroka na haijulikani alikokwenda, hivyo kumwomba kusaidiana kuhakikisha wanampata akiwa salama.
“Kwa kweli huyo kijana alikubali kutoa ushirikiano na akawa anawasiliana na binti yetu na kumueleza kuwa yuko Dar es Salaam na amehifadhiwa na dereva teksi baada ya kukosa msaada wa eneo analotaka kwenda ambako ni kwa bibi yake anayeishi Mburahati, Dar es Salaam,” alisema.
Alisema aliwasiliana na dereva huyo ambaye alimueleza kuwa amesharipoti katika serikali ya mtaa katika eneo analoishi kuwa amemwokota binti huyo bandarini, Dar es Salaam baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kupata msaada.
Mama mdogo huyo alisema mama mzazi wa binti huyo anaishi Muscat, Oman na kwamba amemlea tangu akiwa mdogo.
Alisema walipata mshtuko baada ya kupata taarifa kuwa binti yao amejitupa baharini wakati akitokea Dar es Salaam baada ya kusakwa kwa siku kadhaa na hatimaye kupatikana.
MFANYAKAZI WA NDANI
Mmoja wa mashuhuda na mfanyakazi wa ndani katika nyumba anayoishi manusura huyo alisema wakati akiwa katika boti wakitokea Dar es Salaam juzi, walipata taarifa kuwa kuna mtu amejitupa baada ya kufika Chumbe, lakini hakujua kuwa aliyejitupa anamfamu.
“Baada ya kupata taarifa kuwa kuna mtu kajitupa baharini, tukaanza kupiga kelele na nilimwona akielea baharini, lakini nilijua ni mtoto wa kizungu bila kufahamu kuwa nilikuwa namfahamu,” alisema Hiyari Miraji Othman.
Alisema alikuja kufahamu kuwa anamfahamu manusura baada ya saa nne na kwamba hakutegemea angeweza kufanya kitendo hicho.
Alimwelezea msichana huyo kuwa ni mpole na mwenye nidhamu kwa kuwa amekuwa akimuona hivyo nyumbani kwao Kikwajuni kwa muda mrefu.
“Hapa kwao nakuja kila siku kwa sababu ndipo penye kibarua changu," alisema.
"Hapa huwa tunapika vyakula kwa ajili ya biashara na huwa namwona tabia zake ni mtoto mzuri anayejielewa.”
BINTI MWENYEWE HUYU HAPA
MAKONDA AIBUKA TENA , SAFARI HII KAJA NA HILI ZITO LITAKALO WAONDOA WENGI KWENYE NAFASI ZAO.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amefunguka kuzungumzia namna ambavyo baadhi ya watu walivyotaka kupiga Tsh Bilioni 7 za serikali kwa kutaka kuwalipa watu hewa fidia za kupisha maeneo yao kwajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali ya serikali.
Aidha RC Makonda ameiagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua watu ambao wamehusika katika sakata hilo.
Akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii ofisini kwake jijini Dar es salaam, RC Makonda amesema amepewa jukumu na Rais Magufuli la kusimamia hela ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali kwajili ya maendeleo ya miradi mbalimbali ndani ya mkoa wa Dar es salaam.
“Mh Rais kama alivyoagiza na kuelekeza kwamba kila pesa inayotoka itoke kulingana na malipo halali. Mimi kama mkuu wa mkoa ninayo majukumu mengi ambapo moja wapo ni kusaini vitabu vya wananchi ambao wanakwenda kulipwa fidia katika maeneo mbalimbali ambako miradi inapita.
Katika miradi ya DMDP ambayo inahusika na barabara, ujenzi wa mifereji na uboreshaji mji wa Dar es salaam. Katika vitabu ambavyo nilitakiwa kusaini kwajili ya kupitisha hizo fedha zaidi ya tsh biloni 10 vilikuwa vitabu 31, lakini katika uchunguzi wangu na team yangu nikagundua vitabu 8 zimekiuka taratibu mbalimbali na masharti, na watu hao hawastahili kulipwa, na katika bilioni kumi tumebaini zaidi ya bilioni 5 na milioni 700 ni fedha ambazo zilikuwa zinaenda kulipwa kwa watu hewa,” alisema RC Makonda.
Alisema katika wilaya Kinondoni kati ya tsh bilioni 6 na tsh milioni 600, zaidi ya tsh bilioni 1 na tsh milioni 800 zilikuwa zinaenda kulipwa kwa watu wasiostahili.
RC Makonda amedai katika jambo ambalo lilimshangaza kampuni ya mafuta ilipewa kazi ya kuthamini majengo na ardhi jambo ambalo lipo kinyume na taratibu.
Alisema katika taarifa ambapo alipewa aligundua kuna mtu alitakiwa kulipwa tsh milioni 4 kwajili ya shimo lake la taka.