KINGAZI BLOG: 09/25/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday, 25 September 2016

MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMAPILI SEPT 25




Wema Sepetu Afunguka Maneno Mazito 'Idris ni Katuni'

Kweli ya kale hayanuki! Ndivyo unavyoweza kusema kwani licha ya Idris Sultan kuwahi kuwa mpenzi wake na Bongo nzima kuitambua kapo yao, mrembo Wema Sepetu ‘Madam’ amethubutu kusema kuwa zilipendwa wake huyo kuwa ni sawa na katuni.

Wema alifunguka hayo hivi karibuni katika mahojiano maalum aliyoyafanya na mwandishi wetu ambapo alipoulizwa mtazamo wake kuhusu Idris kutembea na staa wa Bongo Fleva, Esterlina Sanga na kama anapatwa na maumivu yoyote ndipo Madam aliponyanyua kinywa chake na kumnanga Idris.

“Mh! Yule hana lolote, Idris ni katuni tu. Siwezi kupoteza muda wangu kumzungumzia mtu kama yeye, kuna vitu vingi vya kuzungumza hilo ni jambo dogo sana kwangu. “Kwanza siwezi kumjadili maana itakuwa ni kama kumpa faida ambayo pengine angepaswa anilipe, please tuongelee mambo ya maana bwana achana na huyo katuni,” alisema Madam.

Alipotafutwa Idris ili aweze kuzungumzia kauli hiyo ya Madam na pengine ana lipi la kujibu, simu yake iliita bila kupokelewa. Jitihada zinaendelea.

Hivi karibuni, zilisambaa picha za Idris na Linah wakiwa kimahaba na kudaiwa kuwa wawili hao ni wapenzi hali ambayo ilisababisha mijadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari kuripoti ‘kapo’ hiyo mpya. Wema na Idris kabla ya kufi kia hatua hiyo, walikuwa wapendanao kwa miezi kadhaa na Wema kufanikiwa kupata ujauzito ambao baadaye ulichoropoka kisha wawili hao kumwagana.

MSANII VANESSA MDEE AFUNGUKA JUU YA KOLABO YAKE NA TREY SONGZ


Ni Headlines za Vanessa Mdee ambae amekuwa ni moja kati ya wasanii wa Africa waliochaguliwa kurekodi wimbo na mshindi wa Grammy na mwimbaji wa RNB nchini Marekani, Trey Songz kupitia msimu wa 4 kipindi cha Coke Studio Africa.

Akizungumza na millardayo.com & Ayo TV  Vanessa Mdee aliyaongea haya:

Niko Kenya nikifanya msimu wa Coke Studio Africa ambapo msimu huu tumemkaribisha msanii wa kimarekani Trey Songz kuja kufanya collaboration na waafrika nikiwemo na mimi’


‘Ni experience ya kipekee sana nimefuraha sana kuwa katika nafasi hii ya kufanya collabo nae kwani ni hatua nzuri kwangu pia kuitangaza nchini yangu’

 

Gallery

Popular Posts

About Us