KINGAZI BLOG: 09/19/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 19 September 2016

Uangaliaji Wa Filamu Za Ngono Huharibu Akili Yako

Katika pitapita zangu katika mitandao na baadhi ya kazi zangu mtandaoni, nilikumbana na hili chapisho ambalo niliingiwa na hamu ya kuliweka hapa ili kuwajulisha umuhimu wa kufanya mapenzi na mpenzi wako. Chapisho lenyewe hili hapa:

"Tendo La Ngono Litakufanya Uwe Mjanja, Utafiti Waonyesha

Kuna watu watatetea kuwa tendo la ngono ni kama baraka kutoka kwa Mungu, ni dawa ambayo haijawahi kutokea kamwe. Inasemekana kuwa ngono hupunguza mawazo(stress), depression, husaidia kuchoma kaloria mwilini na pia huwa ni furaha kwa wawili wanaopendana. Kuongezea mambo haya yote imebainika kuwa ngono inafanya mtu kuwa mjanja/mwerevu.

Utafiti huu ulifanywa katika familia ya panya na imeibuka kuwa ngono imewafanya kuwa wajanja, na kwa sababu tuna uhusiano wa karibu na familia ya panya, utafiti huo pia unafanya kazi kwa binadamu.

Kulingana na utafiti uliofanywa na wanasayansi tofauti kutoka chuo kikuu cha Maryland na Konkuk, Seoul nchini N. Korea, imeonekana kuwa panya hao wameongezeka kipawa cha kufikiria na pia jambo hilo limeongeza 'neurogenesis' (ongezeko la neurons kwa ubongo)

Utafiti umeonyesha kuwa sehemu inayofaidi zaidi kwa tendo la ngono ni sehemu iitwayo 'hippocampus', sehemu inayoweka matukio ya zamani ya kiumbe. Sehemu hii hukuwa na kunawiri.
Kiufupi tunaweza kusema kuwa matendo ya ngono unayoyafurahia ukiwa miaka ya 30 na 40 itasaidia kuongezea mawazo ya matendo ya ngono uliyoyachukia wakati wa miaka ya 20.

Lakini katika utafiti huo kuna mambo ambayo hayakuwa sawa, kuna sehemu fulani ya ubongo ambayo ukuaji wake ulikuwa duni, nayo ni 'ngono ya uongo'. Ngono ya uongo ni kama kuangalia ilamu za pornography kupindukia. Utafiti unaendelea kusema kuwa matukio yote yaliyowekwa kwa kufanya tendo la ngono yatafutika baada ya kuangalia filamu za ngono mno.

Huu ni utafiti sahihi kwani kuna ule msemo kuwa kuangalia filamu za ngono kuna haribu akili, kunakufanya usahau mengi. Kwa hivyo kuangalia porno nyingi kunakufanya uwe na mawazo duni." -FoxNews

Hebu sasa turudi kwa Nesi Mapenzi kidogo. Ok hivi wewe mara ya mwisho ulifanya mapenzi lini? Na ni lini mwisho uliangalia filamu za ngono?

Ni mara ngapi ulifanya mapenzi na ni mara ngapi ulishaangalia filamu za ngono? Iwapo kuangalia filamu za ngono imepita ile ya kufanya mapenzi basi uko katika tatizo kubwa, tatizo la kupoteza uwezo wako wa kukumbuka mambo siku zako za usoni.

Na kwa kutatua hili tatizo unachukua mkondo upi? Je unachagua kutulia kuacha kuangalia filamu za ngono ama utaamua kuongeza kufanya mapenzi ili kuongeza ushapu wako kimaisha?

Na kama umeamua kufanya mapenzi kwa wingi, je una  mpenzi wa hakika ama ni mpenzi wa kuotea, kesho anakupa kesho kutwa anakunyima?

Ok, kwa kutatua na kukusaidia kukupa mawazo...

Kwa wale ambao tayari wako na wapenzi thabiti (Wanaume Alpha) na wako tayari kufanya mapenzi kila siku ili kukuza bongo zao bila kuchoka wala kuboeka ingieni hapa.

Kuna wale ambao wana wapenzi wa kuotea, wale ambao hawana wapenzi kabisaaa, na kila wakijaribu kutongoza wanashindwa, wanabakiwa kuenda majumbani mwao na kujifungia chumbani huku wakiangalia filamu za ngono na wakipiga punyeto. Kama unaamini kuwa wewe hauko miongoni mwa hili kundi ingia hapa.

Ok. Kazi kwako. Ni wewe wa kuchagua iwapo utaamua kuendelea kuharibu akili yako ama kuikuza akili yako ili upate ujuzi wa kijasiriamali maishani.


MASHAMBULIO MATATU YA KIGAIDI YATOKEA MAREKANI NDANI YA SAA 24


Jumapili na Jumamosi kumetokea mashambulio matatu katika ardhi ya Marekani – bomu lililolipuka Manhattan, watu kuchomwa kisu huko Minnesota na bomu kulipuka kwenye bomba la maji huko New Jersey.
Kuna uhusiano mkubwa na tukio la kigaidi huku watu watano wakikamatwa New York. Bomu lililolipuliwa makusudi huko New York limejeruhi watu 29.
Mamlaka zimedai kuwa hakuna ushahidi iwapo matukio hayo yalikuwa na uhusiano lakini kutokea ndani ya saa 24 kumesababisha hofu za usalama, kitu ambacho tayari kimekuwa muhimu kuzingatiwa katika mchuano wa urais kati Hillary Clinton na Donald Trump.Bomu la pili liligundulika karibu na eneo hilo na polisi walifanikiwa kulitegua.Kwa upande mwingine mtu aliyewachoma kisu watu tisa kwenye mall huko Minnesota Jumamosi, aliuawa na polisi ambaye hakuwa kazini. Mtu huyo amedaiwa kuwa mwanajeshi wa kundi la Islamic state.
Jiunge na Bongo5.com sasa

Magazeti ya Leo Jumatatu 19 September 2016..





















Official VIDEO | Diamond Platnumz Ft. Rayvanny Salome ( Traditional ) | Watch/Download



Aliyeng’atwa ulimi Wakati Akipigana Denda na Mwanamke Ahofia Kuachwa na Mchumba Wake


Kijana Saidi Mnyambi (26) anayedaiwa kung’atwa 1/3 ya ulimi wake wakati wakinyonyana ulimi na mwanamke mmoja, ameingiwa na hofu kuwa mchumba wake anaweza kumwacha kutokana na kitendo hicho.

Kijana huyo mkazi wa Unyankhae, Manispaa ya Singida, aliyasema hayo juzi hospitalini alikolazwa .

Alisema hofu aliyonayo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo kuwa gumzo kubwa ndani na nje ya Singida. 

“Kabla ya tukio hilo, uchumba wangu ulikuwa unaendelea vizuri na mambo yalikuwa yanaelekea kwenye kufunga ndoa lakini sasa nina hofu mwenzangu anaweza akapotoshwa na mambo yakaharibika. Nikitoka hospitalini nitalifuatilia jambo hili kwa ukaribu zaidi ili kuweka mambo sawa,” alisema Mnyambi. 

Kuhusu matibabu, Mnyambi alisema anaendelea vizuri na kwamba sasa anaongea vizuri kama binadamu wengine na maumivu yamepungua. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba alisema wanamshikilia mwanamke huyo (jina hajalitaja) aliyemng’ata ulimi Saidi na wanaendelea na upelelezi kabla sheria hazijachukua mkondo. 

Alisema mkuu wa upelelezi makosa ya jinai Mkoa wa Singida anakamilisha uchunguzi lakini akabainisha kuwa taarifa zilizoenea awali kuhusu tukio hilo ni tofauti na hali halisi. 

“Baada ya kumpata mwanamke anayetuhumiwa kumng’ata ulimi Mnyambi, zimepatikana taarifa mpya. Waandishi kuweni na subira tutawapatia taarifa zenye mashiko wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Kakamba.

 

Gallery

Popular Posts

About Us