He told a cheering crowd in Arizona that he would secure the border, and left open the possibility that millions of illegal immigrants be deported.US Republican presidential candidate Donald Trump has insisted Mexico will pay for a border wall "100%", in a major immigration speech.
Thursday, 1 September 2016
Msajili amlima Barua Maalim Seif kuhusu sakata la Lipumba
Published Under
KITAIFA
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini imemuandikia barua Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kufuatia mvutano wa kusimamishwa uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Profesa Lipumba kumuandikia barua Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akilalamikia kusimamishwa uanachama bila kufuata utaratibu huku akitaka kurejeshwa kwenye nafasi yake ya uenyekiti.
Ofisi hiyo imeutaka uongozi wa CUF kueleza kwa kina hatua ilizopitia hadi kufikia uamuzi huo kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, na kwamba iwasilishe barua hiyo kufikia kesho majira ya saa 9:30 alasiri.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano cha Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa, Monica Laurent amesema kuwa ofisi hiyo ilipokea barua ya Profesa Lipumba Agosti 29 mwaka huu ikiwa na malalamiko na kwamba wametaka uongozi wa CUF kutolea majibu.
“Tumeitaka CUF kutoa majibu kuhusu malalamiko ya Profesa Lipumba, ndipo sisi tutakapotoa majibu,” amesema Monica.
Lipumba ambaye alijiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti mwaka jana akipinga uamuzi wa chama chake kumuunga mkono Edward Lowassa kugombea urais, amerejea na kudai kutengua barua yake ya kujiuzulu.
Baraza Kuu la CUF lililoketi visiwani Zanzibar hivi karibuni lilimsimamisha uanachama Profesa Lipumba pamoja na viongozi wengine 10 akiwemo Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya aliyekuwa Naibu Katibu mkuu (Bara).
Hata hivyo, Profesa Lipumba amepinga uamuzi huo akieleza kuwa kikao cha baraza hilo kililiwa batili.
SHARE!
MCT yampongeza Rais Magufuli vita ya rushwa
Published Under
KITAIFA
BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limeipongeza serikali ya Rais John Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na rushwa pamoja na ubadhirifu na kusema inapaswa kuungwa mkono na kila mmoja na pia vyombo vya habari.
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alitoa pongezi hizo jana wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Baraza hilo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mukajanga alisema kwa kuwa vyombo vya habari ni namba moja katika kupambana na rushwa, wanaiomba serikali itafute suluhu pale vinapokosea badala ya kuvifungia.
“Midhali serikali inajua sheria zilizopo zinahitaji marekebisho, tupunguze kuzitumia kwa sababu hazitupeleki mbele, bali zinaturudisha nyuma,” alisema Mukajanga.
Alisema hivi sasa Kamati ya Maadili ya Baraza hilo ambayo Mwenyekiti wake ni Jaji Juxon Mlay inaendelea kukusanya ushahidi wa kutosha ili waende kuzungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuhusu mgogoro huo wa kuvifungia vyombo vya habari.
Vyombo vya habari vilivyofungiwa na serikali hivi karibuni ni gazeti la Mseto na vituo vya redio vya Magic FM na Radio Five. Naye Rais wa baraza hilo, Jaji Thomas Mihayo alivitaka vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari visiogope kutumia haki yao ya msingi pale inapotokea wanavunjiwa uhuru wao wa kujieleza kwa sababu mahakama ni sehemu sahihi ya kudai haki kamili.
“Watanzania wengi hawapendi kutumia vyanzo sahihi vya kuweza kupata haki yao. Waandishi wa habari mnapotaka kupata haki yenu nendeni mahakamani kwa sababu ni chombo cha pekee kinachoweza kutoa haki ya kweli," alisema Jaji Mihayo.
Mbunge wa Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa gazeti la MwanaHalisi, Said Kubenea alisema kuna tatizo kwa waandishi wa habari kuwa wavivu katika kutafuta haki mahakamani, pengine ni kutokana na mchakato mrefu.
Aliiomba MCT kuwa mstari wa mbele katika kuzisimamia kesi hizo mahakamani, kwa kuwa kwa kufanya hivyo kutaipa kesi hizo nguvu.
“Ni rai yangu MCT, lisimame katika kutetea waandishi na vyombo vya habari," alisema Kubenea. Katika hilo, Mukajanga alisema hilo ni jukumu lao wamelipokea hivyo watatenga fedha kwa ajili ya kusaidia uhuru wa habari nchini.
SHARE!
Vanessa amwandikia ujumbe mzito mpenziwe Jux kwenye birthday yake
Published Under
TOP STORIES
Mara nyingi mtu wako wa karibu anapokuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa, ni muhimu kumpa ujumbe muhimu kuonesha jinsi alivyo na maana kwako.
Vanessa Mdee ametumia siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake, Jux kumwandikia ujumbe muhimu kudhihirisha ni kwa kiasi gani anampenda. Ametumia pia fursa hiyo kuutaja wimbo wao wa pamoja, Juu. Usome:
When we first met I was an upcoming songstress with a fast tongue and one hit song on the radio. You … well you were pretty much the same. Your boy asked me if I would spit some bars on your song. I said no. Then walked into the studio and met you and instantly had a change of heart. Fast forward to 2yrs later, tumekuwa.You’ve got the biggest song in the country #Wivu and a multi million dollar brand #AfricanBoy and as for me well … kitu kimoja hakijabadilika though. Kwako sisikii. Lol!Lakini hayo yoteee ni mifano tu ya jinsi gani ukiwa na mahusiano na mtu anayekujenga kifikra na vinginevyo maisha yako yanaweza kukaa sawa. Siwezi kueleza ni jinsi gani uwepo wako katika maisha yangu yamenibadilisha na kunikuza na kuniboresha. All things are God’s design. Namuomba Mungu akuongoze and akupe maisha marefu sana sana sana. Maisha yenye mafanikio, afya bora na furaha tele. Una moyo wa kipekee sana tofauti na mtu yeyote ninayemfaham.Nasikitika kuwa mbali na wewe leo hii lakini unajua nikipata, umepata na tunazidi kwenda #Juu. Oh by the way kwa mashabiki wetu ngoma yetu ya kwanza ya pamoja inaitwa #Juu Basi nisaidieni kumtakia mpenzi wangu Heri ya siku ya kuzaliwa.
SHARE!
WABUNGE WAIBANA BODI YA MIKOPO (HELSB) KWA KUONGEZA POSHO
Published Under
KITAIFA
Wabunge wameibana Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kwa kuongeza posho na kufikia jumla ya Sh1 bilioni katika kipindi kifupi kiasi ambacho hakilingani na kazi wanayoifanya.
Kwa kipindi kirefu, bodi hiyo imekuwa ikitupiwa lawama kwa kuchelewesha mikopo, kushindwa kukusanya fedha za wanafunzi waliokopa na kutoa mikopo kwa wanafunzi hewa.
Hivi karibuni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema bodi hiyo imetoa fedha za kujikimu na mafunzo kwa vitendo kwa zaidi ya wanafunzi hewa 1,000.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdul-Razaq Badru alijitetea mbele ya kamati hiyo akisema ni mgeni katika bodi hiyo na kwamba wanaweka mikakati mizuri ya kurekebisha mambo hayo ili kuhakikisha inafanya kazi kwa weledi zaidi.
Wakizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) cha kukagua Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2014/15 ya bodi hiyo, wabunge hao walisikitishwa na kitendo cha bodi hiyo kushindwa kukusanya zaidi ya Sh3 trilioni walizowakopesha wanafunzi mbalimbali tangu ianze kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Walisema isipobadilika katika utendaji wake, kuna haja ya Serikali kuivunja na kuchagua benki moja kusimamia shughuli hiyo.
“Mnatakiwa kuongeza juhudi na mikakati ili kuhakikisha kwamba madeni yote yanakusanywa kwa wakati la sivyo naona kuna haja ya Serikali kuivunja bodi nakutafuta njia nyingine,” alisema Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Raisa Mussa.
Mbunge wa Same Mashariki (Chadema), Naghenjwa Kaboyoka alihoji kwa nini pamoja na bodi hiyo kuwa na mameneja 18 na wafanyakazi wa kudumu 144, bado utendaji wao umekuwa siyo wakuridhisha.
“Kwa idadi yenu tulitegemea kupata ripoti inayojitosheleza na hata utendaji wenu ulitakiwa kuwa wa ufanisi zaidi,” alisema.
Akijitetea zaidi, Badru alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi yake lakini kwa sasa wamepiga hatua kubwa katika ukusanyaji wa madeni kutoka kwa wanufaika wa mfuko huo.
“Kwa mfano Mei mwaka huu tulikusanya kiasi cha Sh2 bilioni na Juni tulikusanya Sh6 bilioni,” alisema.
Aliongeza kuwa ipo mikakati mingi ambayo wamejiwekea katika kuhakikisha kwamba bodi hiyo inakusanya madeni kikamilifu kutoka kwa wadeni wake wote.
“Kwa kupitia mikakati yetu, tumeweza kuongeza idadi ya wanafunzi ambao tunawapa mikopo kutoka 42,729 hadi 123,783. Katika kipindi hicho fedha za mikopo zimeongezeka kutoka Sh56 bilioni hadi kufikia Sh465.3 bilioni,”alisema.
SHARE!
Scholarships tenable in Mexico for the year 2017
Published Under
KITAIFA
This is scholarship chances for the student who finshed advanced level , May 2016
SHARE!
Tahadhari dhidi ya Taarifa za uongo kuhusu kutangazwa kwa Orodha ya wanafunzi waliodahiliwa kwa mwaka wa masomo 2016/2017
Published Under
KITAIFA
SHARE!
Bongo flavor Female celebrity shilole has left her fans Mouth open after catching her private front place
Published Under
TOP STORIES
Bongo Celebrity Shilole had surprise her fans during her Ti go fiesta 2016 Performance, by catching her front private place on her Body, many of her fans where shouting and tell shilole that she should give it to them hahah. this was so lovely as we know that shilole is one among the greatest Female musician in Tanzania who has a full of Dramas and scandals
SHARE!
Subscribe to:
Posts (Atom)