KINGAZI BLOG: 04/17/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 17 April 2017

Kutana na Harnaam Kaur..Mwanamke Mwenye Ndevu Nyingi Zaidi Duniani..!!!


AKIWA mwalimu wa shule ya msingi na mwanamitindo, Harnaam Kaur aliingia katika Kitabu cha Rekodi za Dunia (Guinness World Records) kuwa mwanamke mdogo duniani mwenye ndevu nyingi zaidi.

Kaur (24), aliweza kukabiliana na changamoto za miaka mingi za hali aliyo nayo ikiwamo kejeri, kebehi, zomea zomea  na kila aina ya maneno mabaya hadi kufanikiwa kujiamini na kukomaa na nywele zake hizo za usoni.

Aliingia katika rekodi hizo kwa ndevu zake za inchi sita ikiwa ni matokeo ya kusitisha mpango wa kuzikata.

Mkazi huyo wa mji wa Slough, Kusini Mashariki mwa Uingereza pia amewahi kupokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa watu asiowafahamu mitandaoni.

Kisa cha kumtishia ni ndevu zake nyingi zinazomfanya asitofautishwe kirahisi na mwanamume.

Mwanamke huyo ana tatizo la homoni linalomfanya kuwa na vinyweleo vingi kupita kiasi likijulikana kitaalamu kama ‘polycystic ovary syndrome.’

Ameeleza alianza kupata tatizo hilo akiwa na umri wa miaka 11 na alikuwa akizinyoa mara mbili kwa wiki.

Awali mwanadada huyo alikuwa akijitahidi kuzipunguza na kunyoa lakini ilishindikana, sasa ameamua kujiamini jinsi alivyo, ingawa vijana wa rika lake humuona kama mtu wa ajabu.

Ameeleza kuwa alipokuwa shuleni alikuwa akionewa kwa kuitwa majina mengi ya kejeli kama ‘jike dume’, na alishindwa hata kuwaangalia watu usoni.

Alipotoka shule, alienda moja kwa moja nyumbani na kujifungia humo siku zote asionekane mara kwa mara.

Anaongeza kuwa kutokana na kuishi katika hali hiyo alifikia hatua ya kutaka kujiua.

“Wakati nimekaa na kupanga kujiua, nilianza kujishauri, nilijiambia: 'Nguvu unayotumia kuhitimisha maisha yako, kwanini usiitumie kugeuza maisha yako na kufanya kitu kilicho bora?”


Na hivyo, akaamua kujiunga na dini ya Singasinga, Imani ambayo hairuhusu watu kunyoa vinyweleo vyao kwa kuwa Mungu ndiye aliyewaumba hivyo.

“Wakati nilipoanza kuacha nywele zikue ilikuwa sababu za kidini, lakini kwa kadiri miaka ilivyosonga mbele, sababu nyingine kuu zaidi ni kwamba napenda jinsi nilivyo”, alisema wakati wa mahojiano baada ya picha yake kutumikla katika maonesho ya kusherehekea watu wenye ndevu bora duniani.

Kwa hiyo ameziachia nywele zake na sasa anaonekana kama mwanaume akiwa na nywele nyingi kidevuni, mikononi na kifuani.

Uamuzi wake awali uliikanganya hasa familia yake, ambayo Kaur anasema: “Mama na baba yangu hawakufurahia uamuzi huo kwa vile walikuwa wana wasiwasi nisingeweza kuishi maisha ya kawaida iwapo ningekuwa na ndevu.

“Walikuwa na wasiwasi kwamba nisingeweza kuolewa wala kupata ajira. Lakini nilitaka kusimamia na uamuzi wangu kwa ajili yangu na si mtu mwingine. Awali niliishi kwa kujificha na kuumia vya kutosha. Hiyo ilitosha!”

Wazazi wake sasa wameukubali uamuzi wake huo na kaka yake Gurdeep Singh (18) ni shabiki wake namba moja.

Kaka yangu ni kweli alikuwa mmoja wa watu aliyeshtushwa na uamuzi wangu wa kutonyoa, lakini alinikumbatia na kunieleza kwamba naonekana mrembo zaidi niwapo na ndevu, lakini hakufahamu kwanini niliamua vile.’

Aliongeza: “maneno haya ya kaka yalitosha kunifanya nikomae na ndevu zangu.’

Anasema: “tangu aamue kujikita na nywele usoni, watu walizidisha kiwango cha kumkazia macho. Awali nilikuwa na hasira, lakini nilitambua hawakufahamu na ni wazi wanaogopa kuniuliza na hivyo huamua kurudisha tabasamu kwao.”

Anaihesabu hiyo kama ‘heshima’ na kwamba itasaidia kuchochea wanawake wengine kujikubali walivyo au wanavyotaka kuwa.

Imani hiyo imempa ujasiri zaidi juu ya muonekano wake, na anajiona mwanamke mwenye mvuto zaidi.

“Nahisi nimekuwa mwanamke zaidi, nina mvuto zaidi na nadhani naonekana hivyo pia. Nimejifunza kupenda jinsi nilivyo na hakuna kitakachonitikisa sasa hivi,” anasema Harnaam.

“Naweza kwenda kwenye maduka ya wanawake bila kuhisi kuwa sitakiwi kuwa kule. Navaa sketi, gauni na vidani na napenda kutengeneza kucha zangu kama msichana mwingine yeyote.”

Machi mwaka jana alikuwa mwanamke wa kwanza mwenye ndevu kushiriki maonesho ya mitindo ya London.

Amekuwa akipokea dili ikiwamo kupamba majarida mbalimbali ya mavazi ikiwamo kupiga picha akiwa katika mavazi ya harusi.

Akiwa na furaha sasa Kaur ameajiriwa kama msaidizi wa walimu katika Shule ya Msingi ya Singasinga na kumfanya imani yake ipae.

Anasema wauza duka shuleni humuita ‘bwana’ na kwamba watu wengine huniangalia kwanza wakionan ndevu kisha wanaposhusha macho chini wanabaini nina matiti pia. Inakanganya watu wengi hakika!.

“Kichekesho zaidi ni kutoka kwa watoto katika shule yangu. Baadhi huniuliza ndevu zangu ni nini. Nawajibu ni vinyango vya vibwengo. Baadhi huniuliza nanunua wapi na huwajibu tu ‘Asda”.

Hatari !! Mwanaume aliyefanya mauaji huku Akionyesha Live Marafiki zake Kupitia Facebook asakwa

Steve Stephens muuaji anayesakwa Marekani

Polisi katika jimbo la Ohio nchini Marekani wanamtafuta mtu anayedaiwa kufanya mauaji,huku akionyesha moja kwa moja mauaji hayo kupitia mtandao wa Facebook.

Maofisa katika mji wa Cleveland wamesema kuwa Steve Stephens anaonekana akionyesha moja kwa moja mauaji wakati akimpiga risasi mwanaume mmoja mtu mzima kupitia Facebook.

Mkuu wa Polisi mjini Cleveland Calvin Williams amemtaka Stephens ajisalimishe mwenyewe.

Williams alisema kuwa mtu huyo ni hatari kuendelea kuwa mafichoni kwake.

Polisi wanasema hawajapata ushahidi madai ya Stephen kuwa amewauwa watu kumi na mmoja.

Baada ya Kumsimamia Roma..Mwakyembe Adai Maisha Yake Yapo Hatarini..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 17/4/2017..!!!




Baada ya Kula Ujana Vyakutosha..Aunty Lulu Sasa Kuimba nyimbo za injili.


BAADA ya maisha ya ujana yenye kila aina ya uchafu hatimaye msanii na Mtangazaji Lulu Semagongo maarufu kama Aunty Lulu, amesema anajiandaa kuimba nyimbo za Injili zitakazozungumzia maisha yake ili watu wengine wajifunze.

Aunty Lulu alisema nyimbo zake zitabadilisha maisha ya watu wengi kwani ujumbe utakaokuwemo ndani yake utazungumzia mambo mengi ambayo amepitia katika maisha yake.

“Najiandaa kuimba nyimbo za Injili na wimbo wangu wa kwanza utaitwa Unikumbuke Mungu, ambapo ndani yake nitaeleza mambo yote niliyopitia kwenye maisha yangu ikiwemo kubadilisha wanaume tofauti, starehe za kila aina, kuvuta sigara na mengine mengi na nimeamua kufanya hivi ili kupitia historia ya maisha yangu vijana wengi wabadilike,” alisema.



Kali ya Mwaka!!! huyu ndiye jamaa aliyetua Mahakamani kuwashtaki waisraeli kwa Mauaji ya Yesu.


Dola Indidis ni mwanasheria kutoka Kenya aliyeishtaki Israel kwa kumuua Yesu). nadai hakuipeleka kesi mahakamani kwa misingi ya kidini bali kwa misingi ya Kisheria. Anasema "Its academic thing not a theological thing" Yeye anachoangalia si unabii bali legal procedure. 

Pia amesisitiza ameamua kumtetea Yesu kama mtoto wa Yusufu (fundi seremala) na sio Yesu kama Masihi "I look Jesus as son of Joseph not as the Messiah"

Alipoulizwa mbona ilitabiriwa Yesu atakufa, anasema anafahamu hilo ila hoja sio Yesu kufa, hoja yake ni process iliyotumika kumuua haikuwa sawa kisheria. Anadai mahakama ilikosea kujiingiza kwenye kesi hiyo "The court should not involve itself in that crooked case."

Anasema Yesu ungehukumiwa kifo kwa kufuata taratibu za kisheria kusingekuwa na shida, ila aliuawa kikatili bila kupewa haki ya kusikilizwa. Wakati Yesu anpelekwa mahakamani (kwa Pilato) tayari alishaanza kusulubiwa kabla hata hukumu haijatoka. 

Huo ulikuwa ukiukwaji wa sheria maana mtuhumiwa hawezi kuadhibiwa kabla ya mahakama kujiridhisha kuwa mtu ana hatia. "no punishment could be made unless the court proved beyond the reasonable doubts that Jesus was guilt" Anasema Yesu angepata wakili wa kumtetea angeachiwa huru. Hata kama ilimpasa kufa angeuawa kwa namna nyingine.

Anadai pia Pilato hakuwa na nguvu ya kisheria ya kusikiliza ile kesi na hata yeye alikiri hilo ndio maana akawarudisha wayahudi kwa Herode. Lakini akalazimishwa kutoa hukumu kwa pressure ya mfalme Herode. "Pilate had no jurisdiction to give the judgment, he confessed, and also he confessed the innocence of Jesus"

Pia anadai Pilato alikiri Yesu kutokuwa na hatia, lakini bado alisulubiwa. Sasa kama Pilato ndio alikuwa Jaji na hakuona hatia ya Yesu kwanini bado Wayahudi walimsubisha?

Akaongeza kuwa kitendo cha Wayahudi kumsulubisha Yesu mbele ya Jaji (Pilato) ni kujichukulia sheria mkononi na ni uvunjifu wa haki za binadamu. "Jesus was tochered in-front of Judge, that is abuse of Human rights" 

Anadai misingi ya haki ilikiukwa katika kuongoza kesi (miscarriage of Justice) na Yesu hakupewa nafasi ya kusikilizwa japo alikuwa akilalamika. "Even Jesus complained but he was not given right to be heard,that is mis-courage of justice."

Amesema pia kuwa maamuzi hayakuzingatia principle of natural justice, na hukumu inapaswa kurekebishwa na Israel kuomba msamaha. "The judgment was bad in law and should be quashed"

Ametumia kesi ya Mwai Kibaki vs Daniel Arap Moi 1999 kama refference ya kesi yake (MWAI KIBAKI Vs DANIEL TOROITICH ARAP MOI, Case Number :Civ App 172 of 1999").

Anaungwa mkono na makanisa kutoka nchi za Norway, Marekani, Israel, Uingereza, Tanzania, Afrika Kusini, Canada na Ujeruman

Rais Magufuli Aagiza TCU kuacha kuchagulia vyuo wanafunzi

Rais John Magufuli ameiagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kutowachagulia vyuo wanafunzi wa elimu ya juu na kuwaacha wanafunzi hao kuchagua vyuo wanavyovitaka wenyewe.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais Magufuli alipokuwa akizindua mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo alikitaka chuo hicho pia kutoza Sh 500 kwa siku tofauti na Sh 800 ambazo zinatoswa kwa hosteli nyingine.

“Ninaamini kama wanafunzi wangepewa nafasi ya kuchagua vyuo wanavyovipenda wenyewe, vyuo vya Serikali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo Kikuu cha Mzumbe vingekuwa na wanafunzi wengi sana,” alisema Magufuli.

Aliendelea kwa kusema kuwa TCU imekuwa ikiwachagulia wanafunzi vyuo visivyo na sifa na makazi ya wanafunzi hivyo kusababisha wanafunzi hao kusoma katika mazingira magumu na wanapomaliza masomo yao hukosa ajira kutokana na vyuo hivyo kutokuwa na sifa. Rais Magufuli alitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) lenyewe kubaki na udhibiti.

Aidha alisema ni vyema Tume ikabaki na majukumu yake kama kuhimiza ubadilishaji wa maarifa/elimu kwa njia ya kuunganisha kimtandao Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu, usajili na utambuzi rasmi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu, uthibitishaji wa programu za kitaaluma, uthibitishaji na uratibu wa udahili wa wanafunzi.

Majukumu mengine ni ufuatiliaji na udhibiti wa elimu bora Vyuo Vikuu na Vyuo vya Vyuo Vikuu, ukusanyaji na usambazaji wa taarifa/ data kuhusu elimu ya juu. “Niombe tu kwa Wizara ya Elimu na TCU tubadilishe kidogo utaratibu wa kuchagulia wanafunzi, wanafunzi wawe wanachagua vyuo badala ya TCU kuwachagulia vyuo vya kwenda,” alisema. Akifafanua zaidi alisema kama wanafunzi wakijichaguliwa vyuo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kingejaa wanafunzi 23,000 wanaotakiwa kuwepo katika chuo hicho.

“Lakini sijajua ni kwa nini mtu amefaulu anataka kuja hapa afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kwenda kwenye kachuo ambako hakana jina akasome pale, wakati hakuna hata mabweni, saa nyingine hata walimu hawana, tunawatesa watoto hawa,” alisema. Alisema anafahamu ingawa hana ushahidi kuwa wakuu wa vyuo hivyo wanatoa fedha kwa viongozi wa TCU ili wapangiwe idadi ya wanafunzi wanaowahitaji kwenye vyuo vyao.

Rais Magufuli alisema kuwa TCU ibaki kuwa mdhibiti wa elimu lakini wanafunzi wabaki kuwa na haki ya kuchagua vyuo kwani baadhi ya vyuo vinaendesha shughuli zake kwa mikopo ya wanafunzi hao. “Tuwaache watoto wachague vyuo wanavyovitaka, vile ambavyo havitachaguliwa, vife kwanini mnalazimisha vyuo ambavyo havina ubora vipate wanafunzi msipolazimisha vyuo ambavyo vina ubora vitapata watu….. najua maneno haya hayawafurahishi baadhi ya watu na mimi siko hapa kumfurahisha mtu?” alisema Rais Magufuli.

Awali Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandara, alisema mradi huo una majengo 20, kila jengo lina gorofa nne na ujenzi wake umekamilika ndani ya miezi minane. Majengo hayo yatachukua wanafunzi 3,840.

Akizungumzia mradi huo wa majengo ya mabweni, Rais Magufuli alisema anafuraha kukamilika majengo hayo kwa sababu ahadi yake imetimia “Yale niliyoyaahidi yametimia, chuo kikuu kimekuwa na matatizo ya makazi kwa ajili ya vijana wetu, matatizo haya ni ya siku nyingi na tumekuwa hatuyaangalii sana kwa sababu yanawahusu wanafunzi hayatuhusu sisi,” alisema Rais Magufuli.

Alisema vijana wengi wanapochaguliwa kuingia chuo kikuu huwa hawajui kuwa kuna tatizo hilo wengine kuishia kupanga vyumba mitaani na wengine kubebana katika mabweni huku kitanda kimoja kikichukua zaidi ya wanafunzi watatu. Rais Magufuli alisema kuwa kutokana na tatizo hilo la makazi kwa wanafunzi wapo vijana wengine wameamua kuoa na kuolewa ili tu waweze kupata sehemu za kuishi.

Alisema chuo hicho ndio chuo kikuu mama katika historia ya nchi na kwamba viongozi wengi wamesoma katika chuo hicho. Rais Magufuli alisema kwa kutambua tatizo hilo aliahidi kutafuta Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya chuo hicho ingawa hakuwa na uhakika wa kufanikiwa lengo lake hilo. “Niliwaita wataalamu nilipowapa ramani wakasema majengo hayo yatagharimu Sh bilioni 150 hadi bilioni 200, hapo unaweza kujiuliza wewe umetenga Sh bilioni 10 unaambiwa inayoweza kutosha ni Sh bilioni hizo, ilikuwa ni lugha ya kukatisha tamaa,” alisema Rais Magufuli.

Alisema hakukata tamaa akaamua kumuita Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Elius Mwakalinga alipopiga hesabu akamwambia Sh bilioni 10 zingetosha katika ujenzi huo. Katika ujenzi huo Rais Magufuli alisema aliihusisha pia Wizara ya Ulinzi kusimamia na pia JKT katika ujenzi wa uzio wakati watu wengine wakishiriki ujenzi huo na pia alikiomba chuo kutoa eneo.

Rais Magufuli alipongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kufanya maamuzi ya kutoa eneo hilo ambapo awali ilishindikana kutumia maeneo hayo na kwenda kujengwa mabweni eneo la Mabibo ambapo ni mbali na chuo hicho. Alisema mabweni ya Mabibo yalijengwa mwaka 2000 kwa gharama ya Sh bilioni 27, yanachukua wanafunzi 4,000, lakini mabweni hayo yaliyojengwa sasa yanachukua wanafunzi 3,840 na gharama yake ni Sh bilioni10.

Rais Magufuli alisema kwa mfano uliooneshwa na TBA iwe fundisho kwa viongozi wa serikali ambao wamezoea zauni zenye gharama kubwa kwa manufaa yao na sio manufaa ya Serikali. “Hii iwe fundisho kwa watumishi na viongozi wa serikali waliozowea kuchukua ten pasenti na wakati mwingine 70 pasenti kwa majengo ambayo yangeweza kujengwa kwa gharama kidogo, pili iwe fundisho kwetu kuamini wakandarasi wa ndani wanaweza,” alisema Rais Magufuli.

Alisema wapo watu ambao hawaamini kuwa watanzania wanaweza kujenga vizuri kama ambavyo imefanyika katika mradi huo, “napenda nitoe wito kwa watanzania, vizuri vinafanywa na watanzania.” Rais Magufuli alisema wapo watu ambao walibeza kuwa kwa gharama ya Sh bilioni 10 isingewezekana kujengwa nyumba hizo ambapo wakiona mradi umekamilika wanashangaa.

“Kwahiyo nawashukuru sana TBA, Mwakalinga umefanya kazi nzuri sana, Bodi ya TBA mmefanya kazi nzuri, mabweni haya mazuri yamekamilika kwa kipindi kifupi inadhihirisha Tanzania tunaweza, tukiamua tunaweza na watu wakaona ni miujiza,” alisema. Rais Magufuli alisema bila ulinzi uliofanywa na jeshi gharama zingekuwa kubwa lakini walilinda vizuri na pia alipongeza Suma JKT kwa kujenga ukuta wa uzio na kumaliza kwa wakati mfupi.

Aidha Rais Magufuli aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kutimiza ahadi yake ya kuweka kwenye mabweni hayo vitanda na makabati, ambapo amewaasa wanafunzi watakaotumia mabweni hayo wayatumie na kuyatunza. Katika suala la bei, Rais Magufuli aliutaka uongozi wa chuo hicho tofauti na inavyolipishwa kwa mabweni mengine kiwango cha Sh 800 mabweni hayo wanafunzi walipe Sh 500 kwa siku.

“Nafahamu suala la bei, wanafunzi hua wanalipa Sh 800, sasa Sh 800 sijui aliyejenga mabweni hayo, hapa walipe Sh 500 si nimejenga mimi pesa inayobaki wanunue kalamu wakae wasome, na ninaamini watayatunza mabweni haya,” alisema. Rais Magufuli alisema serikali yake imeamua kuwekeza katika elimu na hasa kwa watoto wa masikini ili waweze kupata elimu na kuongeza pia mikopo imeboreshwa. Aliagiza pia uongozi wa chuo hicho kununua mabasi kwa ajili ya kubeba wanafunzi kutoka mabweni yaliyo mbali na chuo hicho.

Rais Magufuli alimpongeza Katibu Mkuu wa Maji na Umwagiliaji Kitila Mkumbo ambaye amemteua hivi karibuni kwa kwenda CCM na kuuliza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inavyosema katika suala la maji na sasa ameanza kufanya kazi.

Hata hivyo Rais Magufuli alikitaka chuo hicho kuwaachia wanafunzi ambao wanasoma masomo ya afya katika chuo hicho kwenda kwenye Hospitali ya Mloganzila ambayo inatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni na wengine kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambazo ndizo zinazojihusisha na masomo ya afya kwa vitendo.

Awali Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako alimfahamisha Rais Magufuli kuwa hospitali hiyo iko tayari na hivi karibuni watamuomba kwenda kuzindua. Aidha Profesa Ndalichako alimpongeza Rais Magufuli kutimiza ahadi zake kwa vitendo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabweni hayo pamoja na kuboresha sekta nzima ya elimu ambapo alitoa onyo kwa watumishi wengine ambao wanajenga chumba kimoja cha darasa kwa miaka miwili na kwa gharama kubwa.

 

Gallery

Popular Posts

About Us