KINGAZI BLOG: 04/01/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 1 April 2017

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA WAOMBAJI WA UDAHILI WA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA AWAMU YA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017





                                                 BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
                                                                                             (NACTE)

                                                                                    


TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA WAOMBAJI WA UDAHILI WA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA)
KWA AWAMU YA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi liliratibu zoezi la udahili kwa waombaji wa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) kuanzia tarehe 23 Februari, 2017. Zoezi la maombi ya udahili lilifungwa rasmi tarehe 06 Machi 2017 ili kuruhusu uteuzi wa kwa waombaji wa kozi hizo.
Baraza linapenda kuwaarifu waombaji wa kozi za Astashahada na Stashahada; na umma kwa ujumla kuwa, matokeo kwa waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali yametangazwa tangu tarehe 25 Machi 2017 kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) uliotumika kufanya maombi ya udahili. Waombaji wanashauriwa kutembelea kurasa zao (profiles) za kuombea udahili kupitia CAS ili kuona kama wamechaguliwa.
Ili kutembelea ukurasa wako, waweza pia kubofya hapa.
BONYEZA HAPA

Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
Tarehe: 26 Machi, 2017

VIDEO: ‘Tunataka tujue kama tunaibiwa, tumeibiwa kiasi gani?’-Rais Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 01 Aprili, 2017 amewaapisha wajumbe wa Kamati Maalum ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini uliomo ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Kamati hiyo ya Wanasayansi 8 walioteuliwa na Rais Magufuli tarehe 29 Machi, 2017 inaongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Abdulkarim Hamis Mruma ambayo itafanya kazi ya uchunguzi kwa siku 20 kisha kuwasilisha ripoti yake kwa Rais.
Akizungumza baada ya kuwaapisha, Rais Magufuli amesema ameamua kuunda Kamati hiyo yenye wasomi waliobobea katika masuala ya Jiolojia, Kemikali na Uchambuzi wa kisayansi ili wawawakilishe Watanzania zaidi ya Milioni 50 ambao wanataka kujua ukweli kuhusu rasilimali yao ya madini.
“Tunataka tujue kama tunaibiwa, tumeibiwa kiasi gani na kama hatuibiwi, haujaibiwa kiasi gani. Nendeni popote mnapohitaji kufanya kazi tutawapa ushirikiano, fungueni makontena popote yalipo, chukueni sampuli na mkazipime mjue kilichomo na naviagiza vyombo vya dola vihakikishe hakuna mtu atakayewakwamisha.” – Rais Magufuli.
Aidha, Dkt. Magufuli amesema baada ya kuunda Kamati hii ya wanasayansi, ataunda Kamati nyingine ya wachumi na wanasheria kwa ajili ya kufanya tathmini na kuiangalia sera na sheria ya madini kwa lengo la kupata taarifa zaidi juu ya biashara ya madini hapa nchini.
Bonyeza play hapa chini kuitazama.


VIDEO: Yule Mtoto mwenywe uwezo wa kujibu maswali papo kwa papo kataja timu na viongozi


Ikiwa ni siku chache zimepita tangu mtoto Aithamu ataje majina ya viongozi walioteuliwa kufuiatia mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri hususani wizara ya habari,utamaduni,sanaa na michezo na wizara ya sheria na katiba,leo ameelezea jinsi alivyofahamu mabadiliko hayo.
Aitham ambaye ni mzaliwa wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera ametaja pia timu anazozipenda ikiwa ni pamoja na mtangazaji anayemfahamu Tanzania.
Full video nimekuwekea hapa chini…

V

Hii ndiyo Idadi ya mimba alizotoa mwanadada Linah



March 31 2017 kupitia kipindi cha The weekend chat show Msanii wa Bongo fleva Linah Sanga amekiri alishawahi kutoa mimba takribani mbili kabla ya hii aliyonayo sasa hivi na anategemea kujifungua hivi karibu.

Linah amesema anajutia hilo na sababu iliyompelekea kutoa mimba hizo ni kwa sababu alikuwa anamuhofia baba yake kwakuwa hakuwa ameolewa na kudai baba yake alisha watahadharisha juu ya kubeba mimba wakiwa nje ya ndoa wajitenge wenyewe kwenye familia yao.

Mtangazaji Soudy Brown alimuuliza Linah kama alishawai kutoa Mimba na majibu yake yalikuwa haya..>>>“Yah nisiwe muongo nilishawahi kutoa mimba kipindi cha nyuma, nilikuwa naogopa kwasababu Baba yangu alikataa mtu kubeba mimba nje ya ndoa”

“Mimba nimezitoa, siyo mara nyingi ila naweza kusema kama mara mbilii”:-Linah

Wakubwa (18+)MAJANGA.....HAWA NDIO MASTAA WA MAREKANI WANAOONGOZA KWA KUTUPIA PICHA ZA NUSU UTUPU KWENYE MTANDAO WA INSTAGRAM


Mastaa hawa huutumia mtandao wa Kijamii wa instagramu kuonyesha zaidi maungo yao na zisizo na maadili kuliko chochote, kuna wakati Mtandao huu ulifikia hatua ya kuwafungia akaunti zao lakini ndio kwanza wanazidi kufungua account mpya,
Tabia hii ya kutupia picha za nusu uchi  mtandaoni imekuwa ikishabikiwa sana na watu wengi kutoka pande zote za dunia hali inayopelekea kuweza kufahamika zaidi na kujizolea umaarufu mkubwa mtandaoni, 
Pia kuna wakati ilisemekana baadhi ya Mastaa hawa ni miongoni mwa wacheza filamu za ngono hivyo wanaweka picha hizo ili kuwa vutia wateja wa filamu hizo. Hebu ona baadhi ya picha hizo

0








Kumekucha! Bifu la Watangazaji wa Shilawadu na RC Makonda lafikia patamu na limenoga sasa

Image result for shilawadu


Wakiwa katika Kipindi chao ambacho kilikuwa mubashara kabisa Mtangazaji muongozaji wa Kipindi pendwa na Watanzania wengi hadi Mheshimiwa Rais wetu JPM aitwae Soud Brown amekuwa kila mara akifumba Fumbo huku akicheka mno na mwenzake Kwissa.

Ukiwaangalia zaidi utagundua kuwa kwa yale yaliyowatokea wiki mbili zilizopita utagundua kuwa Kipindi chao Kizima cha leo ni kama vile na wao wameamua kulipiza Kisasi kwa waliyofanyiwa na ' Mvamizi ' Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Christian Makonda.

Mtangazaji Soud Brown amekuwa kila mara akifumba fumbo moja hilo hilo huku akilinogesha na Kiitikio na Mistari iliyopo katika Wimbo maarufu wa Ney wa Mitego wa WAPO huku kila mara akimuuliza mwenzie kuwa ' Je mlango wetu umefungwa? '.

Fumbo lenyewe la Mtangazaji Soud Brown ambalo si Siri kuwa amelielekeza ' makusudically ' kabisa kwa ' adui ' yao na ' mvamizi ' wao Makonda ni kama lifuatalo nalinukuu " Hata wanaovua Viatu na Soksi zao zinanuka Wapo........unasema Wapo.......hata wanaonuka Midomo pia Wapo......unasema Wapo.....Oya Kwissa umefunga mlango lakini?...... Jamani hata wanaonuka miguu wakivua Viatu vyao Wapo.......unasema Wapo......hata wanaonuka Midomo sana Wapo......unasema Wapo......Kaka angalia umefunga lakini mlango? Walinzi wapo gado?

Sasa Kazi imeanza na naomba mlio karibu na hawa Watangazi akina Soud Brown na Kwissa mtusaidie kutuulizia kutoka Kwao kuwa huyo anayenuka Soksi na Miguu akivua Viatu ni nani? Halafu na huyo anayenuka mdomo pia ni nani?

Chokoza wote lakini kamwe usichokoze na kuanzisha vita na Waandishi wa Habari kwani wana mbinu nyingi za kukuchafua, kukumaliza na ikibidi hata kukudhalilisha. Pole sana ' mvamizi ' Mkuu wa Clouds nadhani sasa Vita baina yako na wao ndiyo imeanza na imefika patamu mno.

Kuna Watu wanajua mno kulipiza Visasi hasa kwa waliyofanyiwa au mateso ya kimanyanyaso waliyopata.

Nawasilisha.

TAARIFA KUTOKA NACTE KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI / APRILI, 2017

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA

KUFUNGULIWA KWA MFUMO WA PAMOJA WA UDAHILI KWA KIPINDI CHA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuutangazia Umma na wadau wote wa Elimu nchini, kuwa mfumo wa Udahili wa pamoja yaani “Online Central Admission System (CAS)”, umefunguliwa rasmi tarehe 23 Januari, 2017, saa 6 mchana, kwa kupokea maombi ya mwombaji katika kozi mbalimbali, ikiwemo ngazi ya, Astashahada na Stashahada kwa Kipindi cha Machi/April, 2017 kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Namna ya Kufanya Maombi
Maombi yote yafanyike kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) au kupitia chuoni ambapo mwombaji anapendelea kwenda kusoma, ambapo chuo kitamdahili mwanafunzi husika kwenye mfumo wa udahili kupitia “Institutional Panel”.

Tanbihi: Waombaji wa kozi za Afya waliohitimu Astashahada (NTA Level 5), pia wataomba kwa utaratibu ulioelezwa hapo juu.

Mwombaji wa Astashahada na Stashahada anaweza kuomba kwa ajili ya eneo moja au zaidi katika maeneo ya taaluma yafuatayo:
  1. Biashara, Utalii na Mipango, mfano; Uhasibu, Meneja Rasilimali Watu, Wanyama Pori, Mipango.
  2. Sayansi na Teknolojia Shirikishi, mfano; Kilimo, Uhandisi, Mifumo ya Mawasiliano, Usanifu Majengo, Mifugo.
  3. Afya na Sayansi Shirikishi, mfano; Uganga, Maabara, Ufamasia, Uuguzi.
Sifa za muombaji
  1. Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2015 au kabla ya hapo.
  2. Awe na Astashahada ya mwaka 2016 au kabla ya hapo kwa wanaojiendeleza.
  3. Sifa kwa kozi mahsusi ziko kwenye mwongozo wa kozi (Guidebook) ulioko kwenye mfumo (CAS).
Ada ya maombi ni kama ifuatavyo:
  1. Kwa eneo la Afya na Sayansi Shirikishi ada ya maombi ni Tshs 30,000/=.
  2. Kwa eneo moja kati ya maeneo mengine yaliyobaki, ada ni Tshs 20,000/=.
  3. Kwa zaidi ya eneo moja la taaluma, mfano; Afya pamoja na Biashara, ada ni Tshs 30,000/=, ambapo muombaji anaruhusiwa kuchagua maeneo yote.
Mwisho wa kutuma maombi haya ni tarehe 06/03/2017.
Muhimu: Hakutakuwa na muda wa nyongeza wa kufanya maombi. Hivyo waombaji wanashauriwa kuwa makini wakati wa kufanya maombi yao.


Imetolewa na: 
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi

 

Gallery

Popular Posts

About Us