Babu Tale Amchana makavu Erick Shigongo..Adai Magazeti yake Yamefulia na Sasa Anataka Kumwaribia Diamond | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 1 April 2017

Babu Tale Amchana makavu Erick Shigongo..Adai Magazeti yake Yamefulia na Sasa Anataka Kumwaribia Diamond

Baada ya Eric Shigongo kuandika barua ndefu ya kumuonya Diamond kuhusiana na jinsi anavyowawekea ngumu waandaji wa show za ndani kwa kuwatoza bei zile zile kama anavyowatoza wa nje ya nchi na kuhusisha uongozi wa WCB kuwa ni sehemu ya tatizo hilo, Babutale amejibu.

Tale amefunguka mengi huku akimshutumu Shigongo kuwa na hila ya kuharibu biashara zake kupitia magazeti ya Global Publishers.

Kupitia Instagram, Tale ameandika:

Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya…baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako… siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata…ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali…. tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu…

Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie tume kaa kimya… na kujifanya unazunga eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?….. Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? …na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost… ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa….tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na amshabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe….mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa….yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum’bomoa msanii kupitia magazeti yako…..tafadhali heshimu heshima yetu kwako👍…… “Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao…..😓”

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us