HakiAALTONEN JUMBAImageHarusi ya marudio ya Wilson na Anne imeandaliwa katika bustani ya kifahari
Maharusi waliowasisimua wengi baada ya kutumia Sh100 pekee za Kenya kugharimia harusi, wameandaliwa sherehe ya harusi ya kufana jijini Nairobi.
Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya Eden Bliss, Nairobi ulimwengu ukiandhimisha Siku ya Wapendanao.
Harusi ya Anne na Wilson Mutura ya awali iligharimu dola moja pekee ya Kimarekani lakini sherehe ya sasa inakadiriwa kwamba imegharimu takriban Sh3.5 milioni (Dola 35,000).
Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya kifahari ya Eden Bliss viungani mwa Nairobi
Waliofanya harusi ya shilingi 100 za Kenya wapata usaidizi‘Mapenzi yetu yalizidi yote’
Pesa hizo zimegharimiwa na makundi mbalimbali yanayohusika katika uandaaji wa sherehe, ambayo yaliungana kwa pamoja na kuchanga pesa kuandalia Anne na Wilson sherehe ya kukata na shoka.
Wawili hao, wanaoishi eneo la Kasarani, Nairobi, walisifiwa kwa kuonyesha thamani halisi ya mapenzi badala ya kuongozwa na pesa.
Kando na kuandaliwa harusi hiyo, wametunukiwa shamba la kilimo cha kisasa, fungate kwenye hoteli ya kifahari na baada ya sherehe ya leo wanatarajiwa kwenda kwa fungate nyingine mjini Dubai.
HakiAALTONEN JUMBAImageWawili hao wamesafirishwa kwa magari ya kifahariHakiNDUNGU NYORO / FACEBOOKImageBw Wilson akisaidiwa kuweka sawa koti lakeHakiNDUNGU NYORO / FACEBOOKImageBi Anne wakati wa sherehe ya harusi ya marudio
Dola yenyewe walioyotumia Anne na Wilson katika harusi yao waliitumia kununua pete mbili.
Walikuwa wameahirisha harusi yao mara tatu baada ya kukosa fedha za kutosha kuandaa sherehe kubwa ya harusi.
Maombi yao kwa familia na marafiki kuwafanyia mchango, hayakutimizwa.
Baada ya muda, Bwana harusi, Wilson, hakuwa na la kufanya ila kumshawishi mpenzi wake kuhusu uwezo wake.
Harusi za kifahari zapigwa marufuku Somalia
"Wilson aliponieleza hali yake, sikukataa. Mapenzi yetu yalizidi yote," Ann aliambia BBC.
Ingawa walikuwa na uwezo wa kuishi kwa mtindo wa 'come we stay' uliomaarufu kwa vijana wengine ambapo wapenzi wanaishi pamoja bila kuoana, Wawili hao walikwenda kwa askofu Jasper Owach kutoka Kanisa la Community Christian worship centre mjini Nairobi kurasmisha harusi yao.
"Mapenzi yetu yalidumu kwa muda na ili kujistiri kutoka maovu baada ya kupata baraka ya wazazi, tuliamua kufanya mambo yetu rasmi," anasema Wilson.
ImageWilson Muturi na mkewe Ann walitumia dola moja pekee wakati wa harusi yao
Siku yenyewe ilipofika, bwana Harusi, Wilson aliwashangaza waumini baada ya kukimbia nje sherehe ikiendelea.
"Alitoka ghafla kununua pete ya harusi nilipokuwa naendelea na shughuli ya kuwafunganisha," alisema askofu Jasper Owach, ambaye aliongoza hafla hiyo.
Zsa Zsa Gabor, mwigizaji aliyeolewa mara tisa
Wilson alirejea na walipokuwa wanatamka kauli za ndoa, Wilson alitoa pete hizo zilizofungwa kwa gazeti na wakavikana pete.
Wawili hao, wamewarai vijana kutozuiwa na uwezo wao wa kifedha na hivyo basi kuhalalisha mapenzi yao kupitia ndoa.
CHANZO NI BBC SWAHILI