KINGAZI BLOG: 04/06/17

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Thursday, 6 April 2017

TANZIA: Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia

Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia.

Sir Andy amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge.

Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania).

- Historia yake zaidi, tazama video hii;


-----------

Sir Andy Chande akiwa na watu mashuhuri enzi za uhai wake..

Andy Chande Nyerere.jpg 

Akiwa na JK Nyerere

ANDY CHANDE MWINYI.jpg 

Akiwa na A.H. Mwinyi

andy chande mkp.jpg 
Akiwa na BW Mkapa

andy chande JK.jpg 
Akiwa na JM Kikwete

Andy Chande Diamond.jpg 
Akiwa na Diamond Platnumz

andy chande.jpg 
Akiwa na Wanajumuiya wenzake wa Freemasonry


======

SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS
Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi.

Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.

Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.

Siyo hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha mafanikio’.

Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.

Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo.

Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.

Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.

“Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.

Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.

Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra Press.

Anaandika: “Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.

Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.

“Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.

Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.

Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Kanuni za Freemason zinafundisha nini?

Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.

“Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika Chande katika kitabu hicho.

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.

Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu, umakini na haki.

Chande anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.

“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:

“Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu, vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason.

Chanzo: Mwananchi

Kimenuka!!!...Spika wa Bunge ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma.

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.

Pia Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi huo  wa EALA. 

Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo  na anatakiwa kufika leo. 

==>Msikilize Spika Ndugai akitoa maagizo hayo

A

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 6




WEMA AMFUNGUKIA HARMORAPA KUHUSU ISHU YA KUMUOA!!!!!!

MSANII wa filamu nchini Wema Sepetu, ‘Madam’,  ambaye hivi karibuni alihamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amefunguka baada ya Msanii wa Bongo Fleva, Harmorapa kujinadi mtandaoni kuwa yupo tayari kumuoa Wema.
Wema Sepetu
Wema amefunguka na kuandika kuwa anamheshimu Harmorapa kama msanii mwenzie hivyo kitendo cha kujinadi mtandaoni kuwa yupo tayari kuwa na Wema katika mahusiano si sawa ajaribu kwa watu wengine na si yeye.
Harmorapa.
Aidha Wema ameandika kuwa kitendo cha Harmorapa kujinadi ni kumchafulia heshima yake kwa jamii na kwa chama chake cha CHADEMA.
Ujumbe wa Wema Mtandaoni.
NIMEKUWEKEA VIDEO HAPA…
T

VIDEO: "Spika Unaleta Ufala"-- HALIMA MDEE

Nadhan hapa tunapasa kuweka itikadi zetu za vyama ,dini na kabila pembeni. kuna kipindi tunapaswa kusimama kama watanzania tukaweka mambo mengine yote mifukoni mwetu tukabaki na utanzania.

Tanzania ya sasa si tanzania ya jana...inabadilika inakuja na mambo leo ambayo mengine si mazuri. Nimemsikia mbunge mmoja akiongea lugha ya ajabu sana bungeni ambayo sitegemei mbunge msomi na ampambanaji ongee hata kama alikwazika sana. Angalau kistaarabu angeomba msamaha maana wanasema ada ya mja hunena uungwana ni vitendo.

Kwa mbunge kutamka maneno "fala" "mpumbavu" si maneno mazuri ingawa sishangai hili tatizo si kwa wabunge vijana tu . tulishawah sikia mtu mzima mmoja akiitwa wenzie "wapumbavu" si maneno ya kistaarabu tukiacha ashakum si matusi. Kuna lugha za mitaani hizo zisipelekwe bungeni kwa nini wabunge huwa hawapewe semina ya communication skills? maneno kama "kimenuka" "fala", "wapumbavu" hatutegemei kuyasikia bungeni.

Wapumbavu wote basi wanapotamkwa watamkwe pia na huo upumbavu walioufanya au nena wasiishiwe kuitwa wapumbavu. Nimesikitika sana kwa aina hii ya wabunge  ni wapi tulipokosea sisi watanzania?


Najua bado kuna watu watakuja kutukana hapa na kumtetea.Kudhihirisha kuwa tuna taifa ambalo either limeathirika na viroba au matumizi ya bangi lakini sisi wenye akili timamu hatutanyamaza. 
 Tazama Video:

USIPITWE NA HII !! Yule jamaa Aliyemuua Mpenzi Wake na Kumweka Kwenye Jaba la Maji amekamatwa .....kamanda Sirro athibitisha.



JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.
Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro akizungumza na wanahabari.
Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa mwandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;
“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.” Ujumbe ulisomeka hivyo.
Katika hatua nyingine Sirro amesema wamewakamata raia watatu wa kigeni kutoka Afrika Kusini wakiwa na vipande viwili vya meno ya vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 45 na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ambao walikamatwa Machi 28 mwaka huu maeneo ya Upanga Dar.
Sirro ameeleza kuwa upelelezi juu ya watuhumiwa hao bado unaendelea ili kubaini kama walikuwa wanamiliki nyara hizo za serikali kihalali na mawasiliano kati ya Idara Maliasili yanaendelea.
 

Gallery

Popular Posts

About Us