Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizoenea kwamba Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amezuia Wanafunzi wenye Stashahada (Diploma) kujiunga na masomo ya Shahada (Degree) katika vyuo vikuu.
Tuesday, 29 November 2016
Kiuno changu ndicho kinachoniweka Mjini – Gigy Money
Video queen ambaye haishiwi vituko, Gigy Money amefunguka kwa kusema kuwa mauno yake ya mwendokasi ndio kitu ambacho kinawafanya wasanii wengi wamtafute kwa ajili ya kufanya naye kazi.
Mrembo huyo ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, amesema kuwa video queen ni kazi ambayo inalipa tofauti na watu wanavyofikia.
“Unajua kazi yoyote ukiiheshimu ni rahisi nayo ikakuheshimu,” alisema Gigy Money. “Mimi hii kazi naiheshimu ndio maana imeniweka mpaka hapa nilipo. Sasa hivi mimi ni mtangazaji wa kituo kikubwa cha redio, kwa hiyo mimi naweza kuwaambia watu wanatakiwa kuiheshimu hii kazi kama kazi nyingine,”
Aliongeza,”Kusema kweli sasa hivi mimi ni moja kati ya video queen ambao tunafanya kazi nyingi lakini haya yote yanatokana na nikipata kazi naifanya isavyo, napiga mauno ya mwendokasi mpaka mtu labda alipanga kunipa scene moja anajikuta nanipa mbili au tatu,”
Maprofesa wampinga na kumkosoa Ndalichako
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
Na ABRAHAM GWANDU-Arusha
WASOMI, wadau wa elimu na wananchi wa kawaida wamekosoa tamko la Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, wakisema kwamba halijafanyiwa utafiti na halitekelezeki kisheria.
Mwishoni mwa wiki, akiwa kwenye mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Ndalichako alisema kuanzia mwakani mwanafunzi yeyote hatajiunga na masomo ya Shahada bila kupitia kidato cha sita.
Alisema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.
Wakizungumzia tamko hilo kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali nchini, baadhi ya wasomi walisema kabla ya waziri kuanza kutoa amri na matamko, alitakiwa kufanya utafiti kujiridhisha juu ya agizo lake hilo.
“Profesa Ndalichako hajasema ametoa wapi ujasiri wa tamko lake, ni kwa utafiti upi aliofanya yeye au hata kukasimu taasisi kwa niaba yake ili ifanye utafiti na kuja na majibu kuwa kidato cha sita ndicho kiwango bora cha kumpitisha mtu kusoma shahada ya kwanza?
“Binafsi naona haya ni matamko ya kisiasa yasiyoweza kutekelezwa kisheria, arekebishe sheria kwanza ndio aje kutoa tamko la kurekebisha mfumo wa elimu, vinginevyo anaweza kuharibu kuliko waliomtangulia,” alisema mkuu wa chuo kikuu maarufu mkoani Arusha ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Naye Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Tawi la Makumira, Mchungaji Profesa Josef Parsalao, alisema pamoja na lengo zuri la kurekebisha mfumo wa elimu, badala ya kuanza na amri na matamko, Serikali ilitakiwa kurekebisha kasoro zilizopo hatua kwa hatua.
“Sijui yeye Ndalichako alipitia hatua zipi za elimu, lakini upo ushahidi wa kuwapo kwa wasomi wengi wakiwamo wale wanaofundisha vyuo mbalimbali nchini, kupitia ngazi ya chini kabisa ya cheti na sasa ni maprofesa na walifundisha hawa wanaobeza ngazi hizo.
“Wapo majaji ambao walianza kazi ya ukarani mahakamani, wakajiendeleza kwa kusoma Chuo cha Mahakama Lushoto ngazi ya cheti, sasa ni madaktari na maprofesa wa sheria tunawategemea,” alisema Profesa Parsalao.
BANA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, yeye alisema haamini kama alichosema Waziri Ndalichako ni tamko na uamuzi wa Serikali, kwani suala hilo haliko kwenye sera ya elimu na kuonya kuwa alifute haraka kwani hiyo si njia sahihi ya kuboresha elimu nchini.
Dk. Bana alikwenda mbali zaidi kwa kutoa mfano wa jinsi yeye alivyosoma kupitia mfumo huo unaopingwa na Ndalichako hadi hapo alipofikia.
“Kama kachukua uamuzi huo, nafikiri amekurupuka, kama anafikiria kidato cha sita ndiyo njia pekee, ameshauriwa vibaya na huo uamuzi aufute haraka sana na ni kinyume na utaratibu wa elimu kote duniani… utakuwa ni uamuzi wa dhambi ya asili na dhambi ya ubaguzi. Kama anataka njia ya kuboresha elimu aje tumfundishe.
“Mimi binafsi sikupitia kidato cha sita na kuna maprofesa zaidi ya 20 au 40 ninaowafahamu, yupo Profesa Baregu (Mwesiga Baregu) hakusoma kidato cha sita, kuna Profesa Mathew Luhanga ambaye alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa miaka 14, yupo pia Profesa Cuthbert Kimambo ambaye alikuwa Mkuu wa Taaluma UDSM na wengine wengi, ni watu wanaoheshimika kote duniani,” alisema.
PROFESA BAREGU
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Profesa Mwesiga Baregu, hakutofautiana na Dk. Bana. Yeye alisema mfumo uliopo unakubalika duniani kote na ndio ulioleta msemo wa ‘elimu haina mwisho’.
“Kauli ya waziri imeonyesha umuhimu wa kuwa na tume ya kitaifa ya kushughulikia suala la elimu, kwa sababu kweli kuna tatizo la ubora wa elimu yetu na halipaswi kunyamaziwa, lakini hii si njia sahihi ya kulitatua.
“Sijamwelewa waziri kwanini ameona diploma kwenda chuo kikuu ndiyo tatizo na kusema kuwa watu wote wana haki ya kujengewa mazingira ya kujiendeleza kielimu,” alisema Profesa Baregu.
PROFESA MPANGALA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa (RUCO), Profesa Gaudence Mpangala, alisema anapinga uamuzi huo wa Profesa Ndachako kwani utawanyima watu uhuru wa kujiendeleza.
Profesa Mpangala naye aliwataja baadhi ya maprofesa anaowafahamu ambao hawakupitia kidato cha sita na akasema wamekuwa msaada mkubwa kwa taifa.
“Profesa Kimambo alikuwa mwalimu wangu wa Kiswahili, yeye alikuwa na elimu ya ualimu ‘Grade’ C wa shule ya msingi lakini amejiendeleza hadi amekuwa Profesa yupo pia Profesa Ndunguru na wengine wengi na waliopitia mfumo wa Cheti-Stashahada wanakuwa na uzoefu mkubwa kuliko wa kidato cha sita na wanafanya vizuri wakifika chuo kikuu,” alisema Profesa Mpangala.
TAMONGSCO
Akizungumzia kauli hiyo ya Profesa Ndalichako, Katibu Mkuu wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania, Benjamini Nkonya, alisema hawaelewi waziri huyo kutoa tangazo kama hilo ni kwa sababu watu wengi wamekuwa watumishi bora sana na wengi hawajasoma kidato cha sita au vinginevyo.
“Wito wetu kwa Serikali ikamilishe mchakato kwa kupeleka rasimu ya sheria mpya ya elimu bungeni, ili pawepo na Baraza la Taifa la Elimu ambalo litakuwa na wawakilishi kutoka sekta ya umma, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na sekta binafsi kama TAMONGSCO, ambayo itaandaa nyaraka (regulations) zote kabla hazijawekewa sahihi na kamishna wa elimu,” alisema Nkonya.
PROFESA MLAMA
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Penina Mlama, yeye alikubaliana na mawazo ya Waziri Ndalichako, akisema mfumo huo ni wa zamani na uliruhusiwa ili kutoa fursa kwa watu kusoma kwa kuwa nchi ilikuwa na wasomi wachache.
“Sasa hivi kuna wanafunzi wengi wa kidato cha sita na fursa nyingi za kusoma kidato cha tano na sita zipo, tofauti na kipindi cha miaka ya nyuma, hakuna ulazima sana wa watu kutegemea njia yingine wakati wanaweza kusoma kidato cha sita na kuwa sawa na wengine darasani,” alisema.
LALTAIKA
Kaimu Mkuu wa Idara ya Ubunifu, Usimamizi wa Teknolojia na Ujasiriamali katika Taasisi ya Sayansi ya Nelson Mandela, Dk. Amani Laltaika, alipongeza hatua ya Profesa Ndalichako, huku akisema amegundua tatizo katika elimu na amethubutu kuchukua hatua ya kurekebisha kuliko waliomtangulia ambao hawakuchukua hatua yoyote.
“Sifa ya kwanza ya kiongozi ni ubunifu na kutatua matatizo yaliyopo, nampongeza waziri kwa kugundua upungufu katika elimu yetu, kwa sababu walikuwapo mawaziri wengi katika nafasi aliyopo sasa, lakini hawakugundua,” alisema Dk. Laltaika.
SIFA ZA TCU KUJIUNGA NA VYUO
Mwezi Juni mwaka huu, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), ilitangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016 na 2017 wanaochukua shahada.
Utaratibu huo mpya ulikuja baada ya miezi miwili tangu kutumbuliwa kwa watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mikopo na Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Pamoja na sifa hizo ambazo ziliwahusu waliomaliza kidato cha sita, pia sifa hizo zilieleza kuwa wale watakaodahiliwa kujiunga na vyuo ni pamoja na watakaokuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne kuanzia alama nne ambazo ni D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A=75-100, B+=65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39 na F=0-38.
Sifa nyingine zinazotajwa ni wenye vyeti vya NVA daraja la tatu, wenye ufaulu si chini ya alama nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na Baraza ka Taifa la Mitihani (NECTA) na Elimu ya Mafunzo ya Ufundi (VETA).
Watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada ‘NTA’ daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi ‘FTC’ katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo.
Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udahili huo ni pamoja na kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye Stashahada zisizokuwa za NTA.
Imeandaliwa na Abraham Gwandu (Arusha), Jonas Mushi na Mauli Muyenjwa (Dar)
Source: Mtanzania
Masharti Ya Kumtext Mwanamke - Makosa 5 Wanaume Wanayofanya
Kila siku mara moja au nyingine huwa tunawatext wanawake. Aidha wawe ni wapenzi wetu, tunaowatongoza ama marafiki zetu. Na kila siku huwa tunapatwa na changamoto mbalimbali kutokana na matangamano yetu. So huwa kunakosekana nini? Ifuatayo ni orodha ya mambo 5 makuu ambayo wanaume wengi hukosea wakati wanapomtext mwanamke, na jinsi ya kutatua.
#1 kukata tamaa mapema kwa mwanamke
Kosa kuu ambalo wanaume wengi hufanya ni kukata tamaa mapema wakati wanapomtext mwanamke. Watamtext mwanamke, na kama hatajibu jumbe zake (ama kujibu kiuchache) watachukulia kuwa mwanamke huyu amepoteza interest na wanakata tamaa. Hili ni kosa kuu sana.
Kama inavyojulikana kikawaida ni kuwa mwanamke anaweza kutojibu meseji zako, na sababu hizo hazina uhusiano moja kwa moja na kutokuwa na interest kwako. Kwa mfano, anawezakuwa labda yuko busy, katika mood mbaya, ama labda hayuko sure ni kitu gani cha kukujibu kwa meseji. Kiufupi ni kuwa haujui kile ambacho kinazunguka kwa akili ya mwanamke, so haina haja ya kufikiria jambo baya.
So, iwapo kama mwanamke hakukujibu ama hayuko interested na wewe, lakini bado unataka kuongea na yeye, hivi ndivyo unavyopaswa kufanya; Mpe muda wa kutosha (siku chache ama hata wiki) halafu anza kumhusisha kwa meseji. Kama vile texts zozote za kawaida, hapa utakuwa unataka kuhakikisha kuwa unamvutia, unamfurahisha na unamchesha. Na zaidi ni kuwa unapaswa kutafuta swali ambalo litamlazimu yeye kureply meseji yako. Yote hayo, huu hapa ni mfano mzuri wa meseji ambayo itamhusisha mwanamke yeyote:
Hello mrembo...hivi kweli uko hai? Nitume kikosi cha maninja kije kikunusuru ama?
Yaweke maneno yako kuwa ya ucheshi, yawe na kamchezo flani na bila shaka utamfanya huyu mwanamke kutabasamu na kuwa katika hali ya kuchangamka. Kama utaweza kumfanya atabasamu basi muda mchache tu atakujibu.
2. Kutext mara nyingi.
Hakuna kitu ambacho kinaweza kuua nafasi yako kwa mwanamke kama kumtumia jumbe mara nyingi. Humfanya mwanaume aonekane mwenye tamaa hivyo kumfukuza mwanamke.
Kwa kuepuka haya yote hizi hapa ni njia unazoweza kuzitumia ambazo zinaweza kukusaidia kumtext mwanamke wakati sawa.
♥Unapomtext mwanamke, hakikisha kuwa jumbe zinakuwa 1:1, Unahakikisha kuwa kila meseji anayotuma unaijibu na moja (pia hakikisha urefu unakuwa sambamba)
♥Acha kumtext na jumbe zisizo na mwelekeo. Usimjibu mwanamke jumbe wakati ambapo haihitaji jibu. Kwa mfano, si lazima uijibu text ya mwanamke ya 'usiku mwema' kama utamwambia 'nawe pia'. Ikifikia hatua hii mazungumzo yenu yatakuwa yameisha. Inachotakiwa kutoka kwako ni kuhakikisha kuwa jumbe ya mwisho inaisha kutoka kwake.
♥Weka fikra ya wengi. Wakati ambapo unamtext mwanamke mmoja, huwa kawaida unakuwa na mtazamo finyu wa kumfiria sana mwanamke huyu ukiogopa asikuache. Well, kutatua swala hili, lile unalotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa katika akili yako weka ya kuwa una wanawake kadhaa ambao wanakufukuzia. Hii itakusaidia kuondoa uhitaji mwingi wowote.
3. Kuchukulia jumbe unazomtumia serious.
Kuna hali tofauti tofauti ya kuwa serious na mwanamke wakati wa mazungumzo lakini kutumia jumbe si moja wapo. Kujifanya kuwa serious wakati wa kumtext mwanamke kunachosha na hakuna mtu anapenda. Hivyo weka seriousness zako mbali kabisa na ulete hali ya ''nataka-tujuane-nawe''. Wakati unapomtext mwanamke, unapaswa kumakinika kuleta furaha.
Sasa, njia nzuri ya kuhakikisha kuwa unamfanya mwanamke anakuwa na shangwe wakati wote ni kwa kutumia 'emoticons'. Wanaume wengi wanajitenga kutumia emoticon wakidhania kuwa ni mambo ya wanawake, ukweli ni kuwa ni mambo ya wanawake na wanawake wanapenda kutumia emoticon. Pia zinasaidia kwa kuwa kile utakachokisema kwa kutumia emoticon mwanamke hatakipuuza. Hatobahatisha hisia zako kamwe kwa kuwa emoticon zinasaidia kupitisha ujumbe unaodhaminia. Na matokeo yake ni kuwa unaepukana na drama zozote zitakazojitokeza.
4. Kutotext wanawake wengi.
Wakati mwanaume anatext mwanamke mmoja, ni rahisi kwake kumaliza maongezi yake mapema kwa kuwa hana fikra pevu kama vile tulivyotangulia kusema awali. Kama unataka kuwa na fikra pevu na uwezo rahisi wa kutangamana na wanawake basi ni lazima uwe unatext wanawake wengi. [Soma: Njia 5 rahisi za kumwomba mwanamke namba ya simu]
Kufanya mazungumzo mengi na wanawake wengi kunakupa ufahamu na mbinu pana za kuweza kuzungumza na wanawake. Ustadi huu utakuja wenyewe iwapo utajikita kuongea na wanawake wengi na tofauti tofauti katika meseji zako. So kinachohitajika kwako ni kutafuta namba za wanawake tofauti tofauti na uanze kuongea nao kupitia jumbe.
5. Tunasahau lengo kuu la kumtext mwanamke.
Wakati mwingine wanaume wanasahau kwa nini wanawatumia jumbe wanawake. Wanakita kuongea mambo ya mbele, nyuma na ovyo bila msingi wowote ule. Wanasahau ile taswira kuu ya kumtext mwanamke. Taswira kuu kama tujuavyo ni kuhakikisha unatoka deti na mwanamke huyu.
Lakini usichukulie kuwa kuchat na mwanamke kupitia texts imepangwa, la. Unapaswa kutumia mfumo ule wa kawaida wa kuleta ucheshi, mzaha nk, kama tulivyoelezea awali. Hivyo basi, mbinu zako za kumtext mwanamke lazima ziwe za kuvutia, za nakshi na ambazo zitaleta msisimko ndani yake. Kama utamtext mwanamke bila mpangilia ama lengo flani, basi bila shaka atapoteza hamu na kuenda zake.
By Nesi Mapenzi
Chanjo Dhidi ya Ukimwi Kufanyiwa Majaribio Afrika Kusini
Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii.
Wanasayansi wanasema huenda ikawezesha binadamu kukabiliana na virusi hivyo iwapo itafanikiwa, shirika la habari la AP linasema.
Wakati wa majaribio hayo, ambayo yamepewa jina HVTN 702, wanasayansi wanatarajiwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400 ambao wanashiriki ngono kutoka maeneo 15 nchini Afrika Kusini.
Washiriki hao watakuwa wa umri wa kati ya miaka 18 na 35.
Majaribio hayo yatakuwa makubwa zaidi na ya kina zaidi ya chanjo ya Ukimwi kuwahi kufanyika nchini Afrika Kusini ambapo zaidi ya watu
"Ikitumiwa pamoja na silaha tulizo nazo sasa za kuzuia maambukizi, chanjo hiyo inaweza kuwa msumari wa mwisho katika jeneza la Ukimwi,"
Anthony Fauci, mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Maradhi ya Kuambukizana na Mzio ya Marekani (NIAID) amesema kupitia taarifa.
"Hata kama mafanikio yake yatakuwa ya kadiri, hilo linaweza kupunguza pakubwa mzigo unaotokana na maradhi hayo katika nchi zenye viwango vya juu vya maambukizi, mfano Afrika Kusini."
Chanjo ambayo itafanyiwa majaribio chini ya HVTN 702 ina uhusiano na majaribio ya chanjo yaliyofanywa mwaka 2009 nchini Thailand.
Chanjo iliyofanyiwa majaribio mwaka huo iligunduliwa kuwa na mafanikio asilimia 31.2 katika kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika kipindi cha ufuatilizi cha miaka 3.5 baada ya mtu kupewa chanjo.
Wanasayansi wametayarisha chanjo hiyo mpya mahsusi kutoa kinga pana na kwa muda mrefu na kwa kuangazia zaidi aina ya virusi vinavyopatikana kusini mwa Afrika.
Watakaoshiriki katika majaribio hayo ni watu wa kujitolea.
Wanachaguliwa bila kufuata mpangilio wowote, ambapo kundi moja litapokea dozi ya chanjo kwa kipindi fulani na jingine kipimo kisicho cha chanjo. Washiriki wote watadungwa sindano tano katika kipindi cha mwaka mmoja.
Washiriki watakaoambukizwa virusi vya Ukimwi katika kundi hilo watatumwa kwa wahudumu wa afya ili kupokea matibabu ya kupunguza makali ya virusi hivyo na pia kushauria jinsi ya kupunguza hatari ya kueneza virusi hivyo.
Afrika Kusini ina zaidi ya watu 6.8 milioni ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi.
Taifa hilo hata hivyo limezindua mpango mkubwa wa kutoa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo na kuudhibiti, mpango ambao inasema ndio mkubwa zaidi wa aina yake duniani.
Kiwango cha wastani cha umri wa kuishi kilikuwa kimeshuka sana nchini humo na kufikia miaka 57.1 mwaka 2009 lakini kutokanana na juhudi hizo, kimepanda hadi miaka 62.9 kufikia 2014.
Matokeo ya majaribio hayo ya chanjo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka 2020.
VIDEO :KAULI YA NDALICHAKO KUHUSU WANAFUNZI WASIOFIKA FORM SIX KUTOJIUNGA NA CHUO KIKUU
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizoenea kwamba Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amezuia Wanafunzi wenye Stashahada (Diploma) kujiunga na masomo ya Shahada (Degree) katika vyuo vikuu.