
Baada ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kukwama tena kupata dhamana mahakamani jana, amewataka mawakili wake kutomhangaikia na kuliacha suala hilo kama lilivyo na atakaa gerezani hadi Januari mwakani.
Akizungumza baada ya Mahakama Kuu kuondoa rufaa ya mbunge huyo aliyekuwa akipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumnyima dhamana, Wakili wa Lema, John Malya alisema mteja wake...