KINGAZI BLOG: 11/18/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday, 18 November 2016

Kinara wa Matusi Instagram Akamatwa na Polisi Baada ya Kutoa Matusi Makubwa Kuhusu Perfume Mpya ya Diamond


Kijana mmoja ambaye anatumia jina la Shilolekiuno_official Huko Instagram  hatimae amekamatwa na jeshi la polisi kwa kutukana na kukashifu watu mbali mbali mtandaoni, kijana huyo amekuwa akiandika matusi mazito na kukashifu watu mbalimbali akiwemo Mwanamuziki Diamond,

 Jana Baada ya Diamond Kutangaza Kuleta Perfume mpya zenye jina lake sokoni, mtu huyo anayetumua jina la @shilolekiuno_officail aliingia mtandaoni na kuandika matusi makubwa ambayo siwezi kuyaweka hapa kuhusu Perfume hiyo ya Diamond

Meneja wa Diamond Ameandika Haya:



Lemutuz Naye Ameandika Haya:



Zahanati ya India kumtibu mwanamme mrefu zaidi Tanzania

Zahanati moja nchini India imejitolea kumsaidia mwanamme kutoka nchini Tanzania, ambaye aliambiwa kuwa kutokana na urefu wake, hawezi kufanyiwa upasuaji nchini Tanzania.


Baraka Elias aliye na urefu wa futi 7.4 au mita 2.20, anahitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia

Daktari katika zahanati ya Speedy Recovery, ameiambia BBC kuwa wanaweza kumsaidia Baraka Elias, ambaye madaktari mjini Dar es Salaam wanasema hawezi kutoshea katika kitanda cha hospitali.

Elias aliye na urefu wa futi 7.4 au mita 2.20, anasema anahitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia alipoanguka.

Pia aliambiwa kuwa hangeweza kutoshea kwa mashine ya X-ray kutokana na urefu wake.


Baraka Elias akiwa amesimama na mwandishi wa BBC Lizzy Masinga

"Nina uhakika kuwa bwana Elias atapata nafuu hivi karibuni, wakati akifahamu kuwa kuna mtu mbali sana anajaribu kumfanyia maabo kuwa sawa," Dr Shaila Raveendran anayeongoza zahanati ya Speed Recovery nchini India, aliambia BBC.

Bwana Elias anatajwa kuwa mtu mrefu zaidi nchini Tanzania.

Mwanamke Afa Akiombewa Kwa ‘Nabii’, Akutwa Hana Nywele Kichwani Pamoja na Nyusi za Macho


Mwanamke mkazi wa Unga-Limited jijini hapa, Lightness Kivuyo ameripotiwa kufa wakati akifanyiwa maombi nyumbani kwa mchungaji aliyejulikana kama ‘Nabii Rajabu’ eneo la Kwa-Mrombo pia jijini hapa.

Kwa mujibu wa dada wa marehemu, Juliana Kivuyo, Lightness alikuwa amesindikizwa nyumbani kwa nabii huyo nyakati za usiku na mumewe aliyemtambulisha kama Shafii Mohammed na kwamba wakati akifanyiwa ibada ya maombi, alianguka na kufariki miguuni mwa ‘Mtume,’ huyo.

“Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema, huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali mbaya kule kwenye maombi,” alisema Juliana na kuongeza kuwa alitoka mbio kwenda Kwa-Mrombo nyumbani kwa Nabii Rajab na kumkuta dada yake amelazwa kwenye kochi, akiwa bila nguo isipokuwa tu khanga alizofunikwa nazo.

Nabii huyo pia anadaiwa kumnyoa nywele zote pamoja na nyusi za macho wakati akimfanyia ‘huduma,’ hiyo.

Polisi jijini hapa wamethibitisha tukio hilo wakiongeza kuwa tayari watu wawili wamekamatwa kutokana na kifo hicho cha ‘maombi tatanishi.’

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo ameongeza kuwa atatoa taarifa kamili mara baada ya kikao chake na Mkuu wa Mkoa.

Mganga Mkuu katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Jacqueline Uriwo amekiri kupokea mwili wa marehemu, lakini akasema, “Kwanza walijaribu kutudanganya kuwa huyo mama alikuwa hai na kwamba aliletwa kwa ajili ya matibabu, lakini tukagundua kuwa walichokileta ni mwili mfu, hivyo tukampeleka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti!.”

Mkurugenzi wa Huduma ya Mazishi katika hospitali hiyo ya mkoa, Dk Francis Coster alisema mwili ulipelekwa hapo na mume wa marehemu ambaye alisisitiza kuwa mkewe hajafa, bali kazimia tu na kwamba mara nyingi huzimia kwa saa nyingi.

Dk Coster aliongeza kuwa ilibidi na wao wasiweke mwili kwenye jokofu na kuulaza kwenye machela kwa saa sita na ndipo wakaamua kuuweka kwenye droo za maiti, kwani ilikuwa wazi sasa kwamba asingeamka tena asilani.

Waganga hospitalini hapo wamekiri kuwa mwili wa marehemu uliletwa hospitalini hapo ukiwa umenyolewa upara, lakini ukiwa na mikwaruzo pamoja na uvimbe hususan maeneo ya mikono na kifua.

Baba mkubwa wa marehemu, Ally Kivuyo ambaye ndiye mlezi wa Lightness, alisema mume wa marehemu alimtaarifu juu ya kifo hicho na kuongeza; “Lakini baadaye nikaletewa taarifa nyingine kuwa Lightness kumbe alikufa wakati akifanyiwa maombi au vitu vingine, nyumbani kwa mtu anayeitwa ‘Nabii Rajabu,’ hapo basi ikabidi niwataarifu polisi ambao walikuja kumkamata mumewe pamoja na huyo anayejiita nabii au mtabiri.

Source: Habari Leo

UKWELI KUHUSU PAPA KURUHUSU TALAKA KWA NDOA ZA KANISA KATOLIKI


Wenzetu nchi zilizoendelea waandishi wa habari wanaoandika habari za aina fulani ni lazima wawe ma uweledi wa jambo hilo.Ukiwa unaandika habari za uchumi,basi ni lazima walau uwe na ABC za mambo ya uchumi,siasa kadhalika,habari za afya na hata zile za mambo ya uhandisi.Ndio maana si ajabu kukuta mwandishi wa habari kaandika habari za mambo ya usafiri wa anga,akaandika "Kutana na mwanamke wa kwanza kurusha ndege aina ya BOEING AIRBUS".Wakati kiukweli hakuna aina ya ndege hiyo duniani.

Habari za kanisa,pia zinahitaji walau mwandishi awe na ABC za mambo ya kanisa na kupata ufafanuzi wa uelewa wa mambo mengi ndani ya kanisa.

Kuna habari inazagaa,na imetolewa ufafanuzi makanisani,sio kweli kuwa Papa ameruhusu "Talaka" kwa ndoa za kanisa katoliki,ila ukweli ni kuwa Papa amerahisisha njia za "utatuzi wa migogoro" ya ndoa ndani ya Kanisa Katoliki.

Ifahamike kuwa toka miaka na miaka,ndoa za kanisa katoliki zimekuwa zinafuata mlolongo mrefu pale zinapoonekana kuwa zina hitilafu ili kuweza kuwa "invalid".Kutokana na elimu ndogo juu ya sheria za ndoa ndani ya kanisa kwa waumini,wapo waumini wengi wanaodhani hawawezi kubatilisha ndoa zao hasa kama zilifungwa bila kufuata vigezo.

Sasa badala ya maamuzi haya kufanyika Vatican kwenye Mahakama ya Ndoa "Rota Romana" sasa jambo hili limaweza kuwa mikononi mwa Askofu Mkazi.Hivyo kuondoa ule mlolongo wa mtu kutoka kigango cha Luhumbo Kishapu Jimbo la Shinyanga kwenda Rota Romana Vatican na sasa mtu huyo ataenda Cathedral Ngokolo Shinyanga kupeleka shauri lake.Huu ndio msingi wa ujumbe wa Papa,kuleta madaraka katika majimbo mahalia.

Kuna kutazamwa kwa ndoa zilizobatilishwa kwa namna mbili,ya kwanza ni "Annulamento",hii ni ndoa inayotenguliwa mahakama za kiraia lkn kanisa linakuwa kinaendelea kuitambua kama ni ndoa "valid" sbb kuharamishwa kwake hakujafuata taratibu na sheria za kanisa,bali za kidunia.Mahakama huzibatilisha ndoa hizi kutokana na "magumu ya dunia".Hivyo Mahakama za kidunia hutalakisha ndoa ambayo ni "valid" kikanisa.Kanisa katoliki inawachukulia watu hawa ni wanandoa,na hiyo inakuwa ni "impediment" kwa wao kufunga ndoa nyingine.

Namna ya pili ni "Nullità",kingereza ni "Nullity".Nullity maanake hiyo ndoa toka "inazaliwa" haikuwa ndoa halali na hivyo kanisa inaibatilisha.Ndiyo maana kanisa katoliki hutangaza ndoa husema "wenye kizuizi",na matangazo huwa kwa muda mrefu na hutangazwa mahali pote wanandoa walipowahi kuishi.

Kuna sababu za Mahakama ya Kanisa ku-nullify ndoa iliyofungwa kanisani,sababu hizo ni kama vile

Uhuru,iwapo itathibitika pasi na shaka kuwa mmoja kati ya wanandoa alilazimishwa.Kumficha mwenzako kama ulikuwa na watoto njeKuficha kuwa upo huru wakati ulishafunga ndoaKuwa impotent (hanisi/tasa) bila uwazi kablaKwa Padre kufunga ndoa na mwanamke bila yeye kusema ni padre

Ili mtu upate kibali cha kufunga ndoa ya pili hizo juu ni sababu mojawapo katika kanisa katoliki, inabidi upate kibali kutoka katika "Mahakama ya Kanisa".Hizi mahakama za "Nullity of Matrimony" zipo katika kila Jimbo Tz,huundwa na mahakimu watatu ambapo hata walei wanaweza kuwepo lkn katika hao watatu ni mkleri ambaye anatakiwa awe kiongozi.

Askofu wa Jimbo lolote anaweza kutoa "nullity" kwa ndoa zile ambazo evidence zake zipo wazi.Kila jimbo palipo na askofu tayari ile ni mahakama.Sasa Maaskofu wanaweza kukubaliana wakaunda mahakama moja inayojumuuisha majimbo kadhaa.Mfano Mahenge,Kilosa na Morogoro wakawa na mahakama moja.

Na katika kila shauri la "Nullity of Matrimony" huwa yupo Padre mwingine kwa ajili ya "defend of matrimony",ambaye lazima awe padre aliyebobea katika sheria za kanisa(Canon law).Na hata wakitokea wanandoa wanakubaliana yeye huwa against na huweza ku-appeal mahakama ya juu ili ndoa hiyo isiweweze kuwa "invalid"

Kuna muundo wa Kimahamaka pia ndani ya kanisa,toka Mahakama ya mwanzo hadi rufaa.Hii huanzia kwa mahakama za kijimbo,ikishindikana shauri hupelekwa kwenye mahakama ya Metropatania(Jimbo Kuu),hapo ikishindikana shauri hupelekwa kwa Askofu Mkongwe(Kwa umri) ktk eneo husika na rufaa ya mwisho huwa Rota Romana Vatican.

Wenzetu wa nchi zilizoendelea,ambao elimu ya sheria za kanisa hutolewa kwa waumini wa kawaida kwa nafasi na uwazi,mambo haya wanayafuatilia na kufahamu.Wapo wakristo Afrika ambao ndoa zao ni "invalid",lkn kwa "kukaririshwa" kuwa ndoa za Kanisa ni mpaka "kufa na kuzikana" basi wanaendelea kukaa katikati ya uvuli wa mauti,lkn kumbe wanaweza kufuata hatua hizi na endapo ikathibitika pasi na shaka,basi ndoa zao zinakuwa "Nullified".Sasa Papa kapunguza mlolongo huu,na sio karuhusu "talaka"

Zamani mashauri haya yote yaliruka moja kwa moja mpaka Rota Romana,Vatican,lkn sasa imerahisishwa,kurahisishwa huku kwa kuanzia ngazi ya Maaskofu,basi waandishi wasiotafiti wanaishia kusema "Papa aruhusu Talaka ndoa za kanisa Katoliki".

HABARI KUU KWENYE MAGAZETI YA LEO IJUMAA YA NOVEMBER 18



























 

Gallery

Popular Posts

About Us