
Wakazi wa Isanga Jijini Mbeya wamekumbwa na taharuki baada ya tukio lisilo la kawaida ambapo maiti iliyokwenda kuzikwa katika makaburi ya zamani ya Isanga ilikutwa ikiwa kwenye godoro ndani ya nyumba alimofia.Taarifa yaJeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya inasema kuwa tukio lilitokea mnamo tarehe 16.01.2017 majira ya saa 4:30 asubuhi katika mtaa wa Igoma “A”, Kata ya Isanga, Jijini Mbeya.Kufuatia taarifa...