KINGAZI BLOG: 09/04/16

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday, 4 September 2016

TRA yakusanya trilion 1.158 kwa mwezi Agosti na kuvuka lengo, Kariakoo kuwa mkoa maalum wa kodi


KATIKA harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuongeza wigo wa vyanzo vya Mapato pamoja na kukusanya Mapato kikamilifu.

Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo;
Kulifanya eneo la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini na kuhakikisha kila mfanyabiashara anakuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.
Katika kutekeleza hilo Mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika jengo la Al-Falah Towers lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika matumizi ya mashine hizo.
Aidha Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo ametoa wito kwa wananachi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo vifuatavyo kwaajili ya zoezi hilo kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo maana baada ya tarehe hiyo zoezi hili litahamia mikoa mingine.

Vituo hivyo vya uhakiki ni pamoja na:
Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara.
Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
Wilaya ya Kigamboni: Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji.

Wakati huo huo Bw. Kayombo amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo la Serikali la kufunga mashine za EFDs kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2016 kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe 1 Oktoba na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.

Katika kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani - VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla au tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka hu wa fedha.

Kwa upande wa walipa kodi zaa makadirio na kodi za makampuni (Corporation Tax) wanakumbushwa kulipa kodi zao mapema mwezi hu wa tisa badala ya kusubiri msongamano mwisho wa mwezi ambao unaweza kuwasababishia usumbufu.

Hivyo hivyo walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.

Kutokana na mikakti mizuri iliyowekwa na uiongozi wa TRA na serikali Mpaka sasa baadhi ya mikakati hiyo imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 TRA imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57. ambapo Mwezi Agosti mwaka 2015 TRA ilikusanya billioni 923.

Wito wetu kwa wanahabari na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kutuunga mkono kwa kuhimiza kutoa risiti pamoja na kudai risiti katika kila manunuzi pamoja na kutoa taarifa za dalili za ukwepaji wa kodi wa aina yoyote mahali popote nchini

TAJIRI ANUNUA NDEGE YA BOING 747 JUMBO NA KUIGEUZA NYUMBA YA LODGE

Ndani ya ndege hii "nyumba ya kulala wageni" kuna vyumba 27, unapata utandawazi, vumba vina luninga, imesha aanza kuchukwa wageni wa kulala na ipo karibu na uwanja wa ndege wa  Arlanda airport karibu na mji wa Stockholm, Sweden

Hii ni sehemu iliyokuwa ya rubani wa ndege hiyo unaweza kulala hapa kuanzia  £170 kwa usiku mmoja..NA JESTINA GEORGE



Nyumba hiyo ya wageni ambayo sasa iko tayari kwa biashara imewekwa karibu na uwanja wa ndege wa  Arlanda airport karibu na mji wa Stockholm, Sweden

Mmiliki wa ndege hiyo Oscar Divs alinunuwa ndege hiyi iliyoundwa 1976 Boeing 747-200 na kuibadilisha kuwa nyumba ya wageni 

Moja ya chumba katika ndege hiyo


Moja ya chumba cha wageni ambacho kina, flatscreen TV and WiFi


Sehemu ya kupumzikia

HIZI HAPA DALILI NANE (8) ZA MWANAMKE ANAYETOKA NJE YA NDOA

Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo kwa mwanaume. 

Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume. Bado nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa.  Uchunguzi wa kina kufuatia dalili hizi ni muhimu sana.

 Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke ambaye anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake:

 1. KUCHELEWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata mara tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila kujali soko liko umbali gani. Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.

 2. KUBADILI MAENEO: Hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu, hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya.

 Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana msingi, mwanaume ana kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti unaofanywa.

 3. UNUNUZI USIO WA KAWAIDA: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi. 

 Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama nyumba kwa siri.

4. KUANZISHA VURUGU: Kuna wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda. 

Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa hawara yake.

 5. KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe, yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa wanashiriki. 

 Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.

 6. KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana. 

 Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake.

7. KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake. 

 Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana kwamba, anahofia kuna siri itatoka au kuna kitu ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke anayetoka nje , hasa katika hatua zake za awali za kutoka nje.

 8. KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona vipi , wanaweza kuachana. 

 Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke anakimbilia kusema, “kama ni kuachana, tuachane tu” hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe

Picha 3:JAMAA AAMUA KUCHINJA MBWA NA KUWAUZIA WATU KAMA NYAMA..... HEBU JIONEE HAPA




TOP TEN YA WASANII WAKIUME WANAOWAVUTIA ZAIDI WANAWAKE WAWAPO JUKWAANI


01: DIAMOND PLATNUMZ
Jina lake kamili ni Nassib Abdul, huyu wengi wamempachika jina la sukari ya warembo, idadi kubwa ya wanawake wanampenda kutokana na mwonekano wake na pia uwezo wake mkubwa wa kucheza na sauti anapoimba ingawa wengi hudai hana sauti nzuri lakini huvutiwa na namna anavyoweza kuitumia sauti hiyo na kuwa kivutio katika nyimbo zake.
Maonyesho yake hujaza watu wengi lakini inakadiriwa wasichana wengi hujitokeza katika matamasha ambayo hutangazwa kwamba msanii huyu atakuwepo, pia wengi wao hutamani kumshika msanii huyu ndiyo maana wengi wao hukimbilia kumtunza.

02: ALI KIBA
Msanii huyu anayetamba na wimbo wa ‘Mwana Dar’ na ‘Chekecha Cheketua’ jina lake kamili ni Ally Salehe Kiba, licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kuimba na kucheza lakini wanawake wengi huvutiwa na uwezo wake wa kuchezea sauti yake katika kuimba na pia mwonekano wake akiwa jukwaani ndiyo maana mashabiki wake huwa wakimshangilia kwa sauti na kelele zote wapendavyo kila anapokuwa jukwaani.

03: CHRISTIAN BELLA
Huyu ni zaidi ya msanii kutokana na kuwa na kipaji kikubwa katika sanaa yake ya muziki, wanawake huvutiwa naye kwa sauti yake yenye mvuto wa hali ya juu na namna anavyojiweka akiwa jukwaani na pia ana uwezo mkubwa wa kucheza na mashabiki wake kiasi cha kuteka hisia za mashabiki wake.
Wanawake pia huvutiwa naye kiasi kwamba wengine humtaka zaidi ya muziki na jambo hilo alishakiri mwenyewe kwamba wapo mashabiki wake wanaomsaka kwa ajili ya kupata penzi lake.

04: YAMOTO BAND
Wasanii hawa kwa ujumla wao wamekuwa kivutio kikubwa kwa wanawake hasa wawapo jukwaani, wengi wao wameonekana kutamani kujumuika na kucheza nao jukwaani lakini wanaposhindwa wasanii hao hushuka jukwaani na kujichanganya nao hasa mashabiki wao wa kike.
Mara kadhaa wasanii wanaounda kundi hilo walishawahi kueleza kwamba wapo wanawake watu wazima huwafuatilia kwa kutaka kuwapongeza zaidi ya wanavyoimba jukwaani.

05: DIMPOZI KWA POZI
Anafahamika kama Ommy Dimpoz lakini jina lake kamili ni Omary Faraji Nyembo, wanawake huvutiwa zaidi na msanii huyu kutokana na nyimbo zake za kimapenzi ndiyo maana kila anapokuwa jukwaani humpigia kelele za kutosha.

06: MR BLUE
Msanii huyu ni wa muda mrefu asiyechuja, alipata umaarufu kwa jina la Mr Blue jina lake kamili ni Herry Sameer, ndiye msanii pekee wa hip hop anayewavutia zaidi wasichana kutokana na nyimbo zake kuwa na vionjo vya kimapenzi ambayo huwagusa zaidi wasichana.

07: BARNABA
Anaitwa Elias Barnaba, ni mmoja wa wasanii wasiobadili majina yao ya kisanii, uzuri wa sauti yake na uwezo wake wa kuimba jukwaaani na kutumia vyombo mbalimbali vya muziki ndiyo silaha yake kubwa kuwa kivutio kwa wanawake.
Mwenyewe hupenda kujiita kipenzi cha mabinti kutokana na kwamba wanawake wengi huziimba nyimbo zake mwanzo mwisho, pia ndiye msanii aliyeimba kwa ushirikiano mkubwa na wasanii wa kike ndani na nje ya nchi ambapo kwa sasa yupo mbioni kurekodi wimbo wa kushirikiana na msanii wa kike kutoka nchini Nigeria.

08: BOB JUNIOR
Ray C alifahamika kama kiuno bila mfupa na Raheem Rummy Nanji maarufu Bob Junior naye hivyo hivyo, wasichana wengi huvutiwa na kiuno chake anapocheza jukwaani, katika maonyesho yake mengi wasichana wameonekana kujaa kutokana na kuwa na mvuto naye kwa namna anavyovaa, anavyomiliki jukwaa na namna nyingine nyingi wanazovutiwa kwake.

09: JUX
Huyu ndiye mpenzi wa msanii maarufu, Vanessa Mdee, Juma Jux licha ya kuchipukia katika muziki wa Bongo Fleva lakini juhudi zake na uwezo wake wa kuchezea sauti yake, aina ya mavazi, namna anavyojiweka vimekuwa mvuto mkubwa kwa wasichana kiasi kwamba wengi wao hujikuta wakipiga kelele za kutosha katika maonyesho yake.

10: Ben Pol. 
Sophia ngoma ambayo inahit hadi sasa kutoka kwa msanii Ben Pol wadada kwa wakaka wakiusikia basi inakuwa shida mpya ndani ya miyo. Msanii huyu anaongoza kwa sauti ya pekee kwenye uimbaji wa Rn'B hapa Bongo.

Chama cha Wananchi CUF chamtaka Rais Magufuli aache kutumia madaraka vibaya

Chama cha Wananchi CUF chamtaka Rais Magufuli aache kutumia madaraka vibaya na kumwambia stahiki anazopewa Maalim Seif zipo kisheria.

Wamesema Kitendo cha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kushiriki mkutano wa CCM ni ushahidi tosha kuwa tume ya uchaguzi si chombo kilicho huru.

MAMA ADAI WATOTO WAKE WANAZUNGUMZA NA WATU WALIOKUFA...

Billington (kulia) akiwa na watoto wake. Kutoka kushoto ni Lucy, Jadon na Hellen, ambaye yeye hakujaliwa uwezo walionao wadogo zake.

Wazazi wengi hupenda kujisifu kuhusu vipaji vya watoto wao, lakini unaweza kufikiri Pam Billington angebaki na uwezo wa kipekee wa familia yake mwenyewe.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 38 anavutiwa watoto wake wawili wadogo Jadon mwenye miaka 10, na Lucy mwenye miaka minane, kuwa wanaweza kuongea na watu waliokufa.

Mama Billington, anayetokea Cheshire, anasema wamepata marafiki ambao ni mizimu zaidi ya kumi - akiwamo bibi yao - katika mwaka uliopita.

Anasema watoto hao wanaongea mno na marafiki zao wapya kiasi cha kuhisi kama ni sehemu ya familia yao hiyo.

"Hiyo ilianza miaka kadhaa iliyopita pale Jadon aliponieleza amekuwa akitembelewa na malaika wakati wa usiku," alisema Mama Billington.

"Mwanzoni nilipuuzia kama matokeo ya fikra zilizopitiliza. Lakini pale Lucy alipoanza kuongelea suala hilo pia nikaanza kusikiliza.

"Ni zawadi na pengine uipokee ama kuikataa. Sio mzaha, ninaamini kabisa watoto wangu wanaweza kuongea na mizimu."

Ziara za mizimu hiyo zilianza mwaka 2011 kwenye nyumba ya zamani ya familia hiyo mjini Manchester ambako, kwa mujibu wa watoto hao, mizimu hiyo iliishi kati yao na hata kwenye dari lao.

Machi mwaka huu, familia hiyo ikahamia kwenye nyumba yao mpya huko Sandback, mjini Cheshire, lakini watoto hao walidai mizimu hiyo ikawatafuta na kuwafuata.

Pam, mama wa nyumbani, anasema alikuja kuamini baada ya kushuhudia matukio mapya yeye mwenyewe.

Alisema: "Usiku mmoja nilikuwa nikitazama TV na nikamwambia Jadon kama kweli wapo hapa sasa amwambie mmoja wao avute mguu wa suruali yangu.

"Jadon akamwambia, kisha sekunde chache baadaye nikahisi kitu fulani kikigusa mguu wangu na nikaona kwa macho yangu mwenyewe suruali zangu zikisogea.

"Inashangaza. Sasa, wananigusa wakati wote. Wanaweza kunisukuma mkono na kunigusa kwenye mguu. Nimekuwa hata nikiguswa machoni na mzimu.

"Wanafanya pia televisheni kuwa timtimu pale Jadon anapoamuru mmoja kuthibitisha kwamba alikuwa mahali hapo.

"Unatakiwa kupitia haya kuweza kuelewa. Kila mara nimekuwa nikisoma vitu lakini sikuwahi kukubali kwa hakika hadi nilipovipitia nikiwa na watoto wangu."

Aliongeza: "Ninapenda kuwa na mizimu katika nyumba, nafikiri ni jambo muhimu.

"Nafikiri inaonesha kwamba kila kitu kinawezekana na inanipa matumaini wakati nitakapokufa. Ninafahamu kwamba huu sio mwisho na tunaendelea."

Kama mkanamungu, Mama Billington anasema hajawalea watoto wake kuamini mizimu na hana mashaka na uwezo wao wa kiakili kwa namna yoyote.

Lakini watoto hao, ambao wanasomea nyumbani, wanavutiwa.

Miongoni mwa wageni hao mizimu ni wawili wa Kimarekani wanaoitwa Sam na Simon Crease, ambao Jadon anaongea nao, sambamba na malaika anayeitwa Michael.

Lucy ameunda urafiki na msichana mdogo anayeitwa Rose.

Na, kwenye nyumba yake mpya huko Cheshire, anasema ameshawahi kumuona mzimu mwanamke kwenye bustani ya jirani, anayeaminika kuwa ni mzimu wa mwakamke mzee ambaye alifariki hivi karibuni mahali hapo.

Jadon alisema: "Nimekuwa na matatizo ya kulala sababu kila wakati nilihisi kama kuna mtu ananitazama.

"Nilikuwa naamka usiku na kukimbilia chumbani kwa mama na baba.

"Sasa ninapoona mizimu ninaongea nayo - na inanijibu. Ninaiona wakati wa mchana na usiku."

Aliongeza: "Mama na baba waliniuliza kama nilikuwa naiona kweli au la - hakika kuna mizimu ndani ya nyumba hiyo."

Ingawa Lucy bado anawasiliana na marafiki zake mizimu anakiri bado anatishika na vitendo vyao vya usiku wa manane.

Alisema: "Nimekuwa nikiogopa, Pale ninapowaona kwa mara ya kwanza nielewi kama ni mizimu au fikra zangu tu.

ANGALIA PICHA ZA NG’OMBE WA AJABU AZALIWA NEW ZEALAND,ANA MIGUU 8,MASIKIO 4,MIILI 2 NA KICHWA KIMOJA..


 

Ndama wa ajabu amezaliwa nchini New Zealand akiwa na miguu 8,masikio 4, miilimiwili,masikiomanne
 

Mmiliki wa ndama huyo, Neil Davy,ambaye amemshika ndama huyo aliyekufa kwenye picha aliuambia mtandao wa NZ wa nchini humo kuwa kama yeye asingekuwepo wakati ndama huyo akizaliwa basi ng’ombe aliyemzaa ndama huyo naye angekufa kwani alihangaika sana wakati akizaa.


‘Ilikuwa ni vigumu kumuangalia wakati alipokuwa anazaa,kwani hali yake ilikuwa mbaya sana alikuwa akipiga kelele kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata kutokana na ndama mwenyewe alivyo nilihangaika naye sana hadi nikalowa jasho jingi,’’alisema Davy.

Davy aliongeza kuwa alidhani ng’ombe huyo angezaa mapacha lakini kutokana na sababu ambazo hajazifahamu kikazaliwa kiumbe cha ajabu kama hicho.

 

Gallery

Popular Posts

About Us