Meneja wa wasanii wa bongo fleva maarufu kwa jina la Meneja Maneno, amefunguka na kusema wapo wasanii wengi Bongo wanaamini ushirikina na kukiri kuwa wapo wasanii wengine ambao yeye mwenyewe aliwapeleka kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kuroga.
.
.
Meneja Maneno aliyewahi kuwa meneja wa Diamond Platnumz, Rich Mavoko, Sam wa Ukweli na Nay wa Mitego, amefunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kuwataja wasanii ambao aliwahi kuwapeleka kwa waganga na ambao wanaamini sana ushirikina kuwa ni pamja na Rich Mavoko, Sam wa Ukweli huku akisema katika wote Diamond Platnumz ndiyo zaidi yao. "Ndele ni sehemu ambayo baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema 'Yes' ni 'Yes' tu kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa waganga kuroga ni pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko Kigamboni ndani ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi katikati yaani usiku ule unajifanya chizi kama umevurugwa" alisema Meneja Maneno.
.
.
Meneja Maneno aliendelea kutoa orodha ya wasanii hao ambao kwao shiriki ni kitu ambacho wanakiamini na kukiri kwenda nao huko na kufanya mambo hayo "Hata Sam wa Ukweli siwezi kukataa, ni watu ambao imani yao iliwapeleka huko lakini mimi nakumbuka kazi yangu niliyokuwa nafanya sikutaka kwenda kwa waganga.... ila sasa huyu Mondi sasa nimepata taabu naye, mara leo twende kwa mjomba, tunapeleka unga, leo tunapeleka mchele na mganga alivyo mshenzi hajawahi kuagiza samaki, yeye ni jogoo, mbuzi" alisisitiza Meneja Maneno .
.
TOA MAONI YAKO HAPA
0 comments:
POST A COMMENT