Mkutano wa Kamati kuu ya CHADEMA wavurugika baada ya polisi kuingilia kati. Lowasa, Mbowe, Mnyika washikiliwa. | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 29 August 2016

Mkutano wa Kamati kuu ya CHADEMA wavurugika baada ya polisi kuingilia kati. Lowasa, Mbowe, Mnyika washikiliwa.


Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilichokuwa kinafanyika katika Hoteli ya Giraffe iliyopo Mbezi jijini Dar, kimezingirwa na jeshi la polisi huku viongozi wake wakikamatwa na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.


Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema waliokamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano ni Edward Lowassa, Freeman Mbowe, John Mnyika, Dk Vincent Mashinji na  Said Issah

“Tulikuwa kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichojumuisha wajumbe na wabunge kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya chama. Jumla ya wajumbe walikuwa 170. Tukiwa kwenye kiako walikuja watu wanasema tunatakiwa polisi kwa sababu tumekiuka agizo la lilitokataza mikutano.”

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us