Ni kama vile Guardiola anatengeneza timu ambayo itakuwa tishio sana katika ligi kuu ya Uingereza kwa namna ambayo amekuwa akipangilia kikosi chake na namna ambavyo wachezaji wamekuwa wakitoa matokeo kwa klabu hiyo.
Timu imeongeza kujiamini kwa ujumla na pia baadhi ya wachezaji wamepanda kiwango huku majukumu kwa baadhi pia yakiwa yamebadilika na kuwa tofauti kiasi. Sergio Kun Aguero anaonekana kupunguziwa mzigo wa ufungaji na ndio maana sio ajabu kuona watu kama Raheem Sterling na Nolito wakiwa tayari wameona wavu zaidi ya mara mbili.
Uhuru uliopo kati ya Kevin De Bryune na Silva unawapa City sababu nyingine ya kucheza vyema wanapokuwa wanaelekea eneo la ushambuliaji huku pia Fernandinho akiweza kupatia vyema mfumo wa kucheza kama kiungo pekee wa chini na mkabaji huku akiwa jirani zaidi na John Stones.
Jumapili dhidi ya West Ham United, klabu ya Man City iliendeleza ushindi wake wa asilimia 100 kwa kushinda kwa jumla ya mabao 3-1. Mabao mawili ya Raheem Sterling (7, 90+2) pamoja na lile la Fernandinho yaliwabeba City huku Michail Antonio akifunga bao pekee a West Ham ambao hawajaanza vyema msimu kutokana na majeruhi wengi kikosini.
HIGHLIGHTS
0 comments:
POST A COMMENT