Chuchu Hans: Nikiwa na Ray Nahisi Kama Dunia Yote ni Yangu | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Monday, 29 August 2016

Chuchu Hans: Nikiwa na Ray Nahisi Kama Dunia Yote ni Yangu

Miss Tanga mwaka 2005, Chuchu Hans amesema kuwa ndani ya mahusiano ya kimapenzi na staa wa filamu, Ray Kigosi anajiona kama dunia yote ni yake.
Muigizaji huyo amesema anajisikia furaha sana jinsi anavyoishi kwa kusikilizana na mpenzi wake huyo.
“Nikiwa na Ray wangu, huwa nahisi kama dunia yote ni yangu, Ray ananidekeza sana,”Chuchu aliliambia gazeti la Mtanzania.“Ana mapenzi ya kweli, ananipenda mimi na watoto wangu wawili, amekuwa baba bora sana na hilo ndiyo linanifanya nijivunie na kuachana na maneno ya watu,”
Aliongeza, “Kufunga ndoa ni riziki na ninaamini haijafika siku yake, siku ikifika basi kila kitu kitakuwa wazi na hakuna atakayeweza kukwepa jambo hili, ila mapenzi na thamani tunayopeana ni ya mke na mume.”
Kwa sasa Chuchu na Ray Kigosi wamefunguka kampuni ya filamu iitwayo ‘Chura’.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us