Atletico Madrid walionekana tishio kwa Real Madrid na walionekana kama wanaenda kubadili matokeo ya mwanzo ya mchezo wao baada ya mabao mawili ya haraka haraka.
Alianza Saul Niguez dakika ya 12 kuzichungulia nyavu za Real Madrid kabla ya Antoine Griezman dakika ya 16 kuiandikia Atletico bao la pili kwa mkwaju wa penati.
Lakini wakati Atletico wakiamini wangemaliza kipindi cha kwanza wakiongoza kwa goli 2 kwa 0, dakika ya 42 Isco alifanikiwa kuipatia Real Madrid goli na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa bao 2 kwa 1.
Bao la Isco lilikuwa la kwanza kwake katika michezo yake 31 iliyopita katika Champions League, na bao hilo liliifanya Real Madrid kufunga mfululizo goli katika mechi 67 mfululizo.
Kipindi cha pili Atletico iliwapasa kufunga mabao mengine matatu ili kuitoa Real Madrid na Atletico waliingia wakijitahidi kutafuta mabao hayo lakini ikashindikana na mchezo kuisha 2 kwa 1.
Matokeo hayo yameifanya Real Madrid kufudhu kwenda katika fainali ya Champions League msimu huu na hii ikiwa ni mara mbili mfululizo katika misimu miwili.
Real Madrid sasa wanaifuata Juventus ambao usiku wa Jumanne waliitoa Monaco katika fainali itakayopigwa mwezi ujao tarehe 6 katika mji wa Cardiff nchini Wales.
0 comments:
POST A COMMENT