Mamlaka ya jeshi la Colombia inasema idadi ya waliofariki katika maporomoko ya ardhi nchini humo imefikia watu 250 huku waliojeruhiwa wakiwa 400.
Hata hivyo idadi hiyo huenda ikaongezeka kwani bado kuna zaidi ya watu 200 ambao hawajapatikana .
Vikosi vya wafanyikazi wanaoendesha shughuli za uokoaji wanasema nyingi ya barabara za kulipotekea maporomoko hayo huko eneo la mji wa kusini mwa taifa hilo, Mocoa hazipitiki kutokana na mkasa huo.
Maporomo hayo yametokea baada ya mvua kali kunyesha kwa saa nyingi.
Viongozi wa mataifa jirani wa Mexico na Argentina walikuwa wa kwanza kutoa ujumbe wa pole na kuahidi kwenda kuisaidia Colombia.
Rais Juan Manuel Santosa alitangaza hali ya tahadhari eneo hilo na kusafiri kuangalia shughuli za uokoaji.
Picha zilizochapishwa kwenye mitandao na jeshi zilionyesha baadhi ya majeruhi wakiokolewa kwa kutumia ndege.
Maporomo koya ardhi yamekumba eneo hilo mara kadha miezi ya hivi karibuni.
Mwezi Novemba, watu 9 waliuawa kwenye mji wa El Tambo, karibu kilomita 140 kutoka Mocoa kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyosababiswa na mvua kubwa.
0 comments:
POST A COMMENT