Chama cha Wamiliki wa Mabasi(TABOA) kwa kushirikiana na Wamiliki wa Malori na Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Dar es Salaam kimetangaza mgomo wa usafirishaji abiria na mizigo nchi nzima kuanzia siku ya jumatatu ili kushinikiza serikali kutopitisha sheria ya usafirishaji inayotarajiwa kusomwa mara ya tatu na kupitishwa siku ya Jumanne wiki ijayo.
Akitoa maazimio hayo yaliyofikiwa katika mkutao mkuu maalumu wa chama cha wamiliki wa Mabasi, Malori, Daladala na Baji, katibu mkuu wa TABOA Bwana. Eneo Mrutu amesema sheria inaloyolenga kupitishwa haikuwashirikisha wadau na haitenganishi makosa ya dereva na mmiliki, hali inayosababisha kosa lililofanywa na dereva linasababisha mmiliki kufungwa jela.
Aidha amewaomba wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao kutopisha sheria hiyo mpaka ifanyiwe marekebisho kwa kuwa inalenga kuharibu sekta ya usafirishaji nchini.
Chanzo: ITV
0 comments:
POST A COMMENT