Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Maputo nchini Msumbiji amepata nafasi ya kukutana na mtoto aliyepewa jina lake kama heshima kwake.
Rais Jakaya Kikwete kupitia akaunti yake ya Twitter aliandika “I have met in Maputo a boy named after me. His name is Kikwete.”
Mtoto huyo aliyekutana na Rais Jakaya Kikwete ambaye na yeye anaitwa ‘Kikwete.’
Katika jamii mtu anapokuwa amepewa jina kama la kwako mara nyingi humaanisha au huonyesha kukubalika kwako ndani ya jamii husika na kuyakubali yale yote ambayo umekuwa ukiyafanya. Hivyo kama kuonyesha heshima na kuendelea kukuenzi mtoto hupewa jina lako ili uendelee kuwa katika kumbukumbu miongoni mwao.
Rais Kikwete yupo mjini Maputo nchini Msumbiji ambapo ni mmoja wa wajumbe wanaoshughulikia masuala ya amani.
Tangu alipotoka madarakani Novemba 5, 2015 Rais Jakaya Kikwete amekua akijishughulisha na masuala ya kurejesha amani Afrika hasa nchini Libya, masuala ya Elimu na kupiga vita ugonjwa wa Malaria barani Afrika.
0 comments:
POST A COMMENT