Bodi ya mikopo ya vyuo vikuu imetangaza kuanza kupokea tena maombi ya mikopo kwa wanafunzi waliokosa mna wale wanaokata rufaa, akizungumzana waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya mikopo ya vyuo vikuu ABDULRAZAQ BADRU, amesema bodi hiyo itaanza awamu nyingine ya kupokea maombi ya mikopo kwa ili wote walio na vigezo vya kupata mkopo wapate na waweze kusoma vizuri.
Abdul-Razaq Badru, mkurugenzi wa HESLB akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO jijini Dar es Salaam amewambia waandishi wa habari kuwa bodi hiyo lazima ipitie upya majina ya wanafunzi waliopewa mikopo hata kama wapo katika mwaka wao wa mwisho wa masomo.
Pia akaongeza kwa kusema Wote walioomba na kupitishwa na bodi kupta mkopo tayari wamekwisha pewa mikopo yao na fedha hizo tayari zmekwisha wekwa kwenye akaunti za vyuo husika,
Sambamba na hilo amesisitiza wale wote wanaonufaika na mikopo hasa wale wanaoendelea na masomo wanatakiwa kujaza dodoso au form ya uhakiki wa mnufaika, na Zoezi hilo la uhakiki wa wanufaika litaanza mwanzoni mwa mwezi novemba mwaka huu na litachukua muda wa siku 30
Wanufaika wote wanatakiwa kuingia kwenye akaunti binafsi za HESLB ili kuweza kujaza na kuweka taarifa sahihi
"HESLB tutahakiki upya wanufaikaji wa mikopo waliopo mwaka wa pili, tatu na hata wale wa mwaka wa nne ili kuondoa kila asiye na sifa na kwa wale wa mwaka wa kwanza waliokosa mikopo na wanadhani wanazo sifa wakate rufaa kuanzia Novemba Mosi,” amesema Badru."
0 comments:
POST A COMMENT