Fedha za mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini zimeanza kuingia katika akaunti zao, baada ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) kusema kuanzia Jumatano hii imeanza kuingiza fedha za wanafunzi wote waliokidhi vigezo vya kupatiwa mkopo.
Akizungumza na gazeti la Habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul Razaq Badru aliwahakikishia wanafunzi hao kuwa fedha hizo zinaanza kuingia siku tofauti tofauti.
“Napenda kuwahakikishia waombaji kuwa boom limeanza kuingia leo, kwa kuwa fedha hizo zinapitia benki baadhi wanapata kesho na wengine siku zinazofuata, ila sisi tumeshatimiza wajibu wetu,” alisema Badru.
“Kuna wanafunzi kama 90 wamekosa mikopo kwa sababu ya umri wao kuwa mkubwa, sisi tunatoa mikopo kwa wanafunzi wanaotoka sekondari. Pia kuna wanafunzi wengine kama 6,561 hawakuomba kabisa mikopo licha ya kudahiliwa na TCU hao nao tunasema hawana sifa ya kukopeshwa,” aliongeza Badru.
Katika ufafanuzi wa waliopata mikopo, Badru alisema kati ya wanafunzi hao yatima waliopata mkopo ni 873, wenye ulemavu wa viungo wako 118, wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448, waliofadhiliwa na taasisi mbali mbali 87, wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159 na Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine ni 9,867.
credt MUUNGWANA BLOG
Kwa upande mwingine SERIKALI YATOA SABABU ZA KUTOA MIKOPO KWA VIGEZO
Wizara ya elimu imefafanua kuwa wametoa mikopo kulingana na vigezo vya wanafunzi na pia sio wote wenye vigezo watapata kwa kuwa bajeti ina ukomo.
Naibu waziri amesema wanafunzi wengi walikuwa wanapata mikopo pasipo na vigezo na walikuwa wakitumia mikopo kufanyia mambo mengine kama kunywa pombe kununulia tv na kutembea ambavyo sio kusudio la mikopo hiyo.
-
0 comments:
POST A COMMENT