Hatimaye hekaya za filamu za miaka ya 1980 zawa kweli kwani ndani ya muda mfupi polisi roboti ataanza kutumiwa katika vituo vya usalama.
Katika tamasha la maonyesho ya roboti kwa jina la GITEX jijini Dubai ,mojawapo ya vitu vilivyowavutia watazamaji ni polisi roboti aliye na uwezo wa kufanya utambulisho wa uso wa mtu.
Roboti huyo polisi pia anaweza kutoa adhabu kwa wanaokiuka sheria za barabarani.
Roboti huyo anatarajiwa kupewa kazi ya kushika doria maeneo ambayo kuna wingi wa watalii jijini humo mwaka ujao.
0 comments:
POST A COMMENT