Baada ya Kukataa Wito wa Polisi,Mbowe Aamua Kumpeleka Makonda Mahakamani,..!! | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Saturday, 11 February 2017

Baada ya Kukataa Wito wa Polisi,Mbowe Aamua Kumpeleka Makonda Mahakamani,..!!


Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Aikael Mbowe (MB) leo tarehe 10 February 2017 amefungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salam, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu DSM na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dsm.

Kesi hiyo ilisajiliwa kama Kesi ya Kikatiba namba 1 ya 2017 imefunguliwa kwenye Mahakama ya Kuu masijala ya Katiba (Masijala Mkuu).

Kwenye Kesi hiyo Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke na kuwa Mkuu wa Mkoa hana mmalaka ya kudharilisha, na kukamata.

Mbowe pia ameiomba mahakama itengue vifungu vya 5&7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwakua ni batili na vinakiuka haki za kikatiba.

Katika kesi hizo Mbowe atawakilishwa na Mawakili toka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya CHADEMA.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us