Muziki ni hisia na kila mmoja anaamua kufanya kile anchojisikia bila kujali wengine watatafsri vipi, Hiyo ni sawa na alichokifanya Bongoflava icon Diamond Platnumz kwenye hitsong Salome ambayo amemshirikisa mtu mbaya Rayvanny.Ndani ya siku mbili tayari Salome imekua ni ngoma kubwa ambayo inaongelewa kila kona kwa uzuri na ubaya.Kundi la muziki “Sautisol” la nchini Kenya limetumia ukurasa wake wa Instagram kuyaelezea mahaba yao kwenye
ngoma hiyo baada ya kutundika picha ambayo ni moja kati ya Scenes zilizoonekana kwenye Video “Salome” ikiwa na maelezo yaliyosomeka ”
Ni Bora Dunia ingejua kiswahili, maana hii ngoma ni matatizo… #salome @diamondplatnumz x @rayvanny #TraditionalVersion.
Huenda salome ikawa moja kati ya ngoma za kiswahili zenye ushawishi mkubwa siku za mbele na tusishangae kuona au kusikia imefanywa covers nyingi kulio ngoma yeyote ya Bongoflava.
”
0 comments:
POST A COMMENT