Dogo Janja ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Kidebe’ amefunguka na kutangaza rasmi kuwa ana mpango wa kutaka kuoa na kusema kwamba muda si mrefu anaweza kuvuta jiko na kuweka ndani.
Dogo Janja alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho kilikuwa kinarushwa moja kwa moja kutokea Manzese na kusema kuwa suala hilo lipo kwenye mchakato ila ni kweli ana mpango wa kuoa muda si mrefu.
‘Yah ni kweli nataka kuoa muda si mrefu nitavuta jiko hivyo siwezi kusema ni lini ila suala hilo lipo kwenye mchakato” alisema Dogo Janja.
Kwa upande wa Madee ambaye ni mlezi wa Dogo Janja kimuziki na katika maisha ya kila siku alisema kuwa kitendo cha Dogo Janja kutaka kuoa kabla yake itakuwa kama dharau hivyo anapaswa kusikilizia kwanza mpaka yeye afanye mambo kwanza ndipo na yeye atangaze.
0 comments:
POST A COMMENT