WCB Wasafi ni moja kati ya lebo kubwa za muziki na zinazofanya poa sana Afrika kwasasa. Kutokana na kazi nzuri zinazotoka chini ya lebo hiyo pamoja na nguvu ya kusapoti kazi zao zinazofanywa na wadau pamoja na wapenzi wa muziki katika kuhakikisha muziki wao unafika mbali zaidi.
Yamekuwa ni metamanio ya wasanii wengi kutaka kuwa chini ya lebo hiyo kama ambavyo tumemsikiaDiamond Platnumz mara kadhaa akizungumza kuhusiana na hilo. Lakini round hii ameichana Perfect255kuwa amefungua milango kwa msanii yeyote mwenye uwezo na malengo ya kufika mbali kupitia kazi yake ya muziki kujiunga na lebo hiyo.
Lakini haiwezi kuwa rahisi kama unavyofikiria, kwasababu ingekuwa rahisi kihivyo huenda WCB ingevunja rekodi ya dunia kuwa lebo ambayo imewasainisha wasanii wengi kuliko lebo zote duniani. Sasa katika kupingana na hilo mtu mzima Diamond Platnumz amefunguka kwenye kipaza cha Perfect255 vigezo na masharti ambayo msanii lazima awe ametimiza ili aweze kusainiwa na lebo hiyo.
“WCB milango iko wazi, lakini hatuchukui mtu yeyote tu, tunachukua msanii ambae amehaso, kwasababu kuna wasanii wengi sana ambao wameshakuja WCB tena wenye majina makubwa na hata ambao hawajawa na majina bado, wa ndani na nje ya Tanzania, Afrika na nje ya Afrika. Naweza kukuibia siri kuna msanii mmoja kutoka Nigeria ambaye siwezi kukutajia jina lake na ngoma yake inafanya poa sana sasa hivi na ipo namba moja kwenye chati tofautitofauti za muziki Afrika lakini yeye mwenyewe mpaka kesho yani tamanio lake ni kujiunga na WCB lakini tumekataa kusaini nae kwasababu sasa hivi tunataka tuimarishe kwanza wasanii wa nyumbani kisha baadae ndio tutaenda huko.”
0 comments:
POST A COMMENT