Abiria wa ndege wazuiwa kubeba simu za Samsung Galaxy Note 7 wakati wa safari nchini Canada
Idara ya usafiri nchini Canada imetangaza kupiga marufuku ubebaji wa simu za Samsung Galaxy Note 7 kwa abiria wakati wa safari.
Idara hiyo ilitoa maelezo na kutangaza kuchukuwa hatua hiyo kutokana na kesi za ulipukaji wa betri za Galaxy Note 7 zilizoripotiwa kwa kampuni ya Samsung hivi karibuni.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba simu hizo pia hazitoruhusiwa kubebwa ndani ya mizigo yoyote inayopakiwa ndani ya ndege.
Mkuu wa idara ya usafiri aliwatahadharisha abiria wote na kusema kwamba wataweza kutozwa faini ya fedha endapo watakiuka kanuni hiyo.
Mkuu huyo aliongezea kusema kuwa hatua hiyo itasaidia kudhibiti hali ya usalama wa abiria wakati wa safari za ndege ingawaje wamiliki wa simu hizo watakuwa na hali ngumu.
0 comments:
POST A COMMENT