Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah J. Kairuki amekanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa serikali ina mpango ya kuhakiki namna watumishi wake wanavyotumia mishahara yao.
Waziri Kairuki kupitia akaunti yake ya matandao wa Twitter amesema kuwa taarifa hiyo ni ya uongo na kuwataka wananchi kuipuuza kwani ina lengo la kupotosha umma.
“Kuna taarifa ya uongo inayosambazwa mtandaoni kwamba “kutakuwa na zoezi la kuhakiki watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao”.Ipuuzieni.”
“Si dhamira wala desturi ya Serikali yetu kuingilia maisha binafsi ya watumishi wa umma hususan matumizi ya mishahara yao.Puuzieni uzushi huo.”
Taarifa hiyo imemnukuu Waziri Kairuki kuwa serikali baada ya kukamilisha uhakiki wa vyeti kwa watumishi wake, wataanza uhakiki wa jinsi watumishi wa umma wanavyotumia mishahara yao ili kurejesha maadili kwa watumishi wa umma.
Kuhusu uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa serikali, Rais Magufulii alisema kuwa lengo la zoezi hilo si kuwafukuza watumishi lakini ni kujiridhidha kama malipo yanayofanyika kwa watumishi hao yanalandana na viwango vya elimu wanavyoeleza kuwa wanavyo.
0 comments:
POST A COMMENT