LIFAHAMU KIUNDANI KUNDI LA KIGAIDI LA DOLA YA KIISLAMU LENYE MSIMAMO MKALI LA ISLAMIC STATE, (ISIL/ISIS/IS) | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday, 4 November 2016

LIFAHAMU KIUNDANI KUNDI LA KIGAIDI LA DOLA YA KIISLAMU LENYE MSIMAMO MKALI LA ISLAMIC STATE, (ISIL/ISIS/IS)


Image result for islamic state photos
LIFAHAMU KUNDI HATARI NA LENYE MISIMAMO MIKALI LA DOLA YA KIISLAMU (ISLAMIC STATE), ISIL/ISIS/IS.
Nami Josephat Keraryo Nyambeya.
Kikundi cha Dola ya Kiislamu maarufu kwa jina la Islamic State of Iraq and Levant (ISIL), Islamic State of Iraq and Syria (ISIS), Islamic State (IS) pia hujulikana kwa jina la Daesh ni kikundi cha Jihadi ya Salafi kinachofuata msingi wa Wahhabi katika madhehebu ya Kiislamu ya SUNI.
Kundi hili linalojipiga kifua kuwa linafuata misingi ya dini ya Kiislamu limekuwa likilaumiwa kwa matendo yake maovu kutoka makundi mbalimbali, serikali na hata makundi ya mengine ya dini ya Kiislamu kuwa hayafuati misingi halisi ya dini hiyo.
Kundi hili limetajwa kuwa la Kigaidi na Umoja wa Mataifa na hata nchi nyingi duniani pia zimelitaja IS kama kundi la kigaidi. ISIL inajulikana kwa video zake za kukata watu vichwa, wanajeshi kwa raia pia waandishi wa habari na wafanyakazi wa mashirik ya kutoa misaada wamekuwa wahanga wakubwa wa Ukatwaji vichwa unaotekelezwa na kundi hili.
Umoja wa mataifa umelitaja kundi hili kwa kuhusika na uvunjifu wa haki za binadamu pia shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelitaja kundi hili kwa kuhusika kwake na kufutilia mbali kwa jumuia za watu huko Iarq ya Kaskazini.
KUNDI HILI LILIANZAJE?
ISIL ilianza lilianzishwa mnamo mwaka 1999 na raia wa Jordan aitwae Abu Musab al-Zarqawi chini ya jina la Jama'at al-tawid wal-Jihad .(Kikundi cha Jihadi).
Mnamo mwezi Octoba mwaka 2004 Al-Zarqawi aliungana na Osama Bin Laden kiongozi wa Al-Qaeda na kuanza ushirikiano. Osama alilibadilisha jina kundi hili na kuliita Kundi la la Jihad ngome ya Mesopo (Kwa kiarabu ni ngumu sana kuandika Laptop hainiruhusu kufanya hivyo), au maarufu kwa jina la Al-Qaeda in Iraq (AQI).
Chini ya Al-Zarqawi kundi hli lilihusika sana na mashambulizi ya kujitoa mhanga na hata mauwaji ya kutisha baada ya uvamizi wa majeshi ya Marekani nchini Iraq mnamo March, 2003. kwa anaekumbuka kipindi cha kuanzia mwaka 2003-2007 ilikuwa haipiti siku hata moja bila kusikia watu kadhaa wameuawa Iraq kwa mashambulizi ya kujitoa mhanga. Mashambulizi haya yote yalikuwa yanafanywa na Kikundi hiki cha Al-Qaeda in Iraq (AQI) ambacho leo tunakizungumzia kwa jina lingine kabisa la Dola la Kiislamu (IS).
Mnamo January 2006 kundi hili liiungana na makundi mengine ya Kisuni na kunda Halmashauri ya Shura ya Mujahideen. Baada ya kuuawa kwa Al-Zarqawi mwezi Juni mwaka 2006 kwa mashambulizi ya ndege za Marekani kundi hili la Halmashauri ya Shura ya Mujahideen liliungana tena na vikundi mbalimbali na kuunda tena kikundi kikubwa walichokiita jina la Islamic State of Iraq (ISI) , hiyo ilikuwa mwezi October mwaka 2006.
Kundi hili la ISI liliongozwa na watu wawili Abu Omar al-Baghdad na Abu Ayyub al-Masri hadi walipouliwa kwa mashambulizi ya Jeshi la Marekani mnamo mwezi April, 2010. baada ya wawili hawa kuuawa Abu bakr al-Baghdad alichukua hatamu za uongozi za kundi hili.
Mnamo mwezi August mwaka 2011 baada ya kulipuka kwa mapigano nchini Syria , ISI chini ya al-Baghdad lilitangaza misheni ya kuingia vitani nchini Syria kwa jina la Jabhat an-Nusrah li-Ahli ash-Sham misheni iliyojulikana kwa jina maarufu la AL-NUSRA FRONT (Kama ni mfuatiliaji wa mambo haya nadhani jina hili la AL -NUSRA FRONT siyo geni kwako.
Misheni ya Al-Nusra Front ilifanikiwa sana kupenya katika maeneno mengi yenye waislamu wa madhehebu ya SUNI huko Syria, hapa namaanisha majimbo ya Raqqah, Idlib, Deir ez-Zor na Aleppo. (Nadhani sasa unaanza kupata picha ya kile kinachogombaniwa huko Mashariki ya kati).
Mwezi April , 2013 al-Baghdad alitangaza muungano wa misheni ya Al-Nusra Front na ISI na kuunda kundi la "ISLAMIC STATE OF IRAQ AND LEVANT (ISIL)". Neno levant lisiwatishe kuna siku nitawaambia maana yake. Pamoja na tangazo hilo la Al-Baghdad Abu-Mohammed al-Julani kiongozi wa misheni ya AL-NUSRA FRONT pamoja na Ayman al-Zawahiri kiongozi wa Al-Qaeda walikataa kuutambua muungano huo .
Baada ya miezi minane ya kupigania madaraka na , mnamo kundi la Al-Qaeda lilikata mahusiano na ushirikiano wote na kundi la ISIL kwa sababu za kwamba , Moja- kundi la ISIL lilikuwa likiendesah mashambulizi na misheni zake bila kulihusisha kundi mama la Al-Qaeda, pili kundi hili la ISIL lilikuwa linakiuka misingi halisi ya dini ya Kiislamu kwa vitendo vyake vya Kikatili kama Kukata watu vichwa, kuchina shingo kwa kutokea nyuma n.k.
Lengo kuu la kundi hili la ISIL limekuwa ni kuwaondoa Waislamu wote madhebu ya Kisuni kutoka kwenye manyanyaso ya serikali za Kishiriti (serikali za kishia). Shia ni madhehebu katika dini ya Kiislamu pia.
Image result for islamic state photos
Wapiganaji wengi wa kundi hili haswa wa Upande wa Iraq wamekuwa ni wale wanajeshi waliokuwa wkatika serikali ya Sadam Hussein (ifahamike kuwa Sadam Hussein alikuwa ni Msuni), watoto wa wanajeshi hao pia wamekuwa ni wapiganaji ndani ya kundi hili la ISIL. Wanajeshi hawa wastaafu wa Iraq wamekuwa ndio makamanda wakuu wa kuangalia na kufuatilia shuguli mbalimbali za Kundi hili. Kwa hiyo usishangae kuona misheni nyingi za kundi hili zikifanikiwa, ni kwa sababu wanao watu waliobebea kwenye medani za Upelelezi (spying) na Kijeshi. Wako vizuri kwenye medani ya Vita.
Image result for islamic state photos
IMANI YA KUNDI HILI NI IPI?
Kama nilivyotangulia kusema ISIL linaamin katika misingi ya Kisalafi ndani ya SUNI. (Nikisema Salafi wale waislamu ambao hawakukimbia madrasa wananielewa vizuri). Linafuata misingi mikali ya dini ya kiislamu , na huwachukulia wale waislamu wale wasioafikiana na misingi hiyo kama MAKAFIRI (kwa kingereza makafiri tunawaita Infidels , hahahaha sijui wewe ni nani ewe msomaji, kama hukubaliani na misingi mikali ya ISIL utakuwa Infidel).
Philosophia ya kundi la ISIL inawakilishwa na bendera yao nyeusi , bebdera hii huuita bendera ya Vita ya Mtume Muhammad (S.AW) , bendera hii ina seal ya mtume Muhammad ndani ya duara jeusi na pia kwa juu yake kuna maneno yaliyoandikwa kwa kiarabu yakiwa na maana ya kuwa "HAKUNA MUNGU ILA kuna ALLAH" kwa lugha ya Kimombo yakimaanisha kuwa "There is no God but Allah". Nembo hiyo imekuwa ikiwasikilisha imani ya ISIL kuhusu Uislamu na kuanzishwa kwa Kaliphi ikiwa na malengo makuu ya kuifanya dunia nzima ifuate msingi huo .
Wachambuzi wengine wa masuala ya dini ya Kiislamu na wasomi na wanazuoni wamekuwa wakisema kundi hili la Dola ya Kiislamu limekuwa imani kama ya Muslim brotherhood ya kale, Mslim brotherhood lilipata umaarufu sana mnamo miaka ya 1920 huko nchini Misri kwa misimamo yake mikali juu ya dini ya Kiislamu.
Kundi hili la IS lina makao makuu yake mjini Raqqah nchini Syria, kila maeneo linayoyatawala limeanzisha sharia za dini ya Kiislamu na huko linafuata misingi hiyo hata kwenye mashule watoto wanafundishwa kwa mujibu wa msimamo wa IS.
IS imekuwa ikiamini kuwa dunia inapaswa kurudi kwenye misingi ya kale ya dini ya Kiislamu na hawataki kabisa kusikia mapinduzi au mabadiliko yoyote yakifanywa kwenye dini hiyo.
Kwenye mamlaka za IS watu hutozwa kodi kulingana na dhehebu lake, wale wa madhehebu yaliyo tofauti na SUNI hutozwa kodi ya juu kabisa ukishindwa huambiwa ubadili dhehebu na kuungana nao au kuuliwa kama utaendelea na msimamo wako wa kutobadili dini na kutolipa kodi waitakayo.
IS na waumini wake wamekuwa wakiwalaumu watawala wa sasa kwenye nchi za Kiislamu na haswa Utawala wa zamani wa OTTOMAN kwa kufanya mageuzi kwenye mambo mengi ya dini hiyo na hivyo kuita Uislamu wa Kisasa siyo ule unaotakiwa kuenziwa na waislamu safi.. Pia IS inaamini kuwa utawala halali wenye kufuata misingi ya Uislamu wa kale ndio pekee wenye uhalali wa kuendesha vita ya Jihad , na wamekuwa wakiamini kuwa Jukumu la kwanzawalilo nalo kabla ya Kuziteka na kuzigeuza nchi zisizo za Kiislamu na kuzifanya kuwa za Kiislamu kwanza ni kuwachuja na kuwageuza jumuiya yote ya Kiislamu kufuata misingi waitakayo wao.
Kwa mfano ISIL inaamini kuwa kikundi cha Kisuni cha Palestina cha HAMAS ni kikundi cha KIKAFIRI hivyo hakina uhalali wa kupigana Jihad na wanaona kuwa Kupigana dhidi ya HAMAS na kuwaondoa kwenye mipaka ya Palestina itakuwa Jukumu lao la kwazna kabla ya kuingia kwenye makabiliano dhidi ya Israel na kuikomboa ardhi hiyo wanayodai inakaliwa na Israel kwa mabavu. Msomaji naomba ufahamu kuwa Israel imekuwa ikipigana na kikundi hiki cha Kiislamu cha HAMAS kwa miaka kadhaa sasa , madai ya HAMASI yakiwa yanaitaka Israel iachie ardhi inayoikalia kwa mabavu kutoka kwa Palestina. Na pia ISIL wanaamini kuwa siku moja watakuja kuiondoa Israel katika ardhi hiyo ila jukumu lao la kwanza na kuwasafisha HAMAS maana kwao hawa ni MAKAFIRI (Vey interesting kwa kweli, nadhani unapata picha ya kile nikimaanishacho).
Utofauti walionao ISIL na makundi mengine ya Kijihad ikiwemo Al-Aeda ni kuhusu Hukumu ya siku ya mwisho yaani siku ya Kiama. Na pia ISIL wanaamini kuwa kurudi kwa Imam MAHDI kuko karibu. (Waislamu wambao hawakukimbia Madrasa hapa wanaelewa vizuri). ISIL inaamini kuwa ipo siku na siku hiyo haipo mbali kuwa watayashinda majeshi ya Roma (majeshi ya Kikristo) katika mji wa DABIQ na kukamilisha Unabii. Hapa huwa wanafuata hadithi fulani ndani ya dini yao. (Hadith of the Twelve successors ) . Pia ISIL inaamini kuwa baada ya kiongozi wao huyu Al-Baghdad watafuata wengine wanne (makaliphi) kabla ya kuyashinda majeshi ya Roma mjini Dabiq.
Nikakuomba ufuatilie mji wa Dabiq utapata kuyajua mengi kuhusu mji huu na imani yake katika dini ya Kiislamu). Kwa kukunyofolea tu kidogo ni kuwa gazeti inalotoa habari za kila siku mtandaoni kuhusu kundi hili la IS wanaliita DABIQ nami ni mfuatiliaji mzuri wa gazeti hili. Siwezi kuyaandika mengi kuhusu Dabiq maana siyo lengo la post hii.
NI MAENEO GANI WANAKOTAWALA HAWA DOLA YA KIISLAMU?
Kundi hili la Dola ya Kiislamu liekua likijigamba kuwa dunia nzima ni miliki yake na hayo yamekuwa malengo yake makuu . Ila kwa sasa kundi hili limefanikiwa kujipenyeza na kuunda matawi yake nchini Libya, Misri (kwenye peninsula ya Sinai), Saudi Arabia, Yemen, Algeria, Afghanistan, Pakistani, Nigeria. Na nje ya Iraq na Syria pia lina wanachama nchini Morocco, Lebanon , Jordan , Uturuki, Israel lakini halina matawi maeneo hayo.
Kundi hili linakadiriwa kuwa na wapiganaji 100,000 kwa pande zote za Iraq na Syria, huku upande wa Iraq ukiwa na wapiganaji 40,000 pekee huku 60,000 wakiwa upande wa Syria. Asilimia 30 ya maofisa wakubwa ndani ya kundi hili walikuwa maafisa wa Kiusalama ndani ya Jeshi la Iraq chini ya serikali ya Saddam Hussein.
Vyombo vya kimataifa vimekuwa vikiripoti kuwa kufikia mwezi May mwaka 2015, wapiganaji zaidi ya 25,000 kutoka nchi 100 duniani wamefanikiwa kusafiri na kujiunga na kundi hili . Unaweza ukana ni kwa jinsi gani kundi hili linaungwa mkono na watu mbalimbali kutoka mataifa mengi duniani. Sijui wewe unaliunga mkono? Baki na Jibu lako kimya kimya.
Kundi la ISIL limepata uungwaji mkono mkubwa wa makundi mbalimbali ya Jihad duniani, yakiwemo lile la Boko Haram la Nigeria, Ansar al-Sharia la Tunisia, Jund al_Khilafah, Mujahideen Shura Council in the Environs of Jerusalem, Jamaah Ansharut of Uzbekstan, Jundaallah (Pakistan), Sheikh Omar Hadid Brigade, Khalifa Islamiyah Mindanao (Ufilipino) na makundi mengine mengi .
VYANZO VYA MAPATO VYA MAPATO VYA KUNDI LA DOLA LA KIISLAMU.
Kumekuwa na maswali mbalimbali ya juu wanakopata Pesa, silaha na hata vitu vingine va kuwawezesha kuhudumu katika vita kundi hili la IS , wanazuoni mbalimbali wamekuwa wakihoji ni vipi IS inaweza kuwa imara kiasi hiki bila ya kuwa na ufadhili kutoka nchi zingine?
Serikali ya Iraq imekuwa ikiituhumu Saudi Arabia kwa kuifadhili IS, japo Saudia imekuwa ikiyana madai haya kila kuchapo. Vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo Al-jazeera, BBC, The new York times, na the US-based think tank vimeripoti kuhusu misaada itolewayo na Saudi Arabia juu ya kundi hili. Kama unafuatilia mambo ya Mashariki ya kati utakubaliana na mimi kuwa kwa sasa kumekuwa na uhusiano mbaya sana kati ya nchi ya Iran ambae ndie mfadhili mkubwa wa kijeshi na kifedha wa makundi na nchi zinazopigana dhidi ya IS na nchi ya Saudi Arabia. Nchi hizi mbili zimekuwa zikituhumiwa kuyafadhili makundi mbalimbali ya kiislamu kulingana na madhehebu yake, Iran ikiwa inatuhumiwa kuwafadhili wale wa mirengo ya Kishia ikiwemo Hezibollah ya Lebanon na Houthi (Yemen) ambalo lnapigana dhidi ya Saudia, huku Saudia ikituhumiwa kuwafadhili wale wenye mirengo ya Kisuni. Ifahamike kuwa Saudi Arabia ni ngome ya madhehebu ya SUNI na iran ni ngome ya madhehebu ya SHIA.
Richard Dearlove mkuu wa Shirika la Ujasusi la Uingereza nae pia anadai kuwa Saudi Arabia imekuwa ikuhusika na kuwafadhili IS ili kuondoa utawala wa Kishia katika mashariki ya Kati. Mwaka 2014 mgombea Urais wa Marekani mama Hilary Clinton alidai kuwa Qatar na Saudi Arabia zimekuwa zikihusika kuifadhili IS.
Pia nchi ya Uturuki inadaiwa kuwa mfadhili mkuu wa kundi hili. madai hayo pia yamepatwa kutolewa na makamu wa rais wa marekani Joe Biddeni,
Kundi la IS limekuwa likipata pesa kutoka kwenye mauzo ya mafuta wanayofanya, IS imefanikiwa kuteka maeneo mengi yenye visima vya mafuta hivyo IS imekuwa ikifanya biashara haramu ya mauzo ya mafuta ambayo inakadiriwa kuwaingizia jumla ya Dolla Mil 100 kwa wiki, sawa na Shillingi Bil 220 za Kitanzania, hii ina maana ya kwamba IS wanaingiza Jumla ya shillingi Bil 30 za Kitanzania kwa siku kutokana na biashara hiyo.
Pia kundi la IS limekuwa likipata fedha kutokana na kutoza kodi kwenye maeneno linayoyakalia, pia vyanzo vingine vya mapato vimekuwa ni vile vya Kuwakomboa mateka waliotekwa na kundi hilo. Biashara hii ya kuwakomboa mateka inawaingizia Jumla ya Dolla Mil 20 kwa mwaka.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us