Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako.
Dar es Salaam.Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imeendelea kuufumua mfumo wa elimu uliopigiwa kelele na wadau wakati wa Serikali iliyopita kwamba unashusha ubora wa elimu baada ya Alhamisi iliyopita kutoa waraka mpya unaobatilisha programu za mafunzo ya ualimu.
Mabadiliko mengine ya elimu yaliyofanyika katika Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwaondoa wanafunzi wa cheti na stashahada maalumu ya ualimu wa sayansi Chuo Kikuu cha Dodoma, kufuta GPA na kurejesha Divisheni na kufuta mtihani wa pili (paper two) kwa watahiniwa binafsi.
Katika mkakati wa hivi karibuni, Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetoa Waraka wa Elimu Namba 5 wa mwaka 2016, unaolipokonya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) mamlaka ya usimamizi wa vyuo vya elimu ngazi ya cheti na stashahada na kuyarejesha wizarani chini ya uangalizi wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta).
Hivyo, Necta ndiyo itatahini na kutoa tuzo ya mafunzo ya ualimu wa cheti na stashahada kuanzia mwaka 2016/17.
Source: Mwananchi
0 comments:
POST A COMMENT