Rais Robert Mugabe kugombea tena Katika Uchaguzi Mkuu wa 2018 | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Sunday, 18 December 2016

Rais Robert Mugabe kugombea tena Katika Uchaguzi Mkuu wa 2018


ZIMBABWE: Chama tawala ZANU-PF kimemtangaza Rais Robert Mugabe(92) kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2018

Mugabe mwenye umri wa miaka 92 sasa amekuwa kiongozi wa taifa hilo tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1980 kutoka kwa Wakoloni Waingereza.

Mbali na ZANU-PF kumemtangaza Rais Robert Mugabe kuwania tena kiti hicho, kuna baadhi ya makundi yameibuka huku yakipinga mkongwe huyo kuendelea kuliongoza taifa hilo kwa madai kuwa ameshusha uchumi wa nchi.

Mugabe anasifika kwa kuwa rais mwenye misimamo thabiti licha ya kuwa mzee, lakini akisimamia jambo na kuamua lifanyike lazima lifanyike na hata kama akikataa jambo anamaanisha amekataa haswa. Hateteleki, hamuogopi mtu wala taifa lolote.

google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us