Walimu wa shule ya Msingi Nyakabungo jijini Mwanza wameiomba serikali kuingilia kati swala la ufanyaji wa tohara katika maeneo ya viwanja vya shule jambo ambalo limeonyesha kuwa kero .
Akizungumzia tukio hilo Mwl. Patrick Kamugisha amesema ameshangazwa sana kuona tohara ikifanyika hadharani na si kama mikoa mingine ambayo hufanya matukio hayo katika maeneo yaliyojificha na kwa usiri mkubwa.
Pia wanafunzi wa shule hiyo wamelalamikia matukio hayo hasa nyakati za asubuhi wanafunzi hao wanapokuja kujisomea masomo ya ziada kwa kipindi hiki cha likizo wanakutana na uchafu hasa mabaki yanayotokana na tendo hilo pamoja na kutapakaa kwa damu jambo ambalo wamesema ni hatari kwa afya zao.
Kutokana na tukio hilo la maandamano ya vijana hao wa kabila la wakurya hivyo barabara ya Isamilo hulazimika kufungwa kwa muda ili kupisha maandamano hayo yapite,tofauti na Wilayani Tarime na Rorya ambako tohara hufanyika katika maeneo rasmi.
Kutokana na tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha amemtaka Mkurugenzi, uongozi wa kata, na uongozi wa mtaa wachukue hatua mara moja kuhakikisha zoezi hilo haliendelei kufanyika na pia uongozi wa shule kuweka walinzi.
0 comments:
POST A COMMENT