Breaking News: Rais Magufuli Ateua Mkuu mpya wa Majeshi Tanzania...Mwamunyange astaafu. | KINGAZI BLOG

HABARI KARIBU YAKO ZAIDI.

Breaking News
Loading...

Friday, 3 February 2017

Breaking News: Rais Magufuli Ateua Mkuu mpya wa Majeshi Tanzania...Mwamunyange astaafu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, leo Tarehe 02 Februari, 2017 amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.

Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Major Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

02 Februari, 2017


google+

linkedin

About Author
  • BLOG NAMBA MMOJA KWA MATANGAZO YA AJIRA NA NAFASI ZA KAZI TANZANIA. Soma zaidi

    0 comments:

    POST A COMMENT

     

    Gallery

    Popular Posts

    About Us