Mwanamuziki Diamond Platnumz amezidi kufanya vizuri katika tasnia ya muziki barani Afrika na nje ya Afrika ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wasanii wengi wakubwa wanaozidi kumuongezea mashabiki katika mataifa mbalimbali.
Hivi karibuni Diamond alipotoa video ya wimbo wa Marry You alimshirikisha mwanamuziki Ne-Yo kutoka nchini Marekani aliuweka katika akaunti yake mpya ya Youtube ambayo ipo chini VEVO.
Diamond ni miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye akauti ya VEVO ambapo wanalipwa kutokana na matangazo yanayowekwa wakati wa kutazama video na pia kulingana na idadi ya watazamaji.
Diamond Platnumz ameeleza kwanini alichelewa kujiunga na huduma VEVO na kwanini sasa hivi amejiunga nayo. Kupitia ukurasa wake ameandika;
Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo Vevo… Nikawambia: “uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida.. Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo…na mbali tu ya kumlipa VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo”…..hivyo nikawambia: “siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida….
SABABU YA KUYASEMA HAYA:
Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa
Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu, vilevike umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichkua juu ya sanaa zetu kwa sasa, maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae… nafaham wasanii wengi hawakuwa wakilifaham hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…” kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh…🙏 -SIMBA #MALENGO
0 comments:
POST A COMMENT